tag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post3627098817874611975..comments2023-11-02T14:36:01.744+03:00Comments on Vukani: WAMALAWI NA NDOA ZA VIBINTI!Koero Mkundihttp://www.blogger.com/profile/07548301751725756059noreply@blogger.comBlogger15125tag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-53259618845550244382010-04-07T19:13:07.563+03:002010-04-07T19:13:07.563+03:00Ndugu usiye na jina, maoni yako yatanifanmya leo n...Ndugu usiye na jina, maoni yako yatanifanmya leo nisilale kabisa kwani nishapata mada hapa ya kuandika.

Nimefarijika sana kuona kwamba umefurahishwa sana na kile ninachoandika humu japo kuna wanaoniona kama napoteza muda kwa kupiga taralila.

Niliwahi kusoma mahali kuwa moto uliosababisha chama cha KANU kule kwa majirani zetu nchini Kenya kuondolewa madarakani uliwashwa na Wanablog wa Kenya na hiyo ndio ikawa chachu ya kile kilichotokea nchini Kenya.

Ingawa kulitokea rabsha za hapa na pale lakini mpaka leo hii wengi mtakuwa mashahidi wa kile tunachokishuhudia nchini Kenya, wenzetu wameipigania katiba mpya kwa nguvu zote na sasa wako katika hatua za mwisho kukamilisha mchakato….tuwaombee matakwa ya wananchi walio wengi yasikilizwe.

Lakini tofauti na hapa nchini kwetu, kuna matatizo ya mwamko wa watu kufuatilia habari za mtandaoni, sijui ni ukosefu wa ufahamu walionao wananchi walio wengi au nikutokana na kufinywa kwa teknolojia kutowafikia watu wengi hasa wa vijijini.

Tatizo lingine ni wachangiaji wengi kukimbilia kumjadili mtoa mada badala ya kujadili mada husika, hili ni tatizo kubwa ambalo kama mtu huna moyo kama wa mwendawazimu basi unaweza kuacha kublog na kukaa kimya,. Lakini kwa nini ukae kimya ilhali wapo watu wengi kwa maelfu ambao hunufaika na huu ujinga wetu humu?

Kwa nini mtu ambaye amesheheni mizigo yake kichwani akusababishe uache kutumia kipaji ulichopewa na Mungu tena bure kuwaelimisha watu na kuwakumbusha wajibu wao.

Kuna changamoto nyingi sana zinazotukabili sisi wanablog, na tunachohitaji ni wachangiaji kama wewe ambao mnasoma mada na kuijadili kwa misingi ya kuamsha ari na shauku ya kuhoji kule haki zetu zilipofichwa na watu wachache ambao wametumia hila na ghilba kuingia madarakani.

What is ushindi wa kishindo? Kwa kutumia pesa za walipa kodi kuwalaghai watu ili kupata madaraka na kwa sababu ya ukosefu wa utambuzi walionao wananchi walio wengi hususana wa vijijini, halafu unapita na kukenua meno eti umepata ushindi wa kishindo.!!!!

Ngoja niishie hapa maana hii inahitaji mada inayojitegemea……Koero Mkundihttps://www.blogger.com/profile/07548301751725756059noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-22689253132819185192010-04-07T18:45:02.942+03:002010-04-07T18:45:02.942+03:00Dada Koero na wengine, mnaweza kutumia tuu hiyo qu...Dada Koero na wengine, mnaweza kutumia tuu hiyo quote..haina shida maana ni mawazo tuu.

Ukweli ni kwamba kama uko timamu Tanzania yetu itakuuma inavyoendeshwa na wale tuliowapa dhamana. Lakini tusiishie kuumia, lazima tuchukue hatua za kuibadilisha. Play your part. It can be done. Usimwangalie mwenzako. Its you! Naamini TANZANIA itabadilika kama watu tukitambua kwamba sisi ndo kiini cha mabadiliko. Kama mpiga kura, I ALWAYS believe mabadiliko yatakuja kwa njia ya amani and we can do that.

