Ndugu wasomaji wa blog hii takatifu, leo nataka nijaribu bongo za watu kama zinafanya kazi sawa sawa maana week end hii nimekosa hata cha kuandika kutokana na kuzidiwa na majukumu ya kifamilia.
Nimetenga zawadi za kuwatumia washindi watakaoshinda katika kujibu mafumbo haya yote. Zawadi ya kwanza itakuwa ni Picha yangu kubwa ya ukutani kwa wale walioko ughaibuni au mikoani, au kupata chakula cha usiku mimi na mshindi wa kwanza katika Hoteli maarufu jijini Dar kwa wale walioko hapa Dar. Zawadi ya pili ni kutumiwa zawadi ya kitabu cha The Secret kilichoko online na zawadi ya tatu ni kutumiwa picha ya familia ya mzee mkundi.
Haya tuanze kufumbua mafumbo yafuatayo:
Fumbo la Kwanza:
Mama Yasinta ana watoto watano, wa kwanza anaitwa Nana, wa pili anaitwa Nene, wa tatu anaitwa Nini, wa nne anaitwa Nono, Je wa tano ataitwa nani?
Fumbo la Pili:
Kuna mtu mmoja bubu alikwenda kununua miwani dukani, alipofika alimuonesha muuzaji ishara kama vile anavaa miwani yule muuzaji akamuelewa na kumpatia miwani akaondoka zake, mara akaja kipofu, Je unadhani ataonesha ishara gani ili apatiwe miwani?
Fumbo la Tatu:
Ninazo namba kumi zifuatazo: 1,3,5,7,9,11,13,15,17.19
Kama ukizijumlisha zote yaani 1+3+5+7+9+11+13+15+17+19 unapata 100.
Unachotakiwa kufanya ni kutafuta namba 5 miongoni mwa namba hizo ulizopewa hapo juu na ukizijumlisha unapata 50 yaani nusu ya 100.
Masharti:
Haitakiwa kurudia namba, kwa kuijumlisha mara mbili au kujumlisha namba pungufu ya namba tano zinazotakiwa. kwa mfano: 13+17+15+5 unapata 50. Sio sahihi kwa kuwa idadi ya namba zilizojumlishwa hazifiki 5.
Haya nasubiri majibu yenu…….
IGP WAMBURA AFUMUA KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI
-
*Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Camillus M. Wambura amefanya mabadiliko
madogo kwa Wakuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani. Amemhamisha Naibu...
4 minutes ago
10 comments:
1,3,5,9,15,17
ukizijumlisha hizo hapo unapata 50.
nilikuwa sijasoma maswali ya mwanzo, teh teh, kama kawaida yangu huwa napenda kusoma hitimisho kabla ya dibaji na maelezo, eniwei, wacha nijibu.
Fumbo la kwanza jibu lake ni Yasinta
Fumbo la pili jibu lake ni Kipofu atasema nataka miwani na atapewa.
Fumbo la tatu nishajibu hapo juu.
la kwanza. YASINTA
la pili. KIPOFU ANAZUNGUMZA, HAINA HAJA YA KUTOA ISHARA.
la tatu. 1,3,5,9,15,17g
Fumbo la kwanza jibu lake ni Nina
Fumbo la pili ni kwamba kipfu atasema nataka miwani kwani anaweza kusema.
Fumbo la tatu jibu lake ni 1,3,5,9,15,na 19.
Nimerudi tena naona hilo fumbo la mwisho nimekusea kuandika namba ni 1,3,5,9,15 na 17
Fumbo la kwanza: huyo mtoto wa tano anaitwa Yasinta kwa vile mamake anaitwa mama Yasinta, na kwa mila za kwetu Afrika hasa Tanzania, mama hutambulika kwa majina ya wanae (Nimetumia anaitwa Yasinta kwa vile yupo keshazaliwa badala ya ataitwa nani ya kwenye swali, maana tukifuata swali ataitwa nani huo ni wakati ujao)
Fumbo la pili: Kipofu ana uwezo wa kusema, hivyo atasema anataka miwani na kuuziwa, hivyo haitaji kutoa ishara ili apatiwe huduma hiyo, labda kama muuzaji awe kiziwi.
Fumbo la tatu: Kwa kutumia namba tano kamili, hakuna muunganiko unaoweza kutoa jibu sahihi, yaani namba tano za kujumlisha na kupata 50, au utapata pungufu au utapata zaidi. Hilo jibu, hamsini linaweza kupatikana kwa kujumlisha namba sita kama walivyojibu waliotangulia, au kwa kutumuia namba hizi hapa 1, 3, 7, 9, 11, 19.
Mi naona nshakosa zawadi, maana walotangulia wote wamepatia!
Sasa nyie wengine si muwe mnasubiri na sie wenye akili za kutikisa (shake well before use) tufikirie?
Nshakosa zawadi mie maana waliotangulia washamaliza.
Siku nyingine Da K ukitaka kuweka swali la hivi uwe unatupa "heads-up" sie wenye akili za kushikiza.
Lol
Blessings
Naomba zawadi ya nne!:-(
mie nija jibu la swali la tau. nataka zawadi kwanza ndio niseme. ila nilishaingia mkenge swali la kwanza
Post a Comment