Tuesday, April 19, 2011

BALAA GANI HILI!?

Msinielewe vibaya waungwana, hata mie nashangaa tu!!!!!!

22 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Duh! kaaaaaaaaaaaaazi kwelikweli katika dunia hii...mmhhh!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

unaifananisha na yanani??

Goodman Manyanya Phiri said...

Labda wananjaa. Nchi gani hiyo?

Anonymous said...

Kama wanajaa wapelekwe wabongo maana kwa ngono wameshinda, hao jamaa watazichoka za wabongo mpaka watakimbia wenyewe, dini zingine hovyoo.

Mcharia said...

DUH...!!!!

SIMON KITURURU said...

Ni moja ya kiungo Binadamu hujifanya wankionea aibu hadharani utafikiri sio kiungo tu cha mwili kama viungo vingine ambacho kama ni mwanaume sio siri hata uwe Papa John Paul watu hujua tu unacho!:-(

Nimewaza tu kwa sauti!:-(

emu-three said...

MKUU HATA KAMA NI KIUNGO, LAKINI KINA `USIRI', NDIO MAANA UMEVAA SURUWALI, INGAWAJE UKIWA NANIHII UNAICHOJOA...
Labda kuna ujumbe umefichika katika hayo maandamano, ...dada Vukani, tuweke wazi ilikuwa ni maandamano ya kudai kitu gani...vinginevyo...wanadhalilisha wanaume,AU?

Goodman Manyanya Phiri said...

@M3
@Anonymous
@Simon Kitururu

Tunatakiwa tusome zaidi katika NEUROSCIENCE (sayansi ya ubongo wa binadamu jinsi ulivyoumbwa vilevile jinsi unavyofanya kazi) ili tuelewe kwanini tunavaa nguo au kwanini ni mwiko kutembeza sehemu za siri hadharani kama picha yetu hiyo!


Kwa mfano, kama alivyogusia ANONYMOUS, watu wengi watashangaa kusoma kwamba katika NEUROSCIENCE uchamungu au dini yoyote ile ikiwa uIslamu au uKristo vyote (KATIKA UBONGO WETU SISI KAMA BINADAMU) vimekaa sehemu moja na jinsi vilivyopewa sehemu ya ubongo viungo vyetu vya siri kama hilohilo PENIS liliochorwa huko juu. Yaani, nisehemu moja kabisa kiasi kwamba unapokuwa msikitini Ijumaa au kanisani Jumapili na kumwomba Mungu wako UNAPATA KIASI FULANI CHA NY*G* bila kutahamaki!

Kwa namna ingine, kwa kitaaluma ya NEUROSCIENCE, ubongo wetu "unatuambia Mungu ni VAGINA au niPENIS na VAGINA ya mke wake Manyanya ndiyo Mungu wake”!

Sasa, Mkuu Simon, itakujaje "Mungu atembezwe barabarani akiwa uchi” kama tunaMpenda na kuMheshimu kwa ukweli?

Kama sijaeleweka bado, wacha niseme: kama watu wazima tunajuwa kabisa kwamba mara nyingi katika tendo la kufanya mapenzi moja wa wahusika bila kutahamaki hua kwa utamu wanaanza “ibada” pengine hata kutamka "Mungu wangu weee! OH MY GOD!" ikiwa huku wanafanya mapenzi! Yaani ni sawasawa wanaliita hilo PENIS au VAGINA "ndio mungu wao"! Sasa kama hiyo ni NEUROSCIENCE, na tunakubali Mungu yupo kwa kwenda misikitini na makinisani kila kukicha, itakuwaje mambo yanayohusiana na Mungu huyohuyo (yaani mambo yangono) yatembezwa mitaani yakiwa uchi kama hilo liPENIS katika picha ya mandhari hii?


Wacha ninukuu: [Hata Papa John Paul analo liPENIS].

