Thursday, December 25, 2008

KUMBE BIBLIA ILIWAHI KUKOSEWA!!!!!!!

Mwaka 1631 toleo fulani la Biblia lilikosewa. Hili lilifahamika kama toleo la Mfalme James. Kwenye kitabu cha Kutoka 20, mstari wa 14 kulikuwa na neno lililoachwa wakati wa kuchapishwa.

Hii ni kwenye amri ya saba, ambapo iliandikwa, “In a thou shall commit adultery”, ikiwa na maana “Mzini”
Neno “not” liliachwa kwa bahati mbaya. Nakala za Biblia hiyo ziliitishwa na kuharibiwa kwa amri ay Mfalme Charles I.

Lakini hadi leo kuna nakala kama 11 ambazo kwa bahati mbaya hazikurudishwa kuharibiwa.
Hivyo ukikutana na moja ya nakala hizo, usije ukaiamini. Biblia hiyo ilijulikana kwa jina la Biblia iliyolaaniwa. Kwenye jengo la kumbukumbu ya Biblia la Branson, kuna nakala moja ya toleo hili.
Mchapishaji wa Biblia hiyo alitozwa faini ya sawa na shilingi 400,000 kwa kosa hilo.

Lakini tena mwaka 1653, neno lingine liliachwa kwenye sentensi katika kitabu cha Wakorintho 6, mstari wa 6 hadi 9. Kuna maneno “Know ye note that, the unrighteous shall inherit the Kingdom of God”. Badala ya “ Know ye note that the unrighteous shall not inherit the Kingdom of God” makosa hayo yalikuwa na maana kwamba waovu wenye dhambi ndio watakaouona ufalme wa mbinguni. Hii nayo ilikusanywa na kwenda kuharibiwa. Hii nayo iliitwa “ Biblia isiyonyoofu”

8 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Karibu saana Da Koero kwenye ulimwengu wa ku-blog. Nimefurahi pia kukaribishwa baada ya wewe kutembelea kijiwe changu. Kwa hakika nafurahia mijadala na naamini hapa patakuwa sehemu nyingine ya kuchanganua mambo jambo ambalo nalipenda saaana.
Lidumu jamvi la VUKANI

Yasinta Ngonyani said...

Koero asante sana kwa kuja kunitembelea na karibu sana kama alivyosema Mzee wa changamoto ulimwengu wa ku-blog.

Simon Kitururu said...

Biblia imewahi kukosewa na kama ni mfuatiliaji wa jinsi ilivyoandikwa unaweza kukwazika hata kabla ya kukosewa.

Asante kwa kunitembelea kijiweni kwangu na sito kosa kutembelea VUKANI.

Karibu sana katika kublogi Dada Koero

Koero Mkundi said...

Nawashukuru sana dada Yasinta, kaka Yangu Kitururu na kaka Mtwiba aka Mzee wa Changamoto kwa kunikaribisha katika ulimwengu huu wa Kublog.
Mimi si mtaalamu sana wa haya mambo kwa hiyo mkiona natoka nje ya mstari, mnielekeze.

Fadhy Mtanga said...

Dada Koero,
karibu sana tena sana,yaani sana mno.
Nakupöngeza kwa mambo mawili.
Moja, kwa kuamua kuutumia vema uhuru wa kusema kwa kutushirikisha fikra zako.
Pili, fikra zako zimesimama japo ni siku ya kwanza.
Nilisema mawili, naongeza la tatu, kwa kuthamini fikra za wengine.
Nne, jamani sina mipaka ya kuongea ati kwa sababu nilisema mbili ndo iwe mbili kweli! Nne, kwa kutukaribisha rasmi.
Tutapeana ushirikiano wa kutosha, maana hiyo ndo desturi yetu wanablog.
Karibu sana.

Christian Bwaya said...

Mambo mengi ya kiimani yanaonekana kuwa hayajadiliki. Wanapotokea watu wanaothubutu kuyajadili kwania ya kujifunza, hiyo ni ishara njema. Ujio wa blogu huu naamini ni changamoto mpya katika mijadala ya vile vinavyoitwa dogma.

Koero karibu mno.

MARKUS MPANGALA said...

Eeeeeee bwanaeeeeeee hayo mambo naogopa nikisema wanasema siamini kuhusu mungu! nikisema wanasema nakufuru mmm hasa dada Yasinta ananisema sana mmmmm. LAKINI si ndiyo ile biblia aliyochapisha JOHANESS GURTUNBERG enzi zile za GULDER 1000? au naongopa. swali kwanini injili ya 'bikira' maria iliachwa? kwanini walipiga kura ili ziingizwe katika utaratibu wa kuaminiwa? kwanini wasingeacha zote? lakini sizijui ati msije mkaniuliza hapa. dada KOERO upoooooooooo?????

Koero Mkundi said...

Jamani nipo sana tu na nitaendelea kuwepo.
lakini sikuwa na nia ya kuponda ukristo bali nilikuwa nashangaa tu.