Naomba muniwie radhi kwa kile nitakasimulia hapa leo, maana inawezekana nisiwafurahishe baadhi ya wasomaji wa blog hii au wanablog wenzangu. Ni jambo ambalo nililitafakari sana kabla hata sijaamua kuliweka humu nikaona ni bora niliweke ili niwashirikishe wadau wa blog hii.
Jana majira ya jioni nilitoka na shoga yangu kwende kupata mtori katika mgahawa ulioko jirani na nyumbani. Nakumbuka ilikuwa ni majira ya saa kumi mbili za jioni hivi. Wakati tunaendelea kula mtori wetu mara wakaja akina dada wawili ambapo walikaa katika meza iliyoko jirani na meza tuliyokaa.
Walikuwa wakicheka kwa furaha kuonesha kuwa ni marafiki ambao aidha walipoteana siku nyingi au walikuwa wanapeana habari kama ilivyo kawaida ya kina dada kila wakutanapo.
Hatukuwajali na tuliendelea na stori zetu, lakini nilijikuta nikivutiwa na mazungumzo yao. mmoja wa wale kina dada alikuwa akimasimulia mwenzake jambo fulani ambalo lilinivutia kulisikiliza. Hebu ngoja niwamegee kile nilichosikia kama kilivyo, sitapunguza wala kuongeza ili nisipunguze utamu maana kwangu mimi simulizi ile ilikuwa ngeni kwangu.
Yule dada alikuwa akimsimulia mwenzie juu mambo yaliyomkuta juma lililopita, na simulizi yake inaanza kama ifuatavyo:
Basi, mwenzangu huku kula kwangu vichwa, jana si yakanikuta ya kunikuta......
Hee! bibi wewe ni yapi hayo yaliyokukuta tena? Aliuliza mwenzake waliofuatana naye.
Yule dada akaendelea kusimulia mkasa wenyewe, Si unajua mishe mishe zangu za kutafuta mishiko {Nadhani Fedha} basi juzi mida ya usiku majira ya saa tatu nikazama zangu Club, na kwa kuwa nilipigika ile mbaya nilikuwa nimepania kuwa ni lazima nisitoke kapa, ile natia maguu tu maeneo ya viwanja mara ikasimama Toyota Hurrier moja nyeupe jirani na niliposimama kwenye kiosk kimoja ili kununua zana si uanjua huwezi kwenda vitani bila silaha...... mara kioo kikafunguliwa, na mzee mmoja hivi wa makamu ambaye ndiye aliyekuwa akiendesha lile gari aliniita, nilisita kidogo, unajua mie siwahusudu sana mablakii wa kibongo kwa kuwa hawakati mshiko wa maana, nilijivuta hadi pale aliposimama yule mzee, aliniomba nipande kwenye gari ili tuzungumze, nilimuuliza tunaenda wapi, aliniambia kuwa tunakwenda kupata chakula cha usiku mahali kama kampani tu. "Sikiliza mzee mie niko kazini kama ni biashara sema una kiasi gani, sio mambo ya misosi, kwani mie nilikwambia nina njaa?" nilimwambia kisha nikaanza kuondoka kwa madaha, akaniomba nirudi tumalizane, na niliporudi akaniuliza nitahitaji kiasi gani, nikamtajia kiasi kikubwa cha hela nikidhani atashindwa, akaniambia powa twen zetu......basi tukaondoka zetu
Yule mzee alinimbia kuwa anayo nyumba yake maeneo ya mbezi beach na ndipo tunapokwenda kupumzika, alionekana ni mtu wa heshima na aliyekuwa akiongea kwa upole, aliendesha kwa kasi na alikuwa haongei alikuwa amefungulia muziki wa kizungu wa taratibu kwa sauti ya juu kidogo. tulipofika alipiga honi geti likafunguliwa na mlinzi, tukaingia ndani na kupaki gari kisha tukashuka na kuingia ndani, lilikuwa ni jumba la kifahari hasa. Tulipoingia pale sebuleni nilikuta kuna sofa nzuri za maana na kulikuwa na Bar, yule mzee aliingia pale Bar na kuchukua whisky na barafu na kujimiminia kisha akanimiminia na mimi, nilikataa na kumwambia kuw napendelea Ram badala yake, aliingia kwenye ile Bar na kunichukulia Bacard na Coke na glass ya barafu na kuniletea.
