Monday, November 23, 2009

TUMEMUENZI VIPI HAYATI HUKWE NZAWOSE?

Hayati Hukwe Nzawose

Ahsante kaka Mubelwa kwa kunipa Link ambayo imeeleza kwa muhtasari maisha hadi kifo cha msanii huyu Hukwe Nzawose.

Kusema ukweli sikufahamun kama Hukwe Nzawose amekwisha fariki siku nyingi kiasi hicho, sijui ni kutofuatilia kwangu habari, au msiba wake haukupewa uzito unaostahili kwenye vyombo vyetu vya habari.

Lakini nina maswali kadhaa ambayo ningependa kupata majibu:

Je Serikali yetu iliwahi kumtunukia nishani yoyote ya heshima Dr. Hukwe Nzawose, kabla na baada ya kifo chake?

Je kazi zake zinatumika vipi katika kutangaza utamaduni wetu hapa nchini na hata nje ya nchi?

Je kuna mnara wowote wa kumbukumbu ambao umejengwa kule Bagamoyo kuonyesha kuthamini mchango wake pale chuo cha sanaa Bagamoyo?

Mwisho naomba nitoe changamoto kwa wasomi wetu, kwamba kuna haja ya wao kukaa chini na kuandika historia ya mtu huyu ili iwe ni kumbukumbu kwa vizazi vijavyo.

3 comments:

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kama kajengewa mnara wa kumbukumbu huyu nitashangaa - na ni lazima mnara huo utakuwa umejengwa na wadau binafsi. Alikuwa na marafiki wengi sana kule Sweden na Ujerumani na pengine hao watakuwa wamejitolea kumwekea kumbukumbu na kuhakikisha kuwa jina lake halisahauliki. Hatuna mwamko wa kuenzi utamaduni wetu na ndiyo maana tumezitelekeza hata lugha zetu. Sijui akina Mkwawa, Kinjeketile, Milambo na mashujaa wetu wengineo wanavyoenziwa leo hii.

Niliwahi pia kulalamika kuhusu kutelekezwa kwa kaburi la Shaaban Robert - wakati lile la William Shakespeare likifanyiwa matengenezo yanayogharimu dola 80,000! Soma hapa: http://matondo.blogspot.com/2009/09/kaburi-la-william-shakespeare.html

Ramson said...

Kaka Matondo, una haki ya kushangaa,
Kusema kweli sisi watanzania hatuna mwamko wa kuwaenzi wale wote waliojitolea kataka kuitangaza nchii hii kupitia nyanja tofauti tofauti...
Hata ukienda pale Wizara ya Elimu na uamaduni leo hii na kuuliza jina la Mzee Moris Nyunyusa unaweza kujikuta wakikushangaa.
Hivi leo hii ni nani anamjua Omari Naliene, Huyu alikuwa ni miongoni mwa Vijana waliounda kundi la tatu nane na kuutangaza utamaduni wentu nje, lakini tanngu afariki dunia,...amesahaulika kabisa.

Kuna haja ya kuanzishwa kwa tunzo za sanaa ili kuzienzi kazi za wasanii wetu ambao walitoa mchango wao au wanotoa mchango wao katika kuitangaza nchi yetu.

Nilishangaa sana huku ughaibuni kazzi za sanaa ya uchoraji za Tingatinga ni maarufu sana tofauti na huko nyumbani ambapo hata ukimuuliza mwanafunzi wa kidato cha sita kuwa tingatinga ni nani anaweza kukwambia kuwa ni lile katapila la kuchongea barabara.

Bado tunayo safari ndefu

Unknown said...

Duh!!!
Sina la kusema......