Wednesday, May 4, 2011

JIONI HII PALE POSTA JIJINI DAR
Shiranga la foleni Jijini Dar linatisha, maana leo imenilazimu nijitulize ndani ya mjengo huo jirani na kupata kinywaji barrrrdi ili kuvuta muda foleni iishe, lakini hiyo bei ya vinywaji ni balaa tupu kwa siye tuliyozoea soda za mia tano, roho inauma kweli..............wanapaita Holiday Inn.


10 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaaazi kweli kweli hapo unaweza kuandika kitab u mpaska ukamaliza bila shida ila sasa nadhani shida itakuwa joto kama sikosei....

Goodman Manyanya Phiri said...

Mwaka-juzi (2009) lakini kulikuwepo picha fulani za utalii majengo ya juu juu ng'ambo na posta...namkumbuka chui! Ulijiburudhisha pia kwa hizo picha au la, kama bado zipo? Au uliandika kitabu cha Dada Yasinta?


Aisee! Leo ni siku yangu ya kuzaliwa; na nakuomba utembelee (nakujiunga pia na) blogu yangu mpya http://ninaewapenda.blogspot.com/


Humu najaribu kuelewesha watu ukaribu walugha zetu (Kiswahili na Siswati/Isizulu/Isixhosa).

Pia najaribu niwapate wanablogu wenzangu kama wewe hapo tuwape watoto washule mawaidha ya kufaulu shuleni... mtaalam hapa hamna... na kila mmoja wetu anatoa mawazo yake kusudi Afrika isonge mbele!

Nakushukuru!

SIMON KITURURU said...

Pole na Foleni Koero!

Turudi basi kwetu Upareni kule hakuna foleni halafu Kishumba , Kibulu na denge kwa wingi tu yani !

Nije kukuchukua turudi Upareni au upande wa Wachaga katika familia yako watachachamaa?:-)

Koero Mkundi said...

Kitururu, kwani hujui kama mie ni mchaga? upareni ni Ujombani tu

SIMON KITURURU said...

Kichaga wewe ni Mchaga! Kipare wewe ni Mpare!


Si wewe juzijuzi ulikuwa unatetea haki za wanawake na sasa hivi unajitambulisha kiume kwa kujitambua kama Mchaga kwa kuwa Baba Mchaga?

Angalau kwa WALUGURU kwetu MOROGORO mwamuzi ni MJOMBA na wala sio BABA!:-(

Koero Mkundi said...

Ok hii ni MADA nyingine: nilikuwa nabishana na jamaa mmoja kuhusiana na haya mambo unayotaka kuyaletea ubishi hapa, yeye ni Muislamu......
Akaniambia kama mtu muislamu akifa akizikwa wakati akisomewa dua ya Mazishi wenyewe wanaita TALAKINI kama sikosei, ubini wake hutajwa jina la mama yake..... kwa mfano mie Koero kama ningekuwa muislamu nikifa kwenye mazishi yangu msoma dua ataniita Koero Bin Namsifu na sio Mkundi...sijui umenielewa maana wewe Kitururu Una kichwa kigumu kuelewa……LOL

Niliuliza ni mantiki gani huwafanya wenzetu kutumia jina la mama? Yeye alijibu kuwa kwa kawaida baba halisi wa mtoto anayemjua ni mama, sasa ili kuepuka kutotambuliwa huko Akhera (sijui na nani?) hutumia jina la mama aliyemzaa.

TUKIO LA PILI:
Nikakutana na mama wa Kispanyola kutoka nchini Marekani (Mhispania), yeye akanambia kuwa kule Marekani wakati wa Sensa ya kuhesabu watu, mtoto hutambuliwa kwa utaifa wa Mama, (wenyewe huita Race kama sikosei), na swala hilo lilizua mjadala mkali miongoni mwa Wamarekani na sijui kama limeshapatiwa ufumbuzi au la.

Hivyo basi kwa huku kwetu mimi sioni tabu kujitambulisha kama Mchaga maana nimebeba tabia zote za Kichaga ukilinganisha na za Kipare………… Je nitajiitaje Mpare?

SIMON KITURURU said...

@Koero: mie sidanganyiki kirahisi:

Siamini kuna Muispanyola wala nini wa KIMAREKANI au KIespanya ,...


.. Muislamu akifa kwa kifafa au wakati anajamba:

Mchaga anafuata jina la BABAke kama BABA yake ni MCHAGA ,...