Yule mzee alikuwa akiifakamia ile Whisky kwa kasi ya ajabu kama vile alikuwa akiwahi mahali, anishika mkono na kuniingiza chumbani kwake, nilimuuliza kuwa mkewe yuko wapi, aliniambia kuwa hainihusu na nisitake kujua juu ya mkewe, alikuwa akiongea kwa hasira kama vile tumegombana vile, alinitupa kitandani na alinivamia kama nyati aliyejeruhiwa pale kitandani,.....nilianza kuogopa, nikamuomba atulie nivue mwenyewe...Shoga yangu wee kwani alinisikia, nilibaki kimya kusubiri kitakachotokea, lakini nilishtuka nikamuuliza kama anazo Condom, maana sikuwahi kujinunulia pale kwenye kiosk, akaniambia kuwa hana Condom na hayuko tayari kuvaa condom kwa kuwa sio utamaduni wake,
"Hee mwenzangu ulikuwa hujui...Wazee huwa hawapendi kuvaa condom, kwani hata mie yaliwahi kunikuta pia, tena mara tatu,mie sivitaki kabisa vizee," alidakia mwenzie.
Basi mwenzangu niliogoppa ile mbaya,ikabidi nimuombe anipa pesa yangu kabisa tuliyopatana, yule mzee akanyanyuka na kwenda kabatini, nikajua amefuata pesa, mara akarudi akiwa na Bastola mkononi, niliogopa nusura nizimie, kisha akaniambia kwa ukali. "Sikia wewe malaya, ukileta ubishi nitakuua na hakuna atakayeuona mzoga wako, usiniletee masihara kabisa, unasikia?" aliongea kwa ukali na alionesha kabisa alidhamiria kunifanyia unyama, nilitulia kama maji mtungini, kwanza sikujua nipo wapi na hata sijui akinitoa hapo nje nitaelekea wapi. Alinifanyia alivyotaka tena pekupeku, nakwambia, dada hakunibakisha si mbele wala nyuma, nilikuwa namuomba mungu amalize hamu yake anirudishe aliponitoa.
Alimaliza nakuniruhusu nikaoge kisha anirudishe aliponitoa, niliingia bafuni na kuoga harakaharaka ili niwahi kuondoka maana niliogopa asije akanirudia tena. Basi shosti nilipomaliza nilivaa haraka haraka bila hata kujipodoa na nilipotoka pale sebuleni nilimkuta ametulia akiangalia TV huku akiendelea kunywa whisky yake taratibu.
Tuliondoka pale na kunirudisha pale kijiweni kwangu, ambapo pia alinipa mshiko wangu kama tulivyopatana, yaani nakwambia hata sikuona kama ile hela ina maana kwangu, nilijuta na kujiona kama mjinga kumkubalia yule mzee, kwani sina uhakika kama hajaniachia miwaya, maana alikuwa hana wasiwasi wakati anajua wazi juu ya shughuli yangu ya kujiuza.
"Shoga sasa si ukapime ujue afya yako?" Alishauri mwenzie...
" Nyoo akapime nani? Mie? Thubutuu, haki ya nani sithubutu! ya nini nipime nijiuwe bure kwa presha".
Waliendelea kusimuliana uchafu wao na sie tukaondoka mahali pale, lakini moyoni nilikuwa na maswali kadhaa niliyokuwa nikijiuliza, juu ya ile shughuli waliyokuwa wakiifanya wale mabinti ambao kwa mtazamo wangu wangeweza kujiajiri na kujipatia kipato cha kuwawezesha kujikimu. Kingine ni kile walichodai kuwa wazee hawapendagi kuvaa condom, swali la kujiuliza, hivi wake wa wazee wenye tabia hizi ziko salama kweli? Na je ni wazee au hata vijana wangapi wenye tabia hizi ambao wamepoteza maisha na kusababisha mayatima na wajane kuongezeka na kuwa mzigo kwa jamii na serikali?
Kusema kweli nilivutiwa sana na simulizi ile ambayo kiukweli ilikuwa hainihusu, ila kutokana na umbeya wangu nimeona niwamegee wanablog na wasomaji wenzangu ili tutafakari kwa pamoja.

8 comments:
Mmmhh!
Ngoja kwanza, tumbo linauma...............................................................................................................................
ok nimerudi....aise, hivi kwanini watu wanaogopa kupima UKIMWI? lakini vilevile nadhani kuna haja ya kuangalia haina hiyo ya "KULA VICHWA" maana unakula vichwa vingine ndiyo kama hivi vimedata kabisaaaa.
Wazee... ngoja .....................ebu sikiliza......kuna mtu anagonga mlango....................
ok nimerudi.... sina hisia au labda ni mashaka yangu au la...ila sijui maana wazee wetu wengi wanamkono wa SWETA kwahiyo sijui kama kuna uwezekano wa kutovaa kwasababu hiyo lakini ikiwa kweli kuna haja na imethibitishwa.... huenda ikawa huyo tu siyo woteeeee jamani ingawaje sijwaona.
Mmmmhh tumbo linauma......... ngoja nikanywe muarobaini.......nimeishiwa hoja.....hii mada ngumu
Huyu Mzee nadhani atakuwa ameathirika na anaonekana ana frustruation za kufiwa na mkewe ndio maana hataki hata kuulizwa habari zake
Mimi ni mwanasayansi. Tofauti yangu na wanasayansi wengine kama Isack newton, Eisenstein, Galileo na wengine wengi waliobadili hii dunia kwa vumbizi zao. Mimi ni mwanasayansi niliyefundishwa kukariri kazi za waliopita. Kwa kutumia hesabu(NI MOJA KATIKA MASOMO YA SAYANSI) ninaweza kukueleza kwanini wazee wengi hawatumii Kondom.