Hata akiwa nalo, nani anataka kuona sura ya PENIS lake Papa John Paul?
Jamaani wote,

Daima, fikra na mawazo yetu vyote vinatokana na jinsi ubongo wetu ulivyoumbwa kama binadamu (HOMO SAPIENS).
Ubongo wetu sisi binadamu (HOMO SAPIENS) na sio ubongo wa NYANI au hata NGURUE: unahifadhi aibu, matumaini, uungwana, heshima ("RESPECT" &"HONOUR") na vitu vingine visivyopatikana katika ubongo wa viumbe wenzetu kama paka, panya, nzi na vingine! Ndio maana binadamu anaefanya vitu vya aibu anaweza kuitwa "ngurue", "mbwa" na kadhalika!

Kwendelea kidogo na muniwie radhi, nyani, kwa mfano, anatembea uchi kwasababu hana vitu kama aibu na ndio maana hata ukiwa na uwezo wakumfanya nyani awe daktari, kwamfano Daktari Nyani Wakike, wewe ukiwa Mkuu Simon ukimwendea Daktari Nyani Wakike kwa ugonjwa wako katika sehemu hiyo yasiri atakushangaza huyo nyani: baada ya kukuchunguza vidonda viko sehemu gani na kama havina hatari kwake, na baada ya kupata mniko wa hizo PHEROMONES zako ataanza kukupanda mulemule ndani ya chumba cha wagonjwa Hospitalini ya Muhimbili Dar es-Salaam na hatafukuzwa kazi kwani atajulikana kwa mkurugenzi wa hospitali hiyo kwamba "yeye Daktari Nyani Wakike ni nyani tu"!


Kifupi, hata ukiongeza kiasi gani cha hekima au ustadi katika kampyuta au hata katika ubongo wanyani ili waweze kufanya kazi kama binadamu, hawapati vitu kama ETHICS au heshima!

Kwa kumaliza, namshukuru sana “Anonymous” kwa kuelewa kwamba PENIS (Vilevile VAGINA) ni moja katika dini za watu kadhaa wa kadhaa. Wacha nimnukuu:

“Kama wananjaa wapelekwe wabongo...mpaka watakimbia wenyewe, DINI ZINGINE HOVYOO.”

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Kule Iceland kuna jumba la makumbusho spesheli kwa ajili ya dhakari za wanyama mbalimbali. Na hivi karibuni dhakari za binadamu zimeongezwa

http://news.yahoo.com/s/ap/20110412/ap_on_fe_st/eu_iceland_penis_museum

Sioni cha kushangaza hapa.

Mbele said...

Tukirudi katika imani za jadi, napenda kutaja kabila la Yoruba, kule Nigeria, ambao wanaamini miungu wengi, au miungu-mizimu. Mmoja wa hao miungu/mizimu ni Eshu ambaye ndiye mhusika wa hii ninihino iliyobebwa kwenye picha hiyo hapa juu. Eshu na ninihino hawatenganiki, na ni sehemu ya imani na ibada, hata kwenye michoro na sanamu Eshu aghalabu huonnyeshwa akiwa ninihino kubwa sana.

Yawezekana kabisa kuwa, kama ilivyo kwa wa-Yoruba, hii picha hapa juu inaonyesha shughuli maalum ya kiimani na kidini.

SIMON KITURURU said...

@Profesa Jay: SI labda kauli yako hapo juu labda ni MATUSI kwa kuwa hasa siku hizi hata utamaduni inabidi uvalishwe chupi ili kieleweke KIHESHIMA?

Ni kwa sauti tu nimewaza!!:-(

mumyhery said...

Jamani ni kitu cha kawaida inaitwa kanamara festival, mara ya kwanza nilishangaa, lakini hapo kuna mambo mengi yanayo fanywa hapo ikiwa ni pamoja na kuomba uzazi, kuomba Mungu awaepushe na maradhi yatokanayo na zinaa, pia huwa kuna kuchonga carrot daikon na mengineyo mengi, huwa inafahika kila mwaka kawasaki nafikiri niilisha towa mara moja kwenye blog yangu lakini sikuweka picha labda ukitaka kuangalia http://mumyhery-jp.blogspot.com/2010/04/unaijua-kanamara-festival-weye.html

mumyhery said...

