Saturday, May 7, 2011

JAMAA AKASAHAU KIFANYIO NDANI YA GARI!


Waliamua kumalizia hapa


Jana niliamua kutoka na kuwatembela rafiki zangu ambao nilipoteana nao kwa muda mrefu sasa. Ilikuwa ni furaha iliyoje kukutana na rafiki zangu hawa ambao baadhi nilisoma nao na wengine nilijuana nao kwenye mishe mishe za kutafuta Ngawira. Baada ya kupigiana simu na kutumiana ujumbe wa simu zetu za kiganjani, tukakubaliana tukutane kwenye mghahawa mmoja ulioko maeneo ya Masaki maarufu kwa kutengeneza Pastries unaojulikana kwa jina la Epidor.




Nilifika pale majira ya saa kumi za jioni na kuwakuta wenzangu wanne wameshafika, na walikuwa wakiendelea kupashana habari za hapa na pale. Nilijumuika nao, na tukaanza kukumbashana stori zetu za zamani hususana vituko tulivyokuwa tukifanya wakati tulipokuwa shule na vituko vya Waalimu wetu. Si mnajua wanafunzi wa zamani wanapokutana hukumbushana ujinga wao wa zamani?


Wakati tukiendelea na stori zetu akaja Shoga yangu Zulfa na kijana mmoja aliyemtambulisha kuwa ni Binamu yake anayejulikana kwa jina la Kishindo, Alikuwa ni kijana mtanashati lakini mwenye maneno mengi. Kwa muda mfupi alikuwa ameshachukua nafasi ya kuwa mzungumzaji mkuu akanifunika hata mie, ambaye najulikana kama kiranja wa kupiga soga. Alikuwa ni mtu wa masihara na mwepesi kudakia jambo na kuligeuza Comedy, naamini mnawajua watu wenye tabia za Comedy au Chale Chaplin ambao ukikaa nao ni lazima ucheke. Basi ngoja nifupishe maelezo, kwa kifupi ni kwamba wakati tunapiga tiralila zetu, akatupa stori mbili tatu hivi ambazo zilituvunja mbavu wote tuliokuwa pale, lakini kubwa zaidi zilituacha na maswali. Moja ya stori ambayo ningependa kuwashirikisha ni hii ya KIFANYIO. Tega sikio…………



Kuna jamaa mmoja alikuwa na rafiki yake anayeishi maeneo ya Ukonga naomba nimtambulishe kwa jina Ulimbo , sasa siku moja wakapanga na rafikiye anayeishi maeneo ya Tabata, (naomba huyu tumuite Kizito) wakutane kwenye Baa moja maneo ya Mwenge wajumuike pamoja na kupata moja moto moja baridi. Kizito alifika pale na usafiri wake na akamkuta Bwana Ulimbo ameshafika zamani . Wakati wanendelea kupata kilaji a.k.a ugimbi, Bwana Kizito akapata mgeni, hakuwa mwingine bali mfanyakazi mwenzie ambaye alifika mahali pale kama nasibu tu (Coincidence), Bwana Kizito akamtambulisha yule Binti kwa Bwana Ulimbo ambaye hakuwa ameoa, na kisha wakajumuika pamoja na kuendelea kupata vinywaji.



Muda wote wakati wanakunywa, Ulimbo alionekana kuvutiwa na yule Binti, hivyo muda wote alikuwa bize akimdadisi kutaka kumjua zaidi. Walizoeana ghafla na hatimaye walibadilishana namba za simu. Ilipofila usiku, yule Binti aliomba kuondoka, lakini Ulimbo akaomba kumsindikiza, walipofika nje ya Baa, yule Binti akamuaga Ulimbo kuwa anawahi kupanda Daladala kwani ilikuwa ni usiku majira ya saa nne hivi.


Ulimbo alimuuliza kama anaishi wapi, yule Binti alimjulisha kuwa anaishi Mwananyamala, Kizito alimuomba amsubiri pale nje, akamuage Bwana Kizito ili aje amsindikize. Ulimbo alikwenda kumuomba Kizito Gari lake kwa kuwa yeye hakuwa na usafiri ili amsindikize kimwana maeneo ya Mwananyala. Kizito alimpa gari lakinialimtahadharisha kuwa aendeshe kwa makini ili kuepuka ajali. Ulimbo alimhakikishia Kizito kuwa atarudi salama. Alichukua gari na kuondoka na yule binti kuelekea Mwananymala, walipofika njiani Ulimbo alisimamisha gari kwenye duka la dawa na kumuomba binti amsubiri ili akanunue dawa, kwani mdogo wake anasumbuliwa na Malaria na kuna dawa aliandikiwa angependa kumnunulia.