NINAANZA
1: Kwa Tanzania mzee ni mtu yeyote mwenye miaka 55 na kuendelea.
2: Kama una maisha ya kawaida unaweza kuishi miaka zaidi ya 20 toka upate HIV mpaka kuugua UKIMWI
3: Unaweza kuishi tena zaidi ya miaka 5 kama unaweza kutumia dawa ukishakuwa na ukimwi
4: Mimi ni mkristo. kutoka katika bibilia binadamu anatakiwa kuishi makumi mawili matatu na kumi moja moja( yaani miaka 70)
5: Na kwa wastani Tanzania Life expectancy ni miaka 51.9(52.6 kwa mwanamke na 50.4kwa mwanamume0
KWA KUTUMIA HIZO NADHARIA HAPO JUU UTAGUNDUA KWANINI MZEE HATUMII KONDOM
MOJA: Ki TZ tayari amevuka wastani wa Maisha ya watanzania wanayoishi
MBILI: hata kama akipata MIWAYA leo ana uhakika wa kuishi mpaka miaka 70 iliyopangwa na mungu.
TATU: hana tena vitegemezi watoto wote wanajitegemea. hata akifa aachi mzigo nyuma
NNE: Ameshakamilisha ndoto zake nyingi alizojiwekea duniani
TANO, SITA mpaka kumi nitaendelea kesho. NIPO KWENYE WIKI YA MITIHANI. NGOJA NIENDELEE KUKARIRI VITABU VYA WAZUNGU
'EMCHEKU' pekupeku inasemekana ni hatari. mungu atunusuru.
Quoting " Nyoo akapime nani? Mie? Thubutuu, haki ya nani sithubutu! ya nini nipime nijiuwe bure kwa presha".
She is in DENIAL!!!
Na dada andika kitabu cha hadithi, it will be perfect. You are an amazing writer...
Kabla sijakubaliana kitu na DADA "mfanywa" wacha niungane na waliotangulia. NADHARIA ya Kaka GODWIN ni ya kufikirisha saana na inaweza kuwa na ukweli mkubwa nyuma yake. Lakini pia Da Candy amesema nilichokuwa nasema over and over kuwa unastahili kuanza kuandika japo vi-"paukwa pakawa" kwani style yako ya uandishi ni swafi. Ila kama tulikushauri uandike gazetini ukasita na sasa utaanza, basi na hii utafanya tuuu.
OK!!!!!!
Nirejee kwa hao wadada. Kwanza nakubaliana na huyo mtendwa kuwa yawezekana ameambukizwa maradhi. Nisilokubaliana naye ni suala la kutotaka kupima ili kujipa presha kwani presha itakuja tuu. Labda asilojua ni FAIDA ya kujijua mapema.
Na mwisho nirejee kwenye MADA yenyewe. Kuwa ni kweli WAZEE HAWAPENDI KUVAA KONDOMU? Hapa suala li umri bali kinachoendelea. Huyu mzee anaweza kuwa mmkoja kati ya wale ninaowaona wako kwenye MISSION IN PROGRESS. Yaani ni OPRESHENI CHAKAZA KIZAZI ama waweza ita OPERESHENI SAMBAZA VIRUSI.
Na yeyote aliye katika hii operesheni hajali analala na nani kwani kwao hakuna ugonjwa m'baya kama waliona nao na kwa kuwa wanao, kila kitu ni nafuu kwao.
Kulikuwa na "mzee" mmoja ambaye alijigundua kuwa anao. Alichofanya kilitia kinyaa. Alirubuni kuanzia wake wa rafiki zake mpaka watoto wao kwa kuomba "mara moja" (akijua kuwa wahitaji mara moja tu kuambukizwa) na akachakaza kizazi vibaya mbaya. Na kwa kuwa alikuwa na pesa na hakuna aliyekuwa akijua hali yake, ilimchukua muda kuanza kudhoofika na hata alipodhoofika wakahusisha na "maradhi ya kitajiri" kama maini (eti sababu ya kunywa pombe kali) na mwisho wa siku walipogundua ni familia zipo kwenye "waiting list"
Hakutenda hayo sababu ya umri. Sababu alikuwa kwenye mission na sasa familia yake inaishi kwa wasiwasi wakidhani watu watawafanyia revenge.
Kwa hiyo siamini katika umri, bali katika "situation' na pia ule mtazamo wa "siondoki peke yangu" ndio sababu
Blessings Sis.
swali lampangala, ukipima unakuwa na wasi wasi kuliko ukiwa hujapima. hata kama huna hutoamini kutokuwa nao
Post a Comment