Wasomaji wapendwa wa blog hii isiyoisha vituko, Kwa sasa niko jijini Dar es salaam nimerejea kimya kimya na leo nilikuwa najaribu kufanya utafiti wa lugha za makabila yetu hapa nchini. Kwa mujibu wa tafiti inasemekana kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini.Niliamua kuangalia zaidi salaam, hususan za asubuhi, Kutokana na utafiti wangu nimepitia makabila kadhaa na kukutana na maneno yanayotumiaka katika salaam za asubuhi ambayo yanafanana kidogo, hebu tuone maneno hayo ni yapi:
KINGONI: Uyimwiki = Habari za asubuhi
KIZIGUA: Kugona vihi = Habari za asubuhi
KINYAKYUSA: Ughonile = Habari za asubuhi
KIYAO: kwimukaga = Habari za asubuhi
KIPARE: Murevuka = Habari za asubuhi
KIUNGUJA: wambaje = Habari za asubuhi
KISAMBAA: Onga makeo = Habari za asubuhi
KIANGAZA: Mwalamtse = Habari za asubuhi
KINYAMWEZI: Mwangaluka = Habari za asubuhi
KICHAGA: Shimbonyi = Habari za asubuhi
KIMERU: Konumbware = Habari za asubuhi
KIMASAI: Sopai = Habari za asubuhi
KISUKUMA: Mwadila = Habari za asubuhi
KIHEHE: Kamwene = Habari za asubuhi
KIBENA: Kamwene = Habari za asubuhi
KIKINGA: Ulamwihe = Habari za asubuhi
KINYIRAMBA: Ulalaliani = Habari za asubuhi
KIHAYA: Wabonaki = Habari za asubuhi
Kwa leo naishia hapa mwenye nyongeza anaweza kuongeza ili tujifunze pamoja.
Tukutane wakati ujao
23 comments:
Asante sana dada Koero kwa kutupa hizo,salam nyingine hata nilikuwa sizifahamu,mmmh ila hiyo ya kisukuma hebu fanya utafiti kidogo.
wewew kihaya umechamsha. Wabonaki sio za asubuhi bali ni mambo vp
Jamani kukosea ndio kujifunza.
kamala, mambo vipi, yawezekana ikawa ya asubuhi au ya jioni...au?
na dada Schola hilo la wasukuma niliambiwa tu si unajua kuuliza si ujinga...au nimedanganywa mwayego.....LOL
haya na wengine wekeni changamoto zenu humo.....
Koero nawe asante sana kwa salamu hizi. Hapo kwenye kingoni unaweza kusema UYIMWIKI kama ulivyosema au pia HABARI ZA LUKELA ni sawa tu. Nimefurahi kweli haya uyimwike. KIMATENGO: Kujumuka= Habari za asubuhi
Sasa mie napenda salamu hizi zikitafsiriwa moja kwa moja. Mfano WABONAKI itafsiriwe kama "umeona nini?"
Hahahahaaaaaaaaaaaaaa. Niliku-miss dadangu. Nasubiri "vijimambo" vya huko ulikopotelea.
Nakupa big up kwa kutuletea salamu kadha wa kadha.
Naomba kufanya marekebisho kidogo kwenye Kibena, nadhani na Kihehe yanaweza kuingiliana.
Katika Kibena, Kamwene ni salamu unapokutana na mtu kwa mara ya kwanza pasi kujali ni asubuhi, mchana ama jioni.
Salamu itumikayo kumaanisha 'habari ya asubuhi' husemwa 'ulamwihe' ama 'ulamwihe wuli' ambayo kwa tafsiri ya moja kwa moja ya kimsamiati ni kusema 'umeamkaje'
Sina hakika na Kihehe, sina ujuzi nacho. Lakini nina hakika na Kisangu cha huko Mbarali, Mbeya kwani kinaingiliana sana na Kibena.
Ahsante sana da Koero. Wikendi njema.
Hili ni somo la bure, siku nyingine utuwekee na jinsi ya kushukuru
koero
wabonaki ni kwa mkubwa kwenda kwa mdogo. vinginevyo inabidi ilembwe lembwe.
za asubui ni OloileOtai au plural Mulailemtai
waongelamo?-kijita. na pia Wachio nade?-kijaluo
Kinyaki pia hutumia 'ukwasilee' (akiwa mmoja) na 'mkwasilele' (wakiwa wengi), lakini mara moja moja sana.
Mzee wa changamoto: salamu nyingi za kibantu hazitafsiriki vema ikiwa unataka iwe hivyo. Pengine mwanzo ilikuwa hivyo lakini hali ya kutumika kama salamu inazififisha maana za kimaneno moja moja.
mfano 'shikamoo' na mdogo wake 'marahaba' tukizifuata maana zao tutakuwa hatusalimiani, uwongo?
salamu kama 'habari za asubuhi/mchana na kadhalika' huwa haina maana hasa kujua 'hali' husika. ndio maana majibu ya salamu hii asilmia kubwa (pengine 96+) ni 'nzuri'. maana ya salamu hizi ni kutambua na kutambulika katika jamii na uwapo wa wanajamii wenyewe. ingawaje hata hivyo maana za naneno yaliyomo katika salamu zetu hayafishwi katika matumizi yasiyo salamu.
Mwangaluka kisukuma za asubuhi. Mwadila ni jioni... tambua ya kuwa kinyamwezi na kisukuma salamu hazitofautiani
Kisukuma umechemka mzeiya, mwadela sio habari za asubuhi, mwadela ni habari za mchana/jioni/za kushinda
KUSUKUMA - Mwangaluka - habari za asubuhi.
Swadakta
Hapo kwenye kinyakyusa Habari ya asubuhi tunasema "otwa lobhonjo" au "mlembwike" au neno mghonile hutumika wakati wowote iwe asubh mchana au jioni japo hata mchana tunasema mwangele au otwo pamuse na usiku tunasema otwa pakeloo" ambapo huweza kujibizana "mghonile" "mghonile" "ndaga" "ndaga"
Na mie naomba nikurekebishe kwenye kibena, kamwene hutumika kwa watu wasioonana mda mrefu, kama mnaonana kila siku wanatumia "ulamwike" mkinga "ulamwihe" mpangwa "ulamwikhe" tofaut ya makabila haya matatu ni matamshi na rafudhi tu.
Wangaluka.. Walampola... Kinyamwezi..
Wasukuma tunasema mangaloke
Je habari za asubuhi tunasemaje kwa kwa lugha ya
kibondei?
Mtu akikwambia usindile unamjibu vp
Yes amekosea sio mwadila ni Mwangaluka ndo mana ya habari za asubuhi hiyo mwadila inatumika mchana na jioni mpka usiku
Wajibu namna hii mpola za kukaya. Au eit ale mpola du
Mbona sisi waha umetusahau?
Post a Comment