tag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post4173130802508273532..comments2023-11-02T14:36:01.744+03:00Comments on Vukani: TAFAKARI YA LEO: WALIPOKUTANA WANABLOG HAWA, JE WALIPANGA AU ILIKUWA NI NASIBU TU?Koero Mkundihttp://www.blogger.com/profile/07548301751725756059noreply@blogger.comBlogger7125tag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-23924614728985555672010-07-09T17:08:01.240+03:002010-07-09T17:08:01.240+03:00Koeroooooooo!
Kudua na kugosha chedi nini? Nyika ...Koeroooooooo!

Kudua na kugosha chedi nini? Nyika na vome.....lol!o'Wambura Ng'wanambiti!https://www.blogger.com/profile/17146066311562834541noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-10785074036764406392010-07-06T11:11:39.124+03:002010-07-06T11:11:39.124+03:00mimi niekutana nao kadhaa ila nilishindwa kuwajuli...mimi niekutana nao kadhaa ila nilishindwa kuwajulisha. nilikutana na chacha, strictly gospel basikamala Lutatinisibwa Lutabasibwahttps://www.blogger.com/profile/06207381893940710959noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-73685144214355126812010-07-06T09:37:52.068+03:002010-07-06T09:37:52.068+03:00Hodi hodi uwanjani,
Nami niyaseme haya mdomoni,
Ko...Hodi hodi uwanjani,
Nami niyaseme haya mdomoni,
Koero wetu yungali gizani,
Sasa anataka kutoka kizani,
Nami nina msaidia.

Nimeanza hivyo, mama mchungaji, Markus kajibu kuwa haikuwa nasibu. Haya mambo yalianza Jumamosi ya tarehe 8 Mei mwaka huu huu majira ya saa moja unusu jioni. Niliongea na Kaluse akaniambia kuwa amezungumza na Chacha kuwa anatarajia kuwasili Dar siku iliyofuata.

Nikampigia simu Chacha. Tukakubaliana nitampokea airport Jumapili mchana. Ilikuwa rahisi kwa kuwa tumekuwa na mawasiliano siku nyingi kiasi kabla.

Tulipokutana, tukaenda one way Movenpick, tukakutana na Kaluse.

Ukawa mwanzo mzuri kwani tuliweza kukutana mara mbili zaidi na Chacha na ukawa mwanzo mzuri wa kukutana mara kwa mara na Kaluse maana sasa hihesabiki tumekutana mara ngapi.

Baada ya hapo nikapata simu kutoka kwa kaka Chib anakuja Dar. Hapo tukapanga sasa kuwa hiyo tarehe 15 Mei tukutane palepale saa nne asubuhi.

Wakati huo huo kaka Kaluse akawasiliana na Markus. Mi sikuwa na namba ya bloga yeyote zaidi ya kaka Chacha na kaka Chib. Tulipokutana kaka Kaluse akanipa namba yako mama mchungaji, nikakutumia ujumbe, sijui kama uliupata maana siku tukikutana hilo ndilo shitaka la kwanza kwako.

Akaja kaka Markus (shemeji yangu huyu siku hizi).

Baada ya hapo nimekutana na kaka Chacha, Markus na Kaluse mara chungu mbovu. Ndivyo mwanzo wa urafiki ulivyo.

Sisi tulidhani na bado tunaamini huu ni mwanzo mzuri wa kuwa na ushirikiano zaidi ya jina. Na sasa, kama nilivyozungumza na kaka Kaluse, tunajipanga kuandaa siku ambayo tutaweza kukutanisha wanablog wengi waliopo hapa Bongo na wa Ughaibuni wanaokuwepo Bongo kwa wakati huo. Tunahitaji kukuza ushirikiano kwa kiwango kikubwa. Haya tunayoyaandika katika blog zetu yanagusa watu wa kada mbalimbali, hivyo ni lazima tuwe na ushirikiano wenye akili.

Kuhusu kaka Matondo, niliwasiliana naye. Amekwisharejea Amerika. Isivyo bahati kwake, alipatwa na msibwa. Hivyo siku zake hapa Bongo zilitawaliwa na shughuli za msiba na mambo yatokanayo na yaingilianayo na familia. Niliwasiliana naye wakati akiondoka. Alisikitika kuondoka vivi hivi pasi kukutana nasi. Panapo majaliwa, atarudi Bongo siku nyingine maana ndiyo nyumbani.