Kipindi cha kusingizia umasikini, ujinga nk..kimepitwa na wakati. We have to wake up and take full responsibility of our lives. Kwa nini lakini tunapenda mkato? kwa nini tunapenda kuonewa huruma? I believe Africa we aint genetically inferior kama wazungu baadhi wanavyoamini. Lakini matendo yetu na imani zetu zinatufanya tuonekane hivyo! Tutaendelea kurithishana umasikini mpaka lini? Naomba kila mtu ajiulize hili swali. Tangu uhuru..tunapigana na ADUI wale wale WATATU. Ujinga, Umaskini na maradhi! Imagine..next year we cerebrate HALF A CENTURY of INDEPENDENCE. What have we got to show for it? Inauma!

Mimi napenda kusali, lakini kamwe siamini kwamba Mungu atatuondolea matatizo yetu kwa kuomba. Rather, naamini Mungu atabariki juhudi Zetu kama tukifanya kazi inavyotakiwa! Huwezi kuiba/kufisadi hela ya kununua mitambo ya umeme, harafu unategemea kwenda kanisani Mungu akupe mvua! Jamani, why do we misuse our GOD?

Nitajitahidi kuwa nachungulia kwenye hii blog. Nimeipenda.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-43520127218315885822010-04-07T17:13:30.358+03:002010-04-07T17:13:30.358+03:00Mpangala, Wakunyumba! Nimekupata na Patriot yako! ...Mpangala, Wakunyumba! Nimekupata na Patriot yako! hata hivyo nimekusoma zaidi kupitia mtandao mwingine, na ni nimemezeshwa ufahamu wa kutosha juu yako. Nakupa Big Up. I apologize 4 my scud! By the way! natamani sana Likungu, Mbasa, Mbufu na Mbelele, mzee!Jacob Malihojahttps://www.blogger.com/profile/09736640059216467240noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-6850276969706398182010-04-07T14:42:40.058+03:002010-04-07T14:42:40.058+03:00@Koero; hata mimi nimedhamiria kutumia maoni ya An...@Koero; hata mimi nimedhamiria kutumia maoni ya Anony huyo, kwahakika ni kichwa safi. Lakini ukiniambia nisubiri pambio nitakwamba UNAWAZA NINI?

Hii ndiyo raha ya kujadili mambo yanachangamsha raaaaaaahhhhhhaaaa halafu unaongezea na Bakurutu ukinesanesa....

Natamani mjdala huu urudi tena kiambazani hapo au tuletee kingine chenye maudhui hayo tukijadili. Ndiyo uhuru na hatuvunji NYUMBA tunabomoa MLANGO tu. Mwenyekiti naomba kuiba maoni ya Anony huyo na ninaungaisha na ile mada yangu ya NAMJADILI KOERO J. MKUNDIMARKUS MPANGALAhttps://www.blogger.com/profile/11499845930276191685noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-13216794683877707742010-04-07T09:05:21.485+03:002010-04-07T09:05:21.485+03:00Mwe! naona mjadala umefikia patamu, hebu ngoja nim...Mwe! naona mjadala umefikia patamu, hebu ngoja nimnukuu Annony wa tarehe 5 April 2010,

"Tatizo kubwa kwetu sisi waafrika popote tulipo...tunapenda kuwalaumu wengine kwa matatizo yetu. Ukiangalia kwa kiundani..hawa hawa unaowaonea huruma..ndo kesho utakuta wanaandamana kuipigia kura CCM! Sasa jamani..hivi mnategemea ukombozi wa mwafrika utatoka wapi? Mwenyezi MUNGU ALITUPA UTASHI lakini tunashindwa kuutumia. Do you really think Kikwete gives a damn to a dying villager down in Kwimba au Kigoma? only when he needs their votes!"

Mwisho wa kunukuu.

Mwenzangu hapo umenikuna maana maoni yako ni makala tosha. Naomba uniruhusu niyatumie katika makala yangu ya Kisiasa ambayo iko jikoni.
karibu sana VUKANI.Koero Mkundihttps://www.blogger.com/profile/07548301751725756059noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-62538716967251657262010-04-06T20:48:54.419+03:002010-04-06T20:48:54.419+03:00Kaka Jacob Malihoja,
umenigusa sana na suala la u...Kaka Jacob Malihoja,
umenigusa sana na suala la umri wangu,na hongera kwa kuwa na miaka 38,NASHUKURU KUKUBOA TENA SANA.
nataka kukufafanulia kitu ambacho naamini hujakifahamu.