Baada ya muda alirejea ndani ya gari, na kuondoka, walipofika maeneo ya Mwananyamala, Ulimbo alisimamisha gari tena na kudai kuwa anajisikia kwenda haja ndogo, yule binti alimshauri waendelee na safari kwani nyumbani kwake anapoishi sio mbali hivyo wakifika atajisaidia hapo kwake kuliko kujisaidia njiani. Ulimbo alikaidi ushauri wa yule binti akidai kuwa amebanwa. Alishuka na kuzunguka nyuma ya gari aliporudi akazima gari na hadithi ikageuka, ilikuwa ni kama Swala ndani ya himaya ya Chui, Ulimbo hakukubali kumrejesha binti yule bila kumuonja, na kweli baada ya kutumia maneno matamu kama asali hatimaye binti akajikuta akikubali kumpa ulimbo utamu lakini kwa masharti ya kutumia Kifanyio a.k.a Condoms.



Kumbe Ulimbo aliposimama kwenye duka la Dawa hakuwa akitaka kununua dawa bali alitaka kununua Condoms kwa kuwa alishayapima maji na kuyaona kuwa hayakuwa na kina kirefu hivyo isingemuwia vigumu kuvuka hata bila mtumbwi (Yaani isingemgharimu kutafuta Guest House ya chapchap).


Sharti la kutumia Kifanyio lililotumiwa na Binti halikuwa kikwazo, Ulimbo alishakuwa nazo zamaani, (Wanaume waasherati huwa wana akili za ziada) Zoezi likafanyika mle mle ndani ya gari kisha akampeleka Binti nyumbani na kumshusha na kuagana kwa Mabusu kemkem. Alirudi pale Baa na kumkuta Kizito akiwa na ameungana na jamaa wengine wawili, hivyo wakaendelea kupata vinywaji hadi usiku wa saa sita hivi. Kwa kuwa Kizito ni mtu na familia yake akawaaga wenzie na kuondoka zake kurudi nyumbani.




Asubuhi mkewe Kizito alimuamsha mumewe na kumuomba funguo za gari ili waende Kanisani, kwani Kizito alidai kuchoka hivyo alimuomba mkewe aende na watoto, yeye wamwache apumzike.Mkewealipofika kwenye Gari aliamua kulifanyia usafi kwa kutoa Kapeti za gari na kuzikung’uta na kisha kuzirejesha ndani ya gari, alianza na kapeti za mbele na alipotoa kapeti za nyuma……….. Lahaullah……….. akakutana na Kifanyio kilichotumika kikiwa bado kina ubichi………….


Mwanamke yule alikurupuka na kwenda ndani kumuita Mumewe na kumtoa nje….walipofika kwenye Gari alifungua mlango wa gari wa nyuma na kumuonesha mumewe kile Kifanyio kilichotumika…… Mumewe alishikwa na Butwaa na kujikuta akitamka…………….. "Aaaaaaakh Ulimbo umeiponza masikini"…………… Msimuliaji hakufanya hitimisho, alituachia tafakuri kuwa, Je mume atawezaje kumuelewesha mkewe mpaka amuelewe?

5 comments:

Simon Kitururu said...

Je mume atawezaje kumuelewesha mkewe mpaka amuelewe?


-Inategemea na uhusiano wao MKE na MUME ukoje!

Kuna mambo mtu unajua tu haiwezekani kirahisi Kikwete ndio anafanya!

Kwa mfano mimi nikikosea kitu MAMA yangu hahitaji hata kuniuliza na anajua kuwa ni mie muhusika wa kuchemsha huko!

Ila kama tayari mahusiano yao yalikuwa ni ya mguu ndani mguu nje jamaa hata ajieleze vipi Mke atafikiri kifanyio na uji ulioko kwenye kifanyio ni wa mume wake na labda mpaka kuhisi nani muhusika kwa kubunia tu kutokana na ahisio Mumewe anawapenda!

Ni mtazamo wangu!

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana na kaka Simon inategemea uhusiana wa mke na mume ukoje. Kama mume alikuwa na tabia ya kutoka nje basi atapata shida lakini kama sio sidhani kama mke ana haja ya kuwa na wasiwasi. Ila inavyoonekana hana tabia hiyo kwani inaonyesha hana wasiwasi kabisa.... ila ni ngumu kwa mke kujua au kuamini...kaazi kwelikweli

Anonymous said...

Hapo Ulimbo kauziwa tu kesi, hiyo kazi kaifanya mwenyewe Kizito. wanaume ni mafundi wa kuteteana, hivyo hata Ulimbo akiulizwa ataikubali hiyo kesi kwa vile hajaoa!!

emu-three said...

Duuh, hii nikuwa sijainyaka...bab kubwa...

Vimax Asli said...

I like it this really good information.