tag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post7401792536194681232..comments2023-11-02T14:36:01.744+03:00Comments on Vukani: NIMEANZA KUZISHITUKIA HIZI DINIKoero Mkundihttp://www.blogger.com/profile/07548301751725756059noreply@blogger.comBlogger5125tag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-28442120892391089192008-12-31T17:18:00.000+03:002008-12-31T17:18:00.000+03:00Natamani ningekuwa wa kwanza labda ningewasaidia w...Natamani ningekuwa wa kwanza labda ningewasaidia wenzangu kufupisha maandishi. Lakini wamenitangulia na wamenisaidia mimi. Nashukuru kwa mtazamo wenu nyote na nimejifunza mengi. Kaka Fadhy, funga mwaka ya 08 naiona inanoga pande zte. Kila la kheriMzee wa Changamotohttps://www.blogger.com/profile/10491704592061579729noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-72574600759300157932008-12-31T15:41:00.000+03:002008-12-31T15:41:00.000+03:00Dada koero, kama unavyosema huu ni mtizamo wako na...Dada koero, kama unavyosema huu ni mtizamo wako na uko huru kusema chochote. Sio wakati wa kilichodhniwa kuwa ni ukweli kuwa na nguvu za hata juuwawa endapo utatofautiana nacho!

Kuna watu wachache wanaomiliki dini hizi kwa malengo yao. Kumbuka maandiko yanayoitwa matakatifu au matukufu, ni mitizamo ya watu na jamii Fulani. Kwa mfano biblia ni documentary ya maisha ya waislaer.

Kama ulivyosema tulichaguliwa kila kitu zikiwemo dini na ibada, shule nakadhalika. Dini zinatawaliwa sana na Ego kwamba kila dini mungu wake ni bora kuliko wa mwingine. Hata hivyo Mungu huyu anaonekana kutisha kuliko kuwa kimbilio letu. Cku ya mwisho yeye anamoto, majoka, nge, viboko nakadhalika.

Imegundulika kwamba binadamu ndiye anaye muumba Mungu na sio mungu kumuumba mwanadamu katika makanisa yetu. Kwamba ubongo ndio unaotengeneza kumbukumbu na kuzitunza na hivyo kumbu kumbu za mungu ziko kwenye Bongo za wanaomwamini!

Ukiangalia kwa kina mafundisho ya baadhi ya mitume kama Kristo yamepotoshwa kwa makusudi na yote yafyanywayo makanisani sio maagizo ya kristo bali ya wanadamu. Ulishawahi kusoma vitabu vya Lenin na mashoshalisti wengine juu ya ukristo na utumwa/ukoloni? Wizi mtupu
Umeongelea hawa majamaa wa mashariki. Kwa kweli dini zao zinaeleweka na zinaingia akilini kwa kiasi Fulani. kuna kitu wanakiita “science of the soul” wanasema hii ni sayansi pekee ya kumjua mungu(kama unamwita hivyo) kwani huwezi kumjua Mungu kwa kufanya scientific experiments za kawaida na ndio maana wanasayansi wetu wanakataa kwamba hakuna mumgu ila wanadai kuna nguvu

Wanasema huwezi kumuona Mungu kwa macho yako ya kawaida ila kwa njia nyingine ambayo wanajaribu kuiita jicho la tatu. Wanatumia sana kitu kinachoitwa ‘meditation’ na kinasaidia sana katika maisha yetu ya kila siku.,

Labda nikukaribishe sana kwenye madarasa yetu ya utambuzi.kamala Lutatinisibwa Lutabasibwahttps://www.blogger.com/profile/06207381893940710959noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-53128945318957661162008-12-31T13:22:00.000+03:002008-12-31T13:22:00.000+03:00Kuyajadili haya mambo ya dini ni jambo la msingi. ...Kuyajadili haya mambo ya dini ni jambo la msingi. Profesa Shayo aliwahi kusema dini ni ajali ya kijiografia. Mara nyingi mtu haamui ni dini gani awe nayo. Anarithi dini ya wazazi wake. Na inapotokea kuwa mtu anaongoka ukubwani, mara nyingi hufanya hivyo si kwa sababu ya uchambuzi wa kina wa dini husika. Lakini ajabu ni kwamba kila mwamini huamini kuwa dini yake haina matatizo, na kwamba dini nyinginezo zote zina mapungufu makubwa kiasi cha kustahili moto wa milele.