...na wewe ufanyalo ni kujitetea kuwa kwanini hujitambulishi kwa ubini wa MAMA yako ingawa wewe ni bomba la feministi udaio hata wanatitit kupiga magoti mbele yetu vidume ni NOMA wakati wa kutusalimia siye wanaume ambao inabidi wewe Kigoli utuinamie wakati unatusalimu SISI VIDUME kwa kuwa tuna mkuyati kama unatabia nzuri kwenye makabila kibao AFRIKA ....


Hebu jaribu tena Koero kujitetea kwanini wewe ni Koero Mkundi na sio Koero Msangi au ubini wowote wa upande wa Mama yako MPARE !:-)


Teh teh teh Nakuzidi pointi mpaka hapa Koero! Na najua una mashambulizi zaidi! lete mambo basi!

Au unataka nichokonoe mpaka haiwezekani uwe jeuri kihivyo hasa kama ni Msabato kwa kuwa huwezi kuwa huru kama ni Binti Msabato mwenye mawazo huru?


DUH! nchale wa kwanza huo na ngojea nikakimbilie ngao kabla ya mashambbulizi yako yajayo....

Na siunajua labda watoto wako hawata kuwa na ubini wako pia?DUH!

:-(

Uchokozi fulu betri imechaji !
lete vita nikishindwa nakimbia!

Koero Mkundi said...

Hizo sasa ni BANGI Kitururu....LOL

Ngoja nibane PUA.....

Eti..."Na wewe ufanyalo ni kujitetea kuwa kwanini hujitambulishi kwa ubini wa MAMA yako ingawa wewe ni bomba la feministi udaio hata wanatitit kupiga magoti mbele yetu vidume ni NOMA wakati wa kutusalimia siye wanaume ambao inabidi wewe Kigoli utuinamie wakati unatusalimu SISI VIDUME kwa kuwa tuna mkuyati kama unatabia nzuri kwenye makabila kibao AFRIKA ...."

Thubutuuuu.....NANI kasema mie mwana wa Mzee Mkundi nawanyenyekea Wanaume?
naona huna Hoja mpaka hapo maana unataka kuipindisha hii mada makusudi ili kunipima kama naweza kudhibiti mihemko yangu nikikwazwa......
Hunipati safari hii kaka.
Ngoja mie nilale maana usiku ni mwingi......

SIMON KITURURU said...

DUh Koero mpaka umebana pua!

DUh vita hii imenishinda !


Ngojea niendezangu baa unajua tena Sabato hii!:-(

Lala salama na nimatumaini yangu kuwa unajua ilikuwa ni uchokozi tu huu kukutongoza siwezi wala nini yani bali fulu kuhangaika nawe!

Si mpaka Mcharuko na Fadhy wakuache ndio zamu yangu?:-)

Goodman Manyanya Phiri said...

Mpaka mwishoni wa mjadala wa wawili nilikuwa nachekelea na kushangilia Koero wewe mshindi, lakini.......Sijawahi kumsikia Simon (kama madai yako Koero) yeye ni FEMINIST.


Pamoja na hayo, FEMINISM haitakiwi kamwe iongozwe na wanaume kama Simon; itakuwa dharau kwa wanawake. Sisi wanaume tunatakiwa tuunge mkono wale wanamama kama Koero, tusiwe wenyekiti kamwe!


Nguvu katika hoja ya Simon ipo bado pale pale ukizingatia kwamba ukoo wa mtoto kisayasni (MITOCHONDRIAL EVE) unafuatiliwa kwa upande wa mama tu, na siyo wa baba. Tazama tafadhali hapahttp://en.wikipedia.org/wiki/Mitochondrial_Eve


Kusema ukweli ulikuwa ni upuuzi au upumbavu mtupu tu tuitwe kwa ukoo wababa zetu; na kama wa Islamu wanaheshimu suala lake mama katika mazishi labda leo nimepata sababu nyongeza ya kuislimu na sitakuwa Phiri tena, bali Mavimbela!!!! (LOL!!!)


Nje ya vichekesho lakini, Koero: fikiri yai lako (ulikotokea, kwa jina la OVUM) lilianzia kwa bibi yako mzaa mama yako...ikiwa na maana mama yako alizaliwa nalo! Sasa itakuwaje mbegu (SPERM) changa kiasi labda cha mwezi mmoja kipewe jina juu ya mtu (OVUM) aliekuwa kwa mama yake kwa umri karibu wa mama yake?