Friday, February 19, 2010

LEO TUJIFUNZE NAMNA YA KUOMBA MAJI KWA LUGHA ZA MAKABILA TOFAUTI TOFAUTI

Kina mama wakitoka kuteka maji kisimani

Ndugu wasomaji wa kibaraza hiki, leo nataka tujifunze namna ya kuomba maji kupitia lugha za makabila tofauti tofauti.

Hivi karibuni nilikwenda Wilayani Babati, kule nikakutana na watu wa kabila moja liitwalo Wasandawi, nilikuwa na kiu, lakini nilipata tabu sana kuomba maji maana lugha pekee ambayo nilitakiwa kuwasiliana nao ilikuwa ni Kisandawi, basi ilikuwa kaazi kweli kweli.

Kipare:
Nighenja mazi ya kunwa=Nisaidie maji ya kunywa

Kinyawezi:
Nalilomba minze kakunwa=Naomba maji ya kunywa

Kichaga:
Ngikundi Mringa= Naomba maji ya kunywa

Kingoni:
Nitangatilai manji mlongo wangu=Naomba maji ya kunywa ndugu yangu

Kimasai:
Njaaghe Ngare= Naomba maji ya kunywa

Kihehe:
Ndisuka Ululenga= Naomba maji ya kunywa

Kimeru:
Ngitelewa Mringa= Naomba maji ya kunywa

Kijaluo:
Miaa pi= Naomba maji ya kunywa

NIMEPATA MSAADA KWA MJUVI WA LUGHA YA KIJAPANI
Kijapani:
Kwanza inabidi useme:- 1. kao nodo itai - nina kiu

2. mizu nomu itai - nina hamu ya kunwya maji

Ukisha sema moja kati ya hayo hapo juu ndio unaunganisha na lingine kati ya haya hapa:-

1. omizu kudasai

2. omizu chodai

3. omizu onegai shmasu

Kihaya:
Ninshaba amaizi= Naomba maji ya kunywa

Haya wengine mtajazia hapo.

17 comments:

  1. Heee! wa msikana veve unileki hoi! Nimenukuu "Kingoni:
    Nitangatilai manji mlongo wangu=Naomba maji ya kunywa ndugu yangu"

    Pia unaweza ukasema nimwomba manji gakunywa.= naomba maji ya kunywa
    Na halafu Kimanda Nisuka manji gakunywa= Naomba maji ya kunywa

    ReplyDelete
  2. Kisukuma (Kinyantuzu) - Nalilomba minzi agung'wa au nagulombaga minzi agung'wa

    ReplyDelete
  3. Samahani hapo kwenye Kimanda nilikosema unajua kinafanana sana na kingoni Ni hivi Nisuka masi gakunywa. Na pia kwa kiswid ni:- Kani jag be att får ett glas vatten

    ReplyDelete
    Replies
    1. Dada Yasinta samahani naomba nikukosoe kidogo kwa kuwa wote tunaelimishana.
      Hapa unalewa kusema:
      Kan jag få ett glas vatten?

      Ukitaka kutumia lugha ya upole utasema:
      Skulle jag kunna få ett glas vatten?.
      Nipo likizoni Dar. Napatikana kwa namba 0716 333270


      Skulle jag kunna få = could I have/receive

      Delete
    2. Dada Yasinta samahani naomba nikukosoe kidogo kwa kuwa wote tunaelimishana.
      Hapa unalewa kusema:
      Kan jag få ett glas vatten?

      Ukitaka kutumia lugha ya upole utasema:
      Skulle jag kunna få ett glas vatten?.
      Nipo likizoni Dar. Napatikana kwa namba 0716 333270


      Skulle jag kunna få = could I have/receive

      Delete
  4. Kijita atasema mt simon....lol

    Kisimbiti: Ndasabha amanshe ghukunywa

    ReplyDelete
  5. Dada Yasinta, hicho Kiswidi, naomba utufundishe namna ya kutamka kwa kiswahili, maana mwenzako huku ulimi umeteguka

    ReplyDelete
  6. Koero, kwa jinsi ulovyo andika kijapani Watashi wa ina maana mimi
    omizu maji, kwa jinsi ulivyo andika ina maana MIMI MAJI

    ReplyDelete
  7. @ Mumyhery DUH!

    Yaani ndughu dhangu wapare wao hawajui kuomba ila kuthaidiwa thu!

    Love this post

    ReplyDelete
  8. NIGAILE MACHI YA KUNYUWA - naomba maji ya kunywa. Ifakara hiyo ila sijui ni kimbunga, kindamba au kipogoro na kwa kizulu NG'ICELA AMANZI - naomba maji

    ReplyDelete
  9. Kimatengo: "Naa masi ga kuunywa."

    ReplyDelete
  10. Kidachi, Ik wil water om te drinken, au Kan ik heb water te drinken.

    **'Wil' tamka vil, na 'Water' tamka 'Vata'

    ReplyDelete
  11. okey Koerounataka matamshi ya kiswid kwa kama kiswahili yaani kan jag be att får ett glas vatten utatamka hivi:- kani yogu be ati forr eti glasi vatteni.

    ReplyDelete
  12. Tang'a amanche gakunywa (kikurya)

    ReplyDelete

Andika maoni yako, Tujadili kwa kina