1. CHIPITA= ni kitu kinachopita.
2.CHAPITA= kitu kinachopita
3.CHIDAPITA=kitu kilichopita.
katika maoni yangu ya kwanza mwishoni nimeandika N'SAMBE N'NUNGU HAO NDO AMAI ABINGU WA MUTHARIKA.

yaani tuombe Mungu hao ndiyo akina mama wa Bingu wa Mutharika.

KUBLOGU HADI kuchoka ni kwamba haya mambo hayatakiwi tu kuzuka na kuyaandika sote tunatarajia kuona uhalisi unajadiliwa kwa kina na kuelezwa, hivyo kublogu hadi kuchoka kwani kuna mambo yanachekesha kwahiyo nayachukulia kama mzaha,
msingi wa kutenda ni uhitaji wa matendo ya mhusika. Huwezi kusema kwamba neno la mungu ndilo lilikosekana kwa hao watu kwa kujiangalia kwamba kwakuwa unalielewa na kulijua zaidi basi na wengine watashiriki.
NAACHA.....
soma maoni ya CHACHA na kile chama anachotania cha Da' Koero na Yasinta, ndipo utaelewa ninachoamini.
NIELENDELEE AU?
ni suala la fikra huru siyo kwamba nijiingize katika imani ambazo naamini kuwa suala la utetezi wa wanawake basi biblia ndiyo inanukuliwa kuhalalisha ukandamizaji wa wanawake.
Neno la mungu linasemaje katika huku ya adam na eva? AU nakosea na labda Mfalme Costantine na wenzake walichomokea halikuwa neno la mungu?
VIPI?
inawezekana suala la umri nalo ukaliona ni sababu ya mimi kuandika hayo, nakupa pass mark

Sula la mke wangu linakujaje hapa? ndiyo kujadili hoja huko? jadili mambo, jadili SERA ZA UKWMUAJI WA HAYA SIYO MALALAMIKO YASIYOKWISHA, mimi nasema suala la imani na utashi wa wanadamu siyo kila jambo linahitaji Mungu.

Ukishajua mke wangu....nini kitafuata?
NAMALIZA KWA KUCHEKA SANA.....
halafu...samahani mwenyekiti Koero kwa mcharazo ufuatao maana vikombora vya kufyatua matofali ya ubepari yamefika hapa.

SERA ZANGU KWA WANAWAKE.
tufanye nini tunapojadili hapa? Maana CHACHA ameshasema WOMEN CRYING EVERY DAY.

Leo nikae chini nikubali kuharibu katiba ya nchi ili kuweka uwiano sawa 50/50 kwa kusudio la upendeleo?
Ni nani alimpendelea mwanaume? SISI WANAUME NI WAJINGA?
JE HAO WAZEE NI WAJINGA? WAKENYA WANASEMA HIVI; MANENO MINGI KASI NDOGO
SI TUNAJUA UZEE NI BUSARA? UNAFIKIRI NI NINI KILICHOKOSEKANA KWA HAYA YOTE? MUNGU? atufanyie nini tena kwa miaka yote hii jamaniiiiii? tunamlilia kwa mambo mengine ambayo yanasbabishwa na watu ambao wamekosa kitu kidogo sana UTAMBUZI ndiyo maana nasema nawafahamu WAMALAWI siyo kwa kusimuliwa bali kwa kuishi na kuona ukiniambia suala la mungu Malawi nitakwambia nchi hiyo ni habari nyingine... tusiambukizane masikitiko...
HAPANA...
binadamu wana kawaida ya kujitisha, na kila wanachokiona wanajitia hofu, hilo ni anguko la kwanza. Pili tunatanguliza vikwazo ili tushindwe halafu tumuombe mungu.
Majuzi niliambiwa niende kwenye mkesha kuombea amani ya nchi.
NILICHEKA... na labda umri wangu ndiyo unanifanya nicheke..

WALIWAZA NINI HAWA KUOMBEA AMANI? ndiyo ushuhuda??
Nani anawapigia kura wanaoharibu amani?
Nani anawapa mamlaka wale wanaoanzisha asasi za kutetea wanawake, lakini hawafanyi hivyo.
AFADHALI KOERO WANGU ANAANDIKA KATIKA BLOGU NA KWA KUJITOLEA BILA MALIPO.... lakini nini wanachokifanya wale ambao wanafanya hayo kwa kulipwa pesa halafu wanashupalia habari za Mahita kuzaa na hausigeli

soma upya kwangu mimi ulishaisha zmaana ndiyo maana niliamua KUMJADILI KOERO MWENYEWE katika blogu yangu na nitafanya hivyo siku zijazo navuta pumzi..
wakati mwingine nichukulie tu vile unavyoamini na kujitisha kwa hofu... kumbuka nimeitwa jina la MCHARUKO kwasababu ya maoni yangu bloguni

umri wangu utaupata hapa ukinibipu ; lundunyasa@yahoo.com au jikomboe@gmail.com.

