Thursday, November 25, 2010

MHESHIMIWA RAIS ALITUAHIDI HAYA, NI VYEMA KUWEKA KUMBUKUMBU

Ahadi za Muheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa mwaka 2010-2015:

1. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa.
2. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi
3. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi
4. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba
5. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma
6. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda
7. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa
8. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu
9. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino
10. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba
11. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
12. Serikali kulisaidia vyama vya ushirika
13. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa
kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu
14. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani
15. Kulinda muungano kwa nguvu zote
16. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa
17.Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa
18.Kujenga bandari Kasanga mkoani Rukwa
19.Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo
20.Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira
21.Kuzuia hatari za kisiwa cha Pangani kuzama
22.Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini


Chanzo Gazeti la Mwananchi

9 comments:

  1. Naaaaaamm!!!!!!!
    Hizi zoote zitatekelezwa ndani ya miaka mitano.

    Dada ulikuwa wapi? Dada umepotelea wapi? Dada mbona kimya???

    ReplyDelete
  2. hizi ahadi kwa mtizamo wangu hazitekelezeki!!

    ReplyDelete
  3. Kutoa ahadi si kazi kazi kuzitekeleza....Hatimaye umerudi Shukrani

    ReplyDelete
  4. Jamani nimerudi, lakini najaribu kutafakari upya, kwani nafikiria kubadili mwelekeo wangu wa kublog. najiuliza niandike habari za aina gani kwani habari za kisiasa zimenichosha na sasa nataka nijaribu kuandika habari zenye mwelekeo mwingine. lakini sijajua wasomaji wangu wangependa niandike juu ya nini. bado natafakari

    ReplyDelete
  5. Koero mie nashauri uandike habari za Bustani za maua na mapambo ya nyumba.......au?

    ReplyDelete
  6. naomba niseme kuwa 05 Disemba 2005 pale eneo fulani Morogoro vijijini mheshimiwa aliahidi kupeleka umeme....na mwaka huu katoa ahadi hiyo hiyo...
    uzuri wake leo sina mneno mengi...
    nilikumiss sana mchumba.....kuhusu mwelekeo wa kublog labda ushauri wa Ramson

    ReplyDelete
  7. Ahadi ya umeme kuwekwa unaweza ukawekwa, lakini mgawo ulivyo ni sawa na kutokuwepo kwa umeme, sisi siku hizi usikuu ni mwendo wa mshumaa...!
    KARIBU SANA MPENDWA, WE ANDIKA CHOCHOTE, SISI WAPENDWA WAKO TUNATAKA CHOCHOTE KUTOKA KWAKO, ILIMRADI TU USIADIMIKE!

    ReplyDelete
  8. ukijiingiza kwenye siasa zaidi utajikuta mjinga maana wanasi-hasa ni waongo na wanapumbaza

    usiwe na upande, kuwa general

    ReplyDelete

Andika maoni yako, Tujadili kwa kina