Friday, August 14, 2009

HUYU NDIYE YASINTA NGONYANI!!!

Yasinta Ngonyani, Picha kwa hisani ya Maisha Blog

Ni binti halisi wa kitanzania, ingawa anaishi ughaibuni lakini hujivunia asili yake na utaifa wake, ni binti pekee aliyejitolea muda wake kuwaelemisha watu wa rika zote bila kujali rangi, kabila, itikadi, taifa wala jinsia.

Binti huyu si mjivuni na hupenda kubadilishana mawazo na watu mbali mbali, na pia hupenda kufuatilia habari za nyumbani kwao alikotoka na haoni tahayari kuongea lugha ya kwao. Daima hujitambulisha kwa jina la asili ya kwao na huona fahari kutumia jina hilo.

Binti huyu hakuona ajizi kuwajuza wanae asili ya kwao japo wamezaliwa ughaibuni, amekuwa msitari wa mbele katika malezi ya wanae ili kuhakikisha wanae hao hawajitengi na asili ya aliotoka yeye.

Si mchoyo wa ushauri na kupitia makala zake aziwekazo kibarazani kwake amekuwa ni msaada kwa wengi, amekuwa mstari wa mbele katika kuilemisha jamii bila kujali rika. Amejitolea kufundisha kile akijuacho juu ya malezi na matatizo mbali mbali yanayowakabili wanandoa na malezi ya watoto.

Kibaraza chake kimekuwa ni kitovu chenye kukutanisha wadau mbali mbali wenye fikra pevu, na kuibua mijadala yenye kuelimisha, kufundisha, kuburudisha na kuhuzunisha pia.

Binafsi napenda kumuita dada na kwangu mimi ni zaidi ya dada, kwani amekuwa ni mwalimu mzuri kwangu nikijifunza mambo mengi kupitia kibaraza chake nimekuwa nikijifunza mengi, na sisiti kukiri kwamba chimbuko la kibaraza cha VUKANI ni kutokana na kile nilichojifuza kwake.

Ni mkweli na muwazi, na hasiti kusema wazi hisia zake, lakini huwa makini sana ili kuepuka kumuumiza mtu mwingine kihisia, na kama kwa kusema huko kutamkera mtu mwingine, ni mwepesi kuweka sawa maelezo yake ili kuondoa msigishano wa mawazo.

Nakumbuka wakati fulani nlipopata msongo wa mawazo kutokana na tofauti zangu na wazazi wangu, alikuwa ni mtu wa kwanza kunitumia email binafsi akijaribu kuniliwaza na kunitaka nisichukue hatua yoyote kujidhuru, naomba nikiri kwamba email ile ilinisaidia sana kurudi katika hali yangu ya kawaida na nilijisikia fahari kuona kwamba kuna mtu ananipenda na kunijali japo sijawahi kuonana naye uso kwa uso.

Huu kwangu ulikuwa kama muujiza, inakuwaje, mtu kusoma mawazo yangu kupitia blog tu halafu awe karibu nami kiasi hiki, ni kitu gani kimemvuta? Kusema kweli tangu siku hiyo niliamni kuwa maandishi yana nguvu sana na kupitia maandishi yawezekana mtu mwingine kukufahamu vizuri sana.

Nimekuwa karibu sana na binti huyu, na amekuwa ni mwema sana kwangu na mshauri wangu pia, na kupitia vibaraza vyetu, tumekuwa tukibadilishana mawazo na kupeana ushauri mbali mbali ili kuboresha ustawi wetu na wa familia zetu.

Huyu ndiye Yasinta Ngonyani, kwa kumsoma zaidi bofya hapa

13 comments:

Fadhy Mtanga said...

Mfano halisi wa kuigwa.

Unknown said...

She is also PRETTY!!!!.......LOL

Ramson said...

Imenichukua zaidi ya masaa mawili kusoma blog yake...ni kweli dada YASINTA unastahiili hizo sifa....
Koero ahsante kwa kulisema hili, wengi tulikuwa hatulioni..

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

siku nyingine utundike wasifu wa mzee wa Lundu nyasa, sio yasinta tu

Mzee wa Changamoto said...

Sasa ninajiuliza kama tutasahau kuwa Yasinta anayezungumzwa hapa ni MTU, tukaama kufanya kuwa ni "KIELELEZO CHA SIFA ZA UTU ANAZOSTAHILI KUWA NAZO KILA MTU" kisha tukajitahidi kuziiga si tutakuwa tunagusa maisha ya wengi? Na si kuyagusa tuu, bali kuyabadili na kuyaweka panapostahili na hayo ndiyo mafanikio. Nimesoma mahala ambapo mwenye kunukuliwa alisema "mafanikio si kupata utakacho, bali hujumuisha MAFUNZO ULIYOKUTANA NAYO UKIWA KATIKA HAAKATI ZA KUTAFUTA NA MAISHA ULIYOGUSA NA KUBADILI KATIKA HARAKATI ZAKO".
Pengine kwa kufanya afanyavyo Da Yasinta na kuongea yaliyo memma kwetu, TUTAFANIKIWA.
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Sijui nianzie wapi. Ok! Sitasema sana nachotaka kusema ni kwamba AHSANTE SANA MDOGO WANGU KOERO.

Unknown said...

Pia ni Kapulya Mdadisi......LOL

Ramson said...

Koero pia tunaomba wasifu wako...

Nicky Mwangoka said...

wasifu huu ni kweli, na nampa hongera da Yasinta

MARKUS MPANGALA said...

nimewasoma na kuwaelewa, nadhani kaka Ramson alitaka nitundike wasifu wa Koero.....

sijui itakuwaje manake haya mambo ni kama kuziba jua kwa bakuli.
halafu kaka Kamala L nimekuelewa sana tu lakini...... Lol hiyo kazi namwachia mwenye kibaraza chake atajua cha kufanya.... ha ha ha ha ha ipo kazi

Mwanasosholojia said...

Dada Yasinta atabaki juu siku zote!Hongera Koero kutabanaisha ukweli!

Unknown said...

Nami napenda kusema kuwa dada yetu Yasinta ni mfano bora kwa taifa letu.. Mimi ni msomaji mzuri wa kibaraza chake na kwakweli kipo juu..

Yasinta Ngonyani said...

AHSNTENI SANA WOTE KWA MAONI YENU MAZURI NIMEGUSHWA SANA. AHSANTENI SANA NA AAHSANTE KOERO KWA KUNIWEKA HAPA KIBARAZANI KWAKO.UBARIKIWE SANA.