ASANTE KWA KUNISOMA; HII NI INJILI ILIVYOHUBIRIWA NA SHETANI MARKUS MPANGALA pale madhabahuni kwani asingelitambua dhambi kama Torati isingesema. na kwa umri wangu naenda kusikiliza WE MADE YOU ya EMINEMMARKUS MPANGALAhttps://www.blogger.com/profile/11499845930276191685noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-28506600620939904122010-04-06T16:44:50.463+03:002010-04-06T16:44:50.463+03:00Koero na wana blog wote ninawapa bigupp kwa michan...Koero na wana blog wote ninawapa bigupp kwa michango mbali mbali lakini Mpangala ameniboa na amenitia wasiwasi. Katika mchango wake wa kwanza Mpangala anakatisha anaposema blogger (Koero) angechoka kuandika, maana yake ni nini? Kwamba asingeandika haya aliyotuletea au asirudie tenaa, hapa sielewi! Sentensi ya kwanza ya Mpangala inanitia hofu sana, maana neno utajijuu, mara nyingi hutamkwa na mtu ambaye amefanya jambo sasa anajibishana na mlalamikaji juu ya jambo alilolitenda! Mpangala anawaambia Chipita (Kimsingi na walalamikaji wote) watajijuu! Natamani kujua umri wa Mpangala, na natamani sana kujua umri wa mke wake kama ameoa! Kwasababu utajiju ni neon linalopendwa sana na kundi Fulani katika jamii yetu, na Maana ya neon hilo hasa hasa ni kwamba “ndio nishafanya utajijua mwenyewe”, au “ndio ishakuwa utajijua mwenyewe”!

Kwenye maoni yake ya pili, akijibu wazo la Bwana True Faith, Mpangala ameponda imani, yaani ameponda kabisa mchango wa kiroho katika kuttua matatizo ya kijamii! Hii pia imeniogopesha na kunishangaza. Kimsingi hata kama haamini Mungu lakini ukweli unabaki palepale mwenye elimu ya imani ya kiroho hawezi kufanya ushenzi kama huo. Lakini jambo lingine ni kwamba blog ni sehemu ya kubadilishana mawazo na kuonyesha hisia za kila mmoja. Lakini ni mahali ambapo kwa namna moja au zaidi kuna mmoja wa wasomaji anaweza akayafanyia kazi anayoyasoma, na yanayoendana nay eye au anayoyaweza.

Kwahiyo kama Mpangala anaona hana analoweza kuchangia kuhusu mambo ya kiroho akae kimya asiponde mchango wa wenzake. Pengine msomaji mmoja anaweza kwenda kuendesha elimu kubwa ya kiroho na mamo yakapungua huko! kama wewe unaweza kuishawishi Serikali kupeleka elimu fanya hivyo, anayeweza kushawishi polisi kukamata na kuwapeleka katika mkondo wa sheria, na afanye hivyo, anayeweza kushawishi watu wa imani wapeleke mafunzo ya kiroho na afanye hivyo. Huyu akipunguza wawili, huyu akipunguza kumi, huyu akipunguza watano kupitia njia anayoijua mwisho wa siku watu wengi wataondokana na ushenzi huo.

Kila mtu mchango wake unaweza kufanyiwa kazi kulingana na aina ya wasomaji wa mchango ambao mtu anautoa.