Tena mgejeua kwamba inatembezwa mitaani juu kama mwenge tena sio moja ni kila team inakuwa na yao kwa hiyo inakuwa kama maandamano, hapo kuna pipi zinauzwa wanume wanakula pipi zenye sanamu ya kike na wanawake wanakula pipi zenye sanamu ya kiume kunakuwa na ibada pia, nilipoona watoto ndio wako wengi ikanibidi nizoee nione ni kitu cha kawaida lakini uki google kanamara festival au kanamara matsuri utaona mambo mengi zaidi!!!

Mzee wa Changamoto said...

Balaa? Kivipi?

Goodman Manyanya Phiri said...

Wanablogu wenzangu, Kipya Kinyemi Ingawa Kidonda, wahenga walitushauri zamani!

Sasa mimi napendekeza hapa Uswahilini (Afrika) tuanze basi kumla kila marehemu wetu kama dini mpya; labda serikali zetu Afrika zitaweza kuepukana na matatizo sugu ya kutafuta sehemu mpya kila wakati kwa ajili ya kujengea makaburi.


Kwa msiejuwa kwamba mtu analiwa kihalali duniani, tafuteni tu, kwani WEBSITE zipo nyingi sana kuthibitisha hilo.


Kwa mfano, vipo visiwa huko mashariki na dunia, badala ya "pipi za kike na za kiume" (kama picha yetu ya BALAA GANI) wao wanakula nyama ya mtu (CANNIBALISM) baada ya kutoa heshima/dini kwamarehemu mojawapo ikiwa kumpa marehemu jina lipya: "Ngurue Mrefu" (LONG PIG).


Siku hizi mtindo wakula nyama yabinadamu unasikika sana nchi nyingi duniani (hata Afrika Kusini) ingawa serikali karibu zote za piga marufuku...tena marufuku ya nini (Manyanya ninauliza sasa) wakati nyama ya binadamu ni sawa tu na nyama ya ngurue?


Mara ya mwisho kwangu kusoma, nchi ya Ujerumani ilikuwa ndio nchi pekee kutoona kosa la kisheria kwa mtu kupatikana na nyama ya binadamu mwenzake jikoni mwake tayari kupika nakula!

Hiyo ilikuwa baada ya msenge mmoja (Armin Meiwes) kulikata BALAA-GANI la msenge-mwenzake (Bernd Brandes) na kutengeneza mishikaki waliokula wote wawili kabla ya kummalizia mwenzie asubuhi yake kisha nakumla kidogo kidogo (kilo kwa siku) siku ishirini zaidi ili kuridhisha imani yake kuhusu undugu uliokamilika: 'ndugu yako kamili ni yule mtu uliemla ukiwa Ujerumani kwa kuimeza nyama yake kwa divai nyekundu kutoka Afrika Kusini' http://www.guardian.co.uk/world/2003/dec/04/germany.lukeharding

SIMON KITURURU said...

Koero chombezachombeza basi TOPIKI iendelee ili wataalamu washushe zaidi shule wengine tujifunze!

AU?

Adela Dally Kavishe said...

mmmmh kazi ipo

Koero Mkundi said...

Mengi yamesemwa na yataendelea kusemwa, lakini labda niseme tu kuwa kwangu mie ilibidi nijiulize tu kuwa ni balaa gani hili, Via vya uzazi vya mwanaume kufanywa tambiko...Mhhh!!
Niliwaza mengi lakini kubwa kabisa nilijenga shaka kuwa huu waweza kuwa ni muendelezo wa mfumo Dume.... tunarudi kule kuleeee.....

Ukisoma habari za mapenzi na