Maelezo ni mengi kweli hapa, kaka Markus ndo mtaalamu wa kuandika nonstop.

Tutakutana tena na tena. Ila sasa tunahitaji kupanua wigo wa kukutana kwetu.Fadhy Mtangahttps://www.blogger.com/profile/10322331153810581894noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-70366999765342566422010-07-05T10:53:28.281+03:002010-07-05T10:53:28.281+03:00Muwe mnauliza kwanza.Ninachoajua ni kwamba kila ki...Muwe mnauliza kwanza.Ninachoajua ni kwamba kila kitu kiliandaliwa na watu wawili yaani Shaban Kaluse na mtani wangu Fadhy Mtanga. Kwahiyo mkisema ni bahati mbaya ni lazima tujiulize ilikwuaje hata Yasinta kutoka Sweden akaunganishwa hapo? Ilikuwaje hata Mtakatifu Kitururu akaunganishwa kutoka Nairobi? Je mlisoma vema maelezo ya Fadhy kuhusu mjumuiko huo? nilitumiwa ujumbe saa tano asubuhi nikiwa katika ofisi yangu kwamba natakiwa kuhudhuria mkusanyiko huo. Je ilikuwa NASIBU? ni kwanini basi niatafutwe kisha kuitwa nami nikaacha kazi zangu hata nikajumuika? Tatizo ni ubinfasi na kudhani kwamba mikusanyiko kama hii ni kueleza kero na shida zetu. KUNA TOFAUTI KATI YA WIVU NA USONGO. Ilikuwaje hata baada ya mjumuiko safari ikaenda tabata? nadhani huu ni ukosefu wa taarifa waungwana. kuna kichwa kimoja SHABAN KALUSE kingeweza kwuaelezeni mengi kabla na baada ya hapo. na mara nyingi nimekuwa na mjumuikona Kaluse, na siyo NASIBU. kawaida ya NASIBU ni kujiaminisha kwamba ndiyo ukweli, na huwa unakuwa mbali na kitendo kwahiyo hata ukaambiwa Mzee wa Lundunya sana anahitaji kumpachika Mungu maswali unaweza kubisha! WAZO TU HILI NA RUKSA KULIBISHIA WAKUUUUUU tuachane na fununuMARKUS MPANGALAhttps://www.blogger.com/profile/11499845930276191685noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-23221371173594258472010-07-05T10:31:12.706+03:002010-07-05T10:31:12.706+03:00Kama walienda pale kila mtu kwa wakati wake bila k...Kama walienda pale kila mtu kwa wakati wake bila kujua nini kinaendelea bila mawasiliano yoyote, ila tu wakajakugundua kuwa wanafahamiana; basi hiyo ilikuwa bahati nasibu.

Ila kama kuna juhudi zilifanyika hata kwa 'kubipiana' tu kutafutana, basi nadhani ulikuwa ni mkakati wa makusudi kukutana na uliofanikiwa.

Ushauri wangu ni kwamba mfano waliouonyesha wenzetu hao, tuuige. Tuanze kutafutana na kubadilishana mawazo uso kwa uso. Inapendeza ati!Christian Bwayahttps://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-26181984913801752872010-07-04T12:22:35.646+03:002010-07-04T12:22:35.646+03:00Mama Mchungaji hongera kwa kuuliza swali swali zur...Mama Mchungaji hongera kwa kuuliza swali swali zuri!

Ukweli ni kuwa mambo mengine huwa hatuvipangi ila vinajitokeza automatically!

Mimi nimekutana na Prof. Matondo Arusha na kuteta naye kwa muda wa masaa kadhaa.

Labda papaa Fadhy atajibu.

Inaonekana una wivu sana ama gubu...lol!o'Wambura Ng'wanambiti!https://www.blogger.com/profile/17146066311562834541noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-70174714676978786382010-07-04T10:56:32.783+03:002010-07-04T10:56:32.783+03:00Nadhani ilikuwa bahati nasibu tu! Ngoja nami nije ...Nadhani ilikuwa bahati nasibu tu! Ngoja nami nije nikutane na mtu..lolYasinta Ngonyanihttps://www.blogger.com/profile/09314172793959023532noreply@blogger.com