Nadhani, tunazo sababu nyingi kuzichunguza dini hizi. Tuzichunguze si kwa lengo la kuona ipi ni sahihi kuliko nyinginezo. Bali kujaribu kuona ikiwa nadharia za dini husika zina mantiki zinazoingia akilini ama la. Tuzichunguze kuona ikiwa kuna uhusiano wa namna fulani baina ya dini hizi (kama kuna namna fulani zinafanana hata kama zinajidai kukosoana) ama kuona ikiwa kila dini inaamini kitu chake tofauti na dini nyinginezo.

Kazi hii hatuna budi kuifanya. Kwa sababu tusipofanya hivyo tutaendelea kukaa katika kifungo cha fikra. Ni furaha yangu kuona kuwa Koero umejitosa katika mjadala wenye mwelekeo huu. Nitakuwa msatari wa mbele kukuunga mkono.

Katika kukuunga mkono, tuanze na SDA uliko sasa kinadharia: Unadhani kuna mapungufu gani ya msingi ya kiimani yanayokufanya ufikirie upya mahudhurio yako huko?

Mchango wa Evarist umeongeza ladha nzuri. Michango ya watu kama hawa inahitajika sana kwenye mijadala kama hii.

Evarest: Kulikoni, mbona safu ya Raia mwema ughaibuni hainokani siku hizi?Christian Bwayahttps://www.blogger.com/profile/13141394805539015266noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-82603727915894980772008-12-31T09:37:00.000+03:002008-12-31T09:37:00.000+03:00mmh...! nimeshusha pumzi kwa nguvu baada ya kuisom...mmh...! nimeshusha pumzi kwa nguvu baada ya kuisoma hii ambayo mi nimependa kuiita funga mwaka. ahsante da koero kwa kuleta changamoto. naomba usiache, kazi imesimama. ngoja nifanye tafakuri ya kufa mtu baada ya kusoma hapa.Fadhy Mtangahttps://www.blogger.com/profile/10322331153810581894noreply@blogger.comtag:blogger.com,1999:blog-7953064069616248417.post-66628404829232844992008-12-31T08:25:00.000+03:002008-12-31T08:25:00.000+03:00Mhhh...dada yangu hapo umeibua mjadala mzito na we...Mhhh...dada yangu hapo umeibua mjadala mzito na wenye manufaa kwa jamii.Mie ni Mkatoliki japo si mhudhuriaji wa kanisani (nasali nyumbani).Rafiki zangu wengi ni Waislam kuliko Wakristo,na hilo lilinisaidia kuujua Uislam kidogo.Kitabu nacho kimenifanya niuelewe kwa undani zaidi.Kwa kifupi,dini ni dhana complicated na contradictory mno.Lakini ninachoamini hadi sasa ni kwamba ili mtu awe muumini analazimika kuitazama dini yake kiteolojia zaidi kuliko kisayansi.Kwa vile msingi mkubwa wa dini ni imani (ambayo kimsingi ni kitu cha kufikirika zaidi kuliko uhalisia),uthibitisho (proof) katika dini ni mgogoro (eg Mungu yuko wapi?Mbinguni ndio mahala gani?nk)

Dini zetu za asili (ATMs) kwa kiasi kikubwa zilikuwa tofauti na hizi za kimapokeo (Ukristo,Uislamu,etc) kwa vile ziliyapa mazingira uzito mkubwa (eg mizimu katika milima au misitu inayoonekana) na pia nafasi ya mwanadamu katika u-mungu ilikuwa kubwa pia (eg nafasi ya mzimu wa babu ktk ukoo au kabila).

Kufupisha hoja yangu,naafikiana nawe kwamba dini za mapokeo zimetawaliwa na mambo kadhaa ambayo licha ya kukinzana na mafundisho ya dini hizo pia yanachochea mgawanyiko badala ya umoja.Ikumbukwe kuwa ni dini hizi ndizo zilizopigana vikumbo kupora waumini wa dini zetu za asili (japo hazijafanikiwa 100% kwani nafasi ya dini hizo bado ni muhimu kwa baadhi ya wakristo na waislam eg mambo ya mila,matambiko,nk).

Mjadala mzuri na unasaidia kupanua mawazo vya kutosha.Ni vema ukiuendeleza mwakani (well,kesho).

HERI YA MWAKA MPYAEvarist Chahalihttps://www.blogger.com/profile/08220429042701710191noreply@blogger.com