Saturday, March 3, 2012

SASA MIMI NI MKE WA MTU!




Asalaamu Aleikhum mabibi na mabwana – hii ni kwa ndugu zangu Waislamu

Shaloom – Hii ni kwa ndugu zangu Wakristo

Ni matumaini yangu nyote hamjambo na mnaendelea vyema na shughuli zenu za kila siku. Ni muda sasa sijaonekana humu Jamvini, na hiyo ilitokana na kutingwa na shughuli nyingi za kujiandaa na harusi yangu ambayo ilifanyika mwaka jana mwezi wa kumi.

Ni masikitiko yangu kwamba sikuweza kuwasiliana na wanablog wenzangu pamoja na wasomaji wa blog hii ya VUKANI, na hiyo ilitokana na kutingwa na mambo mengi yaliyojitokeza kwa kipindi hicho. Huyu mume wangu ni mtu anayependa usiri, hivyo hakutaka jambo hilo tulikuze saaana na kulifanya kwa mbwembwe. Tulifanya kasherehe kadogo sana ambako kaliwakutanisha ndugu wa pande mbili tu na baadhi ya marafiki wa karibu sana. Lakini pia ni vyema mkafahamu kwamba nimeolewa mkoani Kilimanjaro huko Marangu.

Baada ya harusi nilirejea kwenye pilika zangu za kusaka mkwanja, na kama mjuavyo kwamba biashara hapa nchini imebana sana, na watu wanakimbizana kutafuta masoko na hapo hapo tunapambana na TRA ilimradi shida mtindo mmoja.

Mume wangu alinishauri niache kublog, kitu ambacho sikuafiki, lakini baada ya kujadiliana kwa kina, tulikubaliana niendelee kublog, lakini nisimame kwa muda kwanza ili tuweze kusimama kibiashara na kuweka msingi wa maisha yetu kwani tulikuwa tunahitaji muda wa kuwa pamoja zaidi. Kwa sasa naitwa mama kijacho na niko mapumziko (Bed Rest) na ndio sababu nikapata muda wa kuandika na kuweka kitu hapa VUKANI.

Naomba mniwie radhi wote mliokwazika na kutowahabarisha juu ya harusi yangu, lakini nataka kuwahakikishia kwamba tupo pamoja.

16 comments:

Subi Nukta said...

Heko ya arusi na kila la heri katika maisha ya ndoa.

Koero Mkundi said...

Ahsante sana dada Subi.
Niliwa-miss sana, ni vile tu nilibanwa na majukumu. Nimeanza kuzoea maisha ya ndoa mwayego........LOL

Mija Shija Sayi said...

God bless you, nakutakia kila la heri katika maisha yako mapya mama kijacho.

Hongera sana.

Yasinta Ngonyani said...

Koero Mdogo wangu kwa mama mwingine! HONGERA SANA KWA MAISHA YA NDOA..NA PIA KUWA MAMA KIJACHO..

Anonymous said...

Da Mija na Da Yasinta nawashukuru sana kwa hongera zenu. tupo pamoja.

Mdogo wenu

Koero Mkundi

Rachel Siwa said...

Hongereni sana, Mungu awe nanyi daima!karibu sana kwenye maisha ya ndoa.

Fadhy Mtanga said...

Nami nikupe pongezi za dhati kwa hatua hiyo uliyoifikia. Kila la kheri katika maisha ya ndoa.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Hongera sana Dada Koero. Mungu na Akaibariki Ndoa Yenu kwa Kila hali. Amen !!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

Hongera sana mdada

Anonymous said...

hongera sana mdogo wetu Mungu akutangulie ktk maisha yako ya ndoa tulikumiss sana dear umefanya jambo la maana usijali kwa kutumiss bora uzima msalimie shemeji yetu God bless

Anonymous said...

bora umetujulisha nilikuwa najiuliza mbona kima lakini sipati jibu maana napenda sana kutembelea blog yako hongera mwaya kwakupata ndoa ni jambo la maana sana pole kwa yoote tutakuombea Mungu atakujalia kwa kijacho msalimie shemeji yetu

Simon Kitururu said...

Hongera sana!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

eeeeeeeeeewwwwwwwwwwwwwwuuuuu siamini mpakanione picha

Vimax Asli Canada said...

nice blog and article, thanks for sharing

jaya sehat said...

nice blog and article, thanks for sharing

poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605