Hakuna vita inayotumia aina moja ya silaha.Jacob Malihojahttps://www.blogger.com/profile/09736640059216467240noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-86949992721610273632010-04-06T12:01:51.807+03:002010-04-06T12:01:51.807+03:00Malawi...kama Tarime... :-(
Hivi ile NGO ya Koero...Malawi...kama Tarime... :-(

Hivi ile NGO ya Koero na Yasinta inayoitwa Women Crying Every Day inafanya nini jamani? lol

Men RISE up!o'Wambura Ng'wanambiti!https://www.blogger.com/profile/17146066311562834541noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-38610648455928312352010-04-05T15:12:07.289+03:002010-04-05T15:12:07.289+03:00alafu ooh binadamu ni kiumbe mwenye akili kuliko v...alafu ooh binadamu ni kiumbe mwenye akili kuliko viumbe wengine. kwa hili i think we are more animals than humans. mwanamke aliyepevuka kibaolojia (na kiakili) anafaa kuolewa na mwanaume anayempenda au waliyependana. hili la kubambikiziwa babu kizee mie simo, mchanga wa pwani huooo.John Mwaipopohttps://www.blogger.com/profile/11708584279197669683noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-25581604231640419252010-04-05T01:19:28.308+03:002010-04-05T01:19:28.308+03:00Dada Koero, leo ni siku ya kwanza kukutembelea hum...Dada Koero, leo ni siku ya kwanza kukutembelea humu. Nimeipenda sana blog yako. Nimeona umeandika sana kuhusu madhira ya mama zetu. Dada Koero mimi nakuunga mkono, maana I have lived this life. So I know it.

Swali langu kwako na wanawake wengine ni hili: Je ni kipi kifanyike KUPUNGUZA maana KUONDOA hii hali ni vigumu. Inaonekana wengi tunaliona tatizo na tumeishi na haya matatizo, lakini wote tunasema ni serikali ndo yenye jukumu! Mi nadhani we should be the change we seek!

Tuanze na jukumu la kuchagua viongozi responsible na tuwawajibishe. Leo hii CCM akijua kwamba hana majority bungeni ya kupitisha sheria anazozitaka kwa manufaa yake......trust me ..atakuwa na adabu jinsi anavyotuongoza, perhaps hela za ufisadi angeziweka kwenye mipango ya kuwawawezesha na si kuwasaidia hawa akina mama na wananchi kwa ujumla....

Tatizo kubwa kwetu sisi waafrika popote tulipo...tunapenda kuwalaumu wengine kwa matatizo yetu. Ukiangalia kwa kiundani..hawa hawa unaowaonea huruma..ndo kesho utakuta wanaandamana kuipigia kura CCM! Sasa jamani..hivi mnategemea ukombozi wa mwafrika utatoka wapi? Mwenyezi MUNGU ALITUPA UTASHI lakini tunashindwa kuutumia. Do you really think Kikwete gives a damn to a dying villager down in Kwimba au Kigoma? only when he needs their votes!

Hapa tutakuja na excuse kibao..kwamba watu tunachagua viongozi wabovu kwa sababu ya umasikini, lakini tunashindwa kugundua kwamba..Politics is everything! whether you are in America or in poverty stricken Tanzania.

Narudia tena, waafrika..viongozi wetu wanatuchukulia for granted. Na sisi tumeridhika na hii hali.Na sisi tumekubali.. Hata the so called "elites"..ndo wanatuangusha..maana wakisha "toka" imetoka hiyo.....Hawaangalii nyuma....zaidi ya "kuwaonea huruma" waliobaki huko nyuma...

My take: Watanzania tuamke, tuchukue jukumu la maisha yetu. Tuache kumsingizia Mungu wala mwingine. HAITUSAIDII KULAUMU.

Dada Koero, Trust me..leo hata ungeteua 70% ya wabunge wote wakawa wanawake...hali za mama zetu hazitabadilika! Tunahitaji kubadilisha mfumo wa jinsi tunavyojitawala au tunavyotawaliwa. Imagine...mpaka leo hatuna umeme wa kuaminika..lakini hebu jiulize..tangu JK aingie madarakani..tumelipa mabilion mangapi kwa makampuni ya umeme hewa? and guess what? Everybody is quite! and in October we will vote in masses for the same messy!

Ofcourse, CCM siyo tatizo letu pekee..lakini..wakijua kwamba hata wananchi wanafikiria..hali itabadilika. For now..they know..they can do anything and go away with it. Mimi kiukweli...I get the feeling labda..ngoja umasikini uzidi kutuchapa weeeee (zaidi ya huu tulionao sijui itakuwaje ;-)...labda iko siku tutaamka na kuona kwamba we can influence things through the ballot!

