Wednesday, December 22, 2010

JINSI WATU WATOFAUTIANAVYO KATIKA KUSIKIA TUSI!

Katika kuelekea kuumaliza mwaka 2010, nimevutiwa na makala hii ya kaka Simon Mkodo Kitururu ambayo aliiweka pale kibarazani kwake mwanzoni mwa mwaka huu ilikuwa ni Januari 31, 2010.

Nimeona sio vibaya kujikumbusha jinsi watu watofautianavyo katika kusikia tusi..........!

Kunauwezekano kabisa UKIFIKIRIA,....

... utagundua UBUNIFU wa jinsi ya kustukia ni nini hasa ni TUSI haupo katika JAMII .:-(

Swali:

· Huwa unafikiria ni nini hasa siri ya misingi ya fikira zako za UTAMBUZI WAKO WA ni nini hasa ni TUSI?

· UKIFIKIRIA unafikiri binadamu wenye busara na akili UWAJUAO HUWA wanapatia tusi la kulikasirikia?

Kuna uwezekano kabisa UKIFIKIRIA,....

..... utagundua labda tafsiri ya tusi katika mawazo ya wengi ni potofu ndio maana hawastukii TUSI HASA ila wanasikia WALILOFUNZWA KUTAFSIRI TU kuwa ndio tusi katika jamii NA JAMII ,....


..... ambalo laweza kuwa kwa mfikiriaji wala SIO TUSI na ni jinsi tu ya lipakuliwavyo na kuwekwa mbele za mtu kumfanyako mtu kuacha kufikiria na kukasirika kisa kaambiwa ana meno kama uchi wa kuku na haki yanani kapandisha mori kuwa alicho ambiwa ni TUSI.

Swali:

· Ukifikiria kama BINADAMU AKIFIKIRIA unafikiri wengi wadhaniayo ni MATUSI yata faulu mtihani wa kuitwa ni MATUSI duniani ?

Na labda kimfano ,...

.. tusi la kweli ,....

.....KISIASA- ni lile la kubwa zima kufanywa mjinga kwa kuahidiwa AHADI ZA uongo na MWANASIASA KILA WAKATI WA UCHAGUZI MPYA ili umpigie kura KITU AMBACHO kirahisi kikiwekwa katika sentensi chaweza kuwa: ``Haya majinga kweli yani nikitunga TU stori kila wakati wa uchaguzi na kuahidi nisiyoweza hayaachi kunipigia KURA.Yaone vile kama vile haya stukii vile KUWA nalia ofisini na wala siwazi TATUZI la matatizo yao!´´

Na matusi KAMA hayo hutukanwa watu KIJAMII, KIDINI, KIUCHUMI au hata KIUTU tu WAO hata bila kustukiwa kwa kuwa kwa kiswahili watu wamefikia MPAKA kufikiria TUSI KUBWA ni mpaka tu jina la sehemu za siri za mtu.

Swali:

· Si ushastukia moja ya tusi maarufu kwa kiswahili ni kutajiwa JINA LA SEHEMU ZA SIRI ZAKO halafu mbele ya jina la NYETI ZAKO ikaongezewa neno ``YAKO´´?

· Hujastukia watu wengi hukasirishwa na wayatambuayo kama MATUSI ambayo hayana kabisa UBUNIFU?

· Unauhakika ulishawahi kutukanwa au ni tafsiri yako tu ndio itafsiriyo na kulijenga tusi?

· Unauhakika hatuhitaji kuwa na somo mashuleni ya jinsi ya kustukia tusi halisi ni nini ili tuache kukasirikia tafsiri za tusi ambazo zina fanya watu wakosee kustukia tusi halisi ni lipi?


Kwa bahati mbaya,...

... NA WASIWASI kuna uwezekano mkubwa,...

...wengi wadhaniao wamewahi KUTUKANWA na kufanikiwa kulikasirikia TUSI,...


...walichofanya ni kukasirikia TAFSIRI tu zao ZA KILE walichojifunza kukitambua kama TUSI,....

....na wote twajua tafsiri ni mwanaharamu ndio maana hata sentensi ``BAISKELI WEE!´´- ikilengwa kwa mtu mwenye udhaifu na baiskeli anaweza akakurukia kichwa, kabla ya kukukaba kabali halafu akakukata ngwala huku yuko bize akikukutajia jina la kikojoleo cha mwanamke halafu akaongezea neno ``WE´´mbele yake kwa kuwa anaamini kwa kufanya hivyo ana KUTUSI .:-(


Swali:

· Si unakumbuka kusikia au kutambua tusi ni kitendo cha kujifunza KUTAFSIRI TU ndio maana IRAKI kumrushia Rais George Bush KIATU ni tusi wakati kwa Mmarekani kumrushia mtu kiatu MAANA YAKE ni KUMRUSHIA MTU KIATU?

· Unauhakika jina la sehemu zako Nyeti chini kidogo ya kitovu ni MATUSI au ni kitendo tu cha kuzitumia hizo sehemu kabla ya kuhalalishiwa na Kanisa au Msikiti au VIBABU FULANI ndio matusi?



NI WAZO tu hili BINGWA na usikonde!:-(

8 comments:

Albert Kissima said...

Hahahahahahahahahahaha! Dah! Huyu dingi Mtakatifu anawaza jamani! Nalikubali saaaana wazo lake hili!

Ramson said...

Mie hii nimeipenda kwa kweli, ngoja ninukuu........

" tusi la kweli ,....
.....KISIASA- ni lile la kubwa zima kufanywa mjinga kwa kuahidiwa AHADI ZA uongo na MWANASIASA KILA WAKATI WA UCHAGUZI MPYA ili umpigie kura KITU AMBACHO kirahisi kikiwekwa katika sentensi chaweza kuwa: ``Haya majinga kweli yani nikitunga TU stori kila wakati wa uchaguzi na kuahidi nisiyoweza hayaachi kunipigia KURA.Yaone vile kama vile haya stukii vile KUWA nalia ofisini na wala siwazi TATUZI la matatizo yao!´´

Heshima kwako Mtakatifu.....

MARKUS MPANGALA said...

HILI WAZO HATA SITALIVALIA MIWANI, NI BONGE 'mmmmmmmmmmm".

hebu....

· Unauhakika jina la sehemu zako Nyeti chini kidogo ya kitovu ni MATUSI au ni kitendo tu cha kuzitumia hizo sehemu kabla ya kuhalalishiwa na Kanisa au Msikiti au VIBABU FULANI ndio matusi?

emu-three said...

Ni kweli neno tusi au maana ya tusi inategemeana na lugh ya mahala hapo na tamaduni zao, wengine kutamka neno fulani kwao ni kawaida tu kama Wamerekani, kuna neno wanpenda kulitamka mara kwa mara katika maongezi yao,(faki u) samhani nimeliandika kinamna hiyo ili lisichafue hali ya hewa. Hebu litafsiri kimaana yake, je unaweza kulitamka mbele ya watu hapa kwetu. KWAO ni lugha ya kawaida.
Nakumbuka wakati nasoma Umbwe sekondari, kuna mama mmoja alikuwa akiuuza ndizi za kuiva, neno alilolitamka kuwa ndio ndizi mimi nilishika mdomo, lakini ndio lugh yao. Kwahiyo tusi kineno linategemea na lugha, na tusi kitafsiri linategemea na tamaduni na mazingira ya hapo mahala.
Ni hayo tu wapendwa

Yasinta Ngonyani said...

TUSI!nilikuwa nawaza kwa sauti tu.... Darasa nzuri Koero Ahsante kwa kuiweka mada hii hapa kwani hakuna kitu kizuri kama kurudia kusoma kitu. Na Ahsante Mt. Simon kwa kuandika hili.

Mzee wa Changamoto said...

Lady Kitururu ama Kitururu Junior ama?
Nawaza tu na labda kama unadhani hili ni wazo ama tusi, utakuwa unaliangalia kwa namna uiangaliayo wewe ambayo "HAKI YA NANI" siyo niiwazayo mimi

Unknown said...

obat congek
obat darah beku
obat ambeien
obat sinusitis

Unknown said...


obat hematuria
obat asam urat
obat vitiligo
obat hidrokel anak bayi