Ndugu wanablog wenzangu pamoja na wasomaji wa blog hii.
Msione kimya, bado natafakari, makala ya kuweka hapa, maana naogopa kuchafua hali ya hewa.
Mpaka sasa bado sijajua niandike kuhusu nini?
Naomba munipe muda, nikipata cha kuandika, nitarejea.
Friday, January 2, 2009
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Mhh dada yangu mbona vya kuandika vingi tu?Hakuna vituko vyovyote ulivyoviona mwaka mpya vinavyoweza kusaidia kutengeneza mada mwafaka?Kwa mfano,vipi kuhusu 2009 kwa wanafunzi wa vyuo mbalimbali...je "tiba" ya kufunga vyuo ndio "kinga" ya migomo kwa mwaka huu?Anyway,nadhani mada ziko nyingi...cha muhimu usihofie sana kuwaudhi/kuwakasirisha baadhi ya wasomaji wako.Pongezi au criticism ni dalili kwamba unachoandika kina uzito.
Ni hayo tu.
Hakikisha hofu ya kuwaudhi watu haikuzuii kuwa utakavyo. Pengine ni kiwango cha kuwa jinsi utakavyo kinachoweza kuathiriwa na maudhi ya watu, lakini kumbuka mchekeshaji na mwanaharakati maarufu hapa nchini aitwaye Bill Cosby aliwahi kusema "I don't know the key to success, but the key to failure is trying to please everybody".
Ninalomaanisha ni kuwa wahitaji kiasi katika kila utendalo. Usiwaudhi watu sana lakini pia usijipoteze mwenyewe katika kujitafuta. Kuwa wewe, na lazima utafika wakati ambao watu watalazimika kukukubali wewe kama wewe. Misimamo yako, aina yako ya maisha na kila utendacho kwa kuwa watatambua kuwa hawawezi kukubadili kwani uishivyo ndivyo utakavyo.
Usiwaudhi wazazi ila usijipoteze kwa kuogopa kumuudhi mtu.
Matatizo ama mambo ya kuandika ni mengi sana. Ni suala la "angle" ya mtazamo wa jambo lako. Na hata mjadala kulingana na mjada mwingine kama ule uliouanzisha baada ya kumsoma Bwaya na Kaluse.
Daima pamoja.
Blessings
Mwandishi mmoja (niulize jina lake baadaye)aliandika "the essential thing about writing is writing"
tafsiri yangu; "cha muhimu katika kuandika ni kuandika"
Hapo vipi?
hapo sawa mkuu, imetulia ni changamoto kwa dada Koero
JAMANI NIMERUDI.
WALA MSIHOFU.
Post a Comment