Tuesday, April 12, 2011

BODA BODA ILIPONITEGUA MGUU.

Juzi katika harakati zangu za kutafuta mikwanja, nikajikuta nikipigwa defrao na Bodaboda maeneo ya Msasani.

Niliwahishwa Hospitali na ikaonekana nimeteguka kifundo cha mguu wa kushoto. nimefungwa POP na sasa naendelea vyema.

9 comments:

  1. Ahsante kwa taarifa maana kweli ulipotea kweli. Na nakuombea upone kwa haraka. Duh hizi ajali hizi kaazi kwelikweli . Mungu awe nawe...Pamoja daima

    ReplyDelete
  2. Pole sana Msasani maeneo gani maana nami nabangaiza maeneo hayo nataka kuja kukuona, na kukujua hali

    ReplyDelete
  3. Ahsanteni ndugu zangu kwa kunipa pole, naendelea vizuri kwa kweli, na jambo la kufurahisha nimepata muda wa kuperuzi blog mbalimbali na pia kupata wasaa wa kuandika makala zangu. yaani nilikuwa sina muda, na sasa nataka niandike ujinga mwingi kisha niwarushie hapa kibarazani kwangu, kaeni mkao wa kusoma majungu...... LOL

    Kaka M-Three...nashukuru kwa kutaka kuja kuniona, ingawa ajali niliipata hapo Msasani, lakini kwa sasa niko Mbezi Beach kwa dada yangu nikijiuguza, niliondoka nyumbani Mikocheni tangu juzi na kuja huku Mbezi kwa dada yangu kudeka kidogo....LOL

    ReplyDelete
  4. Pole sana na tunashukuru kusikia unaendelea vyema!

    ReplyDelete

Andika maoni yako, Tujadili kwa kina