Waungwana naomba nisiwachoshe..lakini..mimi kiukweli nchi yangu na wananchi wenzangu wananisikitisha sana...Tunashindwa kufanya maamuzi magumu kwa manufaa yetu na watoto wetu. Umasikini na hali ngumu zinazowakabili mama na baba zetu utaendelea kudumu daima. Mpaka tutakapoamka na kusema INATOSHA!

God bless you all.Anonymousnoreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-6624176898183693562010-04-04T20:06:49.965+03:002010-04-04T20:06:49.965+03:00Mungu ili afanyeje? yaani tukeshe makanisani na mi...Mungu ili afanyeje? yaani tukeshe makanisani na misikitini tukiimba PAMBIO kwamba Mungu awanusuru watu hao wakati alitupatia hekima na akili?

Huu mzaha, fanyeni utafiti siyo kulishana masikitiko. ha ha ha ha ha ha, Munguuuuu afanyeje? Neno la Mungu????????????????????????????????????????????????????????????????????????????
Yaani tumefikiria weeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee tumeshindwa kisha tunamrushia Mungu. Haya ni mambo ya imani siyo kujadili hojaMARKUS MPANGALAhttps://www.blogger.com/profile/11499845930276191685noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-31934433448093993272010-04-04T14:40:31.527+03:002010-04-04T14:40:31.527+03:00Inasikitisha sana! Hii yote ni kwa sababu ya kutom...Inasikitisha sana! Hii yote ni kwa sababu ya kutomjua Mungu. Watu kama hawa wanapaswa kufikiwa na Neno la Mungu wa Kweli.Anonymoushttps://www.blogger.com/profile/00702934370622838035noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-4296698694373363262010-04-04T13:14:40.002+03:002010-04-04T13:14:40.002+03:00Nimesoma habari hii nikiwa na masikitiko sana. Ni ...Nimesoma habari hii nikiwa na masikitiko sana. Ni jambo la kushangaza sana kumlazimisha binti aolewe na mwanamume ambaye ni sawa na babu yake kabisa. soma hhapa niliwahi kuweka makala kama hii pale kwangu. http://ruhuwiko.blogspot.com/2009/11/mwanaume-wa-miaka-112-amuoa-binti-wa.htmlYasinta Ngonyanihttps://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-90996010215040821622010-04-03T19:28:24.684+03:002010-04-03T19:28:24.684+03:00ha ha ha ha hawa CHIPITA FORUMS sijui CHAPITA FORU...ha ha ha ha hawa CHIPITA FORUMS sijui CHAPITA FORUMS au CHIDAPITA FORUMS. watajijuuuuuu.

NINA HAKIKA UNGEFANIKIWA KUISHI NA JAMII ZA WAMALAWI UNGEBLOGU HADI KUCHOKA AU UNGEANDIKA KIBATU CHENYE KURASA ELFU KADHAA,
nawaelewa we acha tu.

NSAMBE N'NUNGU, hao ndo AMI ABINGU WA MUTHARIKAMARKUS MPANGALAhttps://www.blogger.com/profile/11499845930276191685noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-39364109415349101432010-04-03T17:31:13.954+03:002010-04-03T17:31:13.954+03:00Nampa pole huyo binti pamoja na wengine wote wanao...Nampa pole huyo binti pamoja na wengine wote wanaokumbwa na madhila kama haya.

Jamii hii inahitaji elimu ya ziada ili kuiepusha na mawazo potofu ambayo wao wanaona ni maisha ya kawaida kabisa. Nasema maisha ya kawaida kwa kuwa yawezekana hata kuna baadhi ya mabinti ambao kwa namna moja ama nyingine huwa wanafurahia baadhi ya mila hizi au zote kabisa kwa sababu ya kutokuwa na namna mbadala ya kufikiri kuhusu mila hizo kwa sababu ya wigo wa kimila unaowapelekea kufikiria kuwa utaratibu huo ni wa kawaida na muhimu katika maisha yao.Wanaharakati wengi zaidi wanahitajika ktk eneo hilo ili washirikiane na waliopo ktk kuinasua jamii hii kwenye hali ya upofu waliyo nayo. Kuna jamii nyingi kama hizi Africa na ni jukumu letu sote kukabiliana na mila na tamaduni chafu kama hizi.Sote wenye nia njema tuwe wanaharakati.Albert Kissimahttps://www.blogger.com/profile/12931488222535021826noreply@blogger.com