Friday, December 24, 2010

MBOMBO JILIPO!

Mkurugenzi wa Takukuru Dr. Edward Hosea

Hili ni neno la Kinyakyusa, kabila ambalo linapatikana kule mkoani Mbeya, likiwa na maana ya ‘Kazi ipo’ ni neno ambalo nilijifunza kupitia kwa rafiki yangu ambaye tulikuwa tulisoma wote wakati fulani hapa jijini Dar.

Niliwahi kumuuliza maana ya neno hilo ambalo alikuwa akilipenda sana kulitamka hasa pale anaposhikwa na butwaa linapotokea jambo la kushangaza na ndipo aliponieleza maana ya neno hilo kuwa ni ‘Kazi ipo’

Nililipenda sana neno hili na nimekuwa nikilitumia sana pale ninaposhangazwa na kitu au jambo lolote. Wiki hii nimejikuta nikitamka neno hilo baada ya kusoma taarifa katika magazeti ya hapa nchini ambayo yalinukuu taarifa uiliyoandikwa katika gazeti la The Gardian la nchini Uingereza ambalo nalo lilinukuiu taarifa zilizovujishwa na tovuti ya Wikileaks.

Taarifa yenyewe ni ile ya mahojiano ya Mkuu wa TAKUKURU, Dr. Hosea, na Jasusi lililobobea la Kimarekani Bwana Purnell Delly ambayo yalifanyika jijini Dar es Salaam mnamo Julai 14 mwaka 2007.

Katika mahojiano hayo yaliyovujishwa na Wikileaks Dk. Hoseah alinukuliwa akidai kuwa Rais Jakaya Kikwete, ndiye chanzo cha baadhi ya vigogo waliotajwa kushindwa kuchukuliwa hatua katika sakata la rushwa.

Lakini katika hali ya taharuki Dr. Hosea akakurupuka na kukanusha kuwa amenukuliwa vibaya. Kitendo cha kukurupuka na kukanusha juu ya taarifa hiyo hakikumsaidia Dr. Hosea na badala yake kimezusha maswali mengine magumu zaidi.

Kunazuka maswali magumu zaidi kwa sababu kile kilichunukuliwa katika mahojiano hayo ya Dr. Hosea na Bwana Purnell, ndicho ambacho Watanzania wanachokiamini. Watanzania wanaamini kuwa kuna ajizi kubwa katika kuwashughulikia wahusika wa ufisadi. Na haiyumkini hilo ndilo lililopunguza idadi ya Kura za Uraisi kwa Muhueshimiwa.

Ama kweli mbombo Jilipo, maana kama taarifa hii ingevuja kabla ya uchaguzi mkuu, sijui matokeo yangekuwaje. Hata hivyo sitashangaa kama yatazuka mengine zaidi ya haya kwani kwa jinsi ninavyoona, nadhani bado kitambo kidogo kila kitu kitakuwa peupe...........

6 comments:

Mfalme Mrope said...

Ni sie watanzania? Hata kama habari hizi zingefuja kabla ya uchaguzi bado sisiemu ingeshinda tu! Je umeshahau kuwa mwendo wetu ni wa kanga za kijani na baiskeli kwa mjumbe wa nyumba kumi?

SIMON KITURURU said...

Mmmh!

kibunango said...

Nimependa jina la mada

Markus Mpangala said...

@Kibunango nakuunga mkono kwa hilo la mada hii. ni bomba sana.
>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>>
jamani markus wee unataka nini? au utakuwa kichaa? hujijui markus wewe? hujitambui au nini?
Lol... aise labda siku nikipata fursa ya kuzungumza na Julian Assange mwenyewe, ndipo nisadiki.

A.
aaaaaHH John Young alianzisha mtandao wa ww.wcryptone.com mnamo mwaka 1996. akiwa anatoboa kinachosemwa ati 'nyaraka za siri'. baadaye John Young akajiunga na mtandao wa WikiLeaks ulioanzishwa mwaka 2005. lakini baadaye John Young aliondoa akilalamika kuwa shughuli zilikuwa zikifanywa na maofisa usalama badala ya WikiLeaks wenyewe.
>>>>>>>>>>>>>>>>
B.
Mwendesha mashtaka Marianne Ny, wa pale Uswidi anasema wanawake wanaomtuhumu Julian Assange kubaka walikuwa maofisa wanaoshughulikia mtandao wa WikiLeaks kipindi cha nyuma. Mwanamke mmoja alidai walikuwa kikazi, lakini Julian Assange akaanzisha mahusiano ya kimapenzi, halafu siku ya tukio hadi kondomu ilipasuka(source; THE ARUSHA TIME, Desemba 11-17, 2010).

KWA UJINGA WANGU NA HITIMISHO LA MAWAZO MBILIKIMO.
Julian Assange bado hujanishawishi mtu wangu. Kwa taarifa nyingi zinazoripotiwa ati chanzo cha habari ni The Guardian la Uingereza, na waandishi wetu na wachambuzi huku bongo wanasea gazeti la The Guardian lina vyanzo vingi. halafu kuna mambo wanapambana ni siri. duh! wanisamehe siwezi kuvugwa akili kiasi hicho. na kweli wanavurugwa watu wepesi.
Julian Assange, anadaiwa kuvujishi siri. mimi najiuliza siri hizo ni zipi?

HAYA.
tunaambiwa jamaa wa takkuru sijui akamlima aya bosi wake ati hataki kuwakamata mafisadi papa.
jamani tayari Julian Assange anavishwa kanzu eti MKOMBOZI.

kwa akili zao kabisa watanzania wanakaa viambazani wakidai Julian Assange anavujisha siri za kibalozi baina ya marekani na nchi zingine. naomba mnisamehe siwezi kuingia katika hekalu hili.

kule afghanistan tunaambiwa mengiiiiii nacheka tu. kifupi siyo Julian Assange wala WikiLeaks hawawezi kuniteka, bado niko mkavu kabisa.

Nashukuru mama mchungaji umeanza kwa kusema KAZI IPO.
mimi nasema Divide and rule

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___