Sunday, May 24, 2009

TUNATAKIWA KUZAANA KWA WINGI!

Tusingekuwa tunakufa tusingepata mahali pa kukanyaga




Nilipoandika kuhusu ongezeko la watu na uharibifu wa mazingira nilipata changamoto kadhaa kutoka kwa wasomaji wengi walinitumia email wakipinga au kuunga mkono hoja yangu.
Hata hivyo ni lazima nikiri kuwa maoni yaliyotolewa na msomaji wa kibaraza hiki aitwae Chacha aliyeko Musoma yalinivutia sana ikabidi niendelee kufanya utafiti juu ya jambo hili. Ili kujiridhisha ilibidi nizame katika makataba ya mzee mkundi huku nikisaidiwa na mtandao.
Katika utafiti wangu nimekuja kugundua kwamba kumbe idadi ya watu waliowahi kuishi hapa duniani ni kubwa ukilinganisha na idadi ya wale waliopo leo.
Kwa mujibu wa tafiti mbali mbali zilizowahi kufanywa imebainika kwamba ni asilimia 30 tu ya watu wote wamewahi kuishi hapa duniani.

Pamoja na ongezeko kubwa la idadi ya watu katika kipindi cha karne moja iliyopita, bado inaonekana kwamba watu waliowahi kuishi hapa duniani ambao sasa ni marehemu ni kubwa kuliko ile ya watu walio hai sasa hivi, hiyo ni kwa mujibu wa tafiti mbalimbali zilizofanywa mwaka 2002, mojawapo tafiti hizo ni ile ya mtaalamu wa idadi ya watu aitwae Carl Haub alifanya.

Mtafiti huyo aliangalia mabadiliko ya idadi ya watu kutoka kizazi kimoja hadi kingine akizingatia mabadiliko ya mazingira, uchumi na matatizo ya uzazi na vifo.
Akifanya utafiti wake kwa kuanzia kipindi cha Adam na Eva, kilichoanza miaka 50,000 kabla ya kuzaliwa Bwana Yesu Kristo. Kumbe Adam na Eva walikuwepo hapa duniani miaka 50,000 kabla Yesu hajazaliwa.
Ingawa sina uhakika miaka hiyo ilipimwa kwa kalenda gani, lakini hilo tuachane nalo.

Kwa kuangalia tafiti nyingine zilizofanywa imebainika kwamba, tangu kuumbwa kwa binadamu wa kwanza, dunia imewahi kukaliwa na watu zaidi ya bilioni 105. Hii ina maana kwamba idadi ya watu walioko duniani hivi sasa ni asilimia 7 tu ya watu ambao waliwahi kuishi hapa duniani.

Hivi kama ingekuwa hatufi ingewezekana vipi watu kuishi hapa duniani hivi sasa? Je ni mpango wa Mungu ili kuepusha watu kufurika hapa duniani na kuhatarisha uwepo wake?
Kwa mujibu wa takwimu za umoja wa mataifa zilizotolewa hivi karibuni, kuna idadi ya watu wapatao Bilioni 7 hapa duniani .
Cha kushangaza Umoja huo wa mataifa unapiga kelele watu wapunguze kuzaa watoto wengi, ili kuepukana na uharibifu wa mazingira.
Hivi ingekuwa hatufi, ingewezekana vipi watu bilioni 105 hapa duniani ilhali watu bilioni 7 tu, wanatishia usalama wa dunia?

Hata hivyo kuna jambo moja ambalo Umoja wa Mataifa umeshindwa kulibaini. Kwa mujibu wa takwimu za hivi karibuni zilizofanywa katika nchi za Ufaransa na Japani, imebainika kwamba nchi hizo nikama vile hawazaani, kwani idadi ya wanaozaliwa na wanaokufa iko karibu sawa (Zero Population) na wazee wanazidi kuongezeka katika nchi hizo, lakini bado Umoja huo wa Mataifa wanahimiza watu kutozaana kwa wingi.

Huko nyuma watu walizaana bila hofu na masharti, na ndio sababu idadi ya watu ilikuwa ikiongezeka kadiri miaka inavyokwenda, lakini siku hizi watu wanazaliwa kwa masharti.

Wakati omoja wa mataifa ukipiga kelele tupunguze kuzaana, na hapo ndipo tunaposhuhudia idadi ya vifo ikiongezeka kila uchao, utasikia mara tetemeko la ardhi limeua watu 3000, mara ajali ya ndege, mara ajali ya treni, mafuriko, magonjwa ya mlipuko, vimbunga, nakadhalika nakadhalika.
Na hapo tena tunasikia watu wakipiga kelele, jamaniee….. vifo vimezidi, watu wanakufa!!!????

Tunasahau kuwa ili dunia iendelee kuwepo ni lazima watu wazaane na nilazima watu wafe, huo ndio mfumo wa kuwepo dunia hii tunayoishi.

4 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kuna wakati yatubidi tuangalie tunaambiwa nini na nani na ili kiwe nini. Kwa mujibu wa takwimu, ili jamii iweze kujihakikishia uwepo wake miaka 25 ijayo, inastahili kuwa na wastani wa uzazi wa watoto 2.11 kwa kila familia. Ikishuka mpaka wastani wa watoto 1.9 kwa familia inakuwa ngumu kuutunza uzazi huo na ikishafika asilimia 1.9 kwa familia basi jamii hiyo itapotea muda si mrefu.
Wenzetu wameshtuka sasa maana kwa takwimu za mwaka 2007 zaonesha kuwa wastani wa uzazi huko Ulaya ni mdogo na sitoshangaa kama wataanza kampeni za kuwataka watu kuzaliana zaidi.
Lakini pia tugeukie upande wa pili. UPANDE WA "KIFUATACHO".
Kuongeza idadi ya uzazi ama watoto si kazi kama ilivyo kukifanya kizazi hicho kuwa chenye mafanikio na manufaa kwa uwepo wake.
Kwa hiyo kama kuongezeka kwa jamii ndiko huku ambako hakuipi jamii nafasi ya kuweza kujiendeshea maisha yao kwa haki na mafanikio, basi ni afadhali kuwa uzazi mchache maana kuzaa sana ni kuwapa mateso.
Nawakilisha

Koero Mkundi said...

Kaka Mubelwa Nchi zetu hizi za Afrika hazina utaratibu mzuri wa kuwatunza wastaafu, usipozaa kaka yangu umekwisha.
Utanyanyasika na watoto wa ndugu zako, wewe waige tu hao wazungu wanoendekeza ndoa zisizo na matunda yaani watoto.
Sikutishi ila chunguza maisha wanaoishi wastaafau huku nyumbani, yanatisha.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

acheni mambo ya ajabu. maumbile yaliumba na yanaumba na kuleta watu yakijua kabisa jinsi ya kuwalisha na kuwanywesha nyie hofu zenu za watakula nini ni za kiakili zaidi ya kiroho. kwani mazingira yanaalibiwa na ongezeko la watu au ujinga wa watu wanaofanya manyanga na kuharibu mazingira?

wingi wa watu sio noma wewe. uliwahi kwenda msituni? ukifika huko nyasi, miti na vitu kibao vimejazana sehem moja kama nini lakini ukiviangalia vinajitingisha na kufurahia maisha ile mbaya bila malalamiko, sasa unadhani wingi wa watu unashida gani?

HII YA KIROHO ZAIDI; bindamu hawaongezeka wala hawafi bali hubadilisha tu miili na kuvaa mingine, wapo, walikuwepo na watakuwepo. soma zaidi juu ya re-incarnation uone.

Yasinta Ngonyani said...

kwa kweli ingekuwa shida kama tusingekufa. Lakini sasa kuna uwezekanao kutakuwa hakuna watu baada ya miaka. kwani watu sasa wanazaa kwa mahesabu.