Friday, October 30, 2009

HUU NDIO WEMA!

Jirani kala nini?Huu ndio wema! Unapotenda wema usitegemee fadhila. Unapokuwa na marafiki, ndugu, na jamaa wa karibu, watendee wema bila kudhamiria kupata fadhila kutoka kwao. Ninapoongelea wema na kutoa ninamkumbuka mama Theresa wa Calcutta ambaye kwa umri na maisha yake angelikuwa Bilionea lakini kwa kujitolea kwake alikufa masikini, lakini akiwa ni tajiri wa nafsi. Nina maana alikufa akiwa na ridhiko, kwani kazi aliyotaka kuifanya aliifanya tena kwa kufaulu. Je wewe hufurahii kuwa kama yeye?

Kumbuka amri kuu isemayo “mpende jirani yako kama unavyojipenda” Je unapokula na kusaza huwa unajiuliza kuwa jirani kala nini?

Tafakari………

6 comments:

Subi said...

hii picha, maisha ya Mama Theresa... basi, leo umeniacha na tafakari mengi sana.
Sote tunaishi katika kipande kimoja cha ardhi kweli! doh, namshangaa sana Mungu.

Ramson said...

Mmh!!! hata mie umenifikirisha kweli dada Koero

Yasinta Ngonyani said...

Koero hapa leo umenena na kweli inabidi tutafakari.

SIMON KITURURU said...

Nashangaa kwanini watu wengi hawadaki filosofi za Mother Teresa ambazo alikuwa anazikiri waziwazi kuwa umasikini ni kitu kilichokaribu na mbinguni na kuwa alikuwa hata siku moja haamini katika aidia za kuwatoa watu umasikini kwa kuwa aliamini hakuna kitu kiko karibu na utakatifu zaisi ya kuwa masikini.


Mtu mwingine naye shangaa kuwa anaonekana bomba la mtakatifu ni Mahatma Gadhi ambaye mpaka anakufa kinajulikana alikuwa analala na niece wake uchi kwa kitu kuwa anajipima kuwa midadi yake ya kufanya matusi ataidhibiti au la. Na kila akiamka asubuhi watu wanamshangilia kuwa ni bomba la mtakatifu. Na hapa wala sianzi kugusia jinsi mambo yake ya kibaguzi kisa Caste system au kwa kifupi alikuwa sio rafiki sana wa watu weusi kuanzia South Arika aliko luwa Mwanasheria na mpaka India ambako mpaka sasa hivi kama wewe ni mweusi sana wanajua tu wewe ni Untouchable katika Caste system.

Hivi inakuwaje haya mambo yote yanajulikana na bado Mother Theresa au hata Gadhi wanachekelewa na watu ambao wanaweza kufuatia mambo na kinamna hawafuatilii?


Ni mtazamo wangu tu kutokana na ufuatiliaji wangu tu wa mpaka akina Bikira Yesu.:-(

Mbarikiwe kwa jina la Mtakatifu asiye na dhambi Nyerere au Papa John Paul kwa kuwa mwenye dhambi ni Mtakatifu Idi Amini!.-(

Ila kabla hamja nitusi Watafitini muwanukuuo kitakatifu kidogo kabla hamja wageuza Mandela Mtakatifu kwa mtazamo wa wasio wake za Mandela aliowaacha wawili kwa kumpata mke wa Samora Masheli baada ya Samora Machel kuwa kafa baada ya yeye kutoka jela.

Mzee wa Changamoto said...

Labda siri iko kwenye ukweli unaofukuzwa ukitafutwa. Wengi wanadhani kuwa sisi ni "BINADAMU ZAIDI" tunaosaka uwepo wa Mungu na kusahau kuwa sisi tuna uUngu zaidi na twatakiwa kuishi kibinadamu.
Na ndio matokeo ya kusaka tusichokijua unaotufanya kuwa tusivyotakiwa kuwa.
Yaani inanibidi nirejee kile ambacho nimeshakisema saaana kuwa "tunajipoteza katika harakati za kijutafuta"
Wanaojijua wanaishi maisha mema na rahisi na kwa urahisi na wale wanaojikanganya kutafuta pa kwenda bila kujua kuwa wapo wanapotakiwa kuwepo, wanazidi kujipoteza.
Labda watu wanasaka UMASKINI WA NAFSI kuliko wa ROHO na ndio maana hata wakiwa na pesa zinazofikia kiasi cha kuhatarisha maisha yao wataendelea kuzisaka ili wawanyanyase wengine. Na wengine wanasaka pesa kwa masharti ya kuwafanya wawe na nyingi na wasizitumie.
Pengine la kujua ni kuwa UTAJIRI NI NINI NA WATUFAA VIPI.
Blessings
Baba Naniliuuuu

Markus Mpangala said...

sina zaidi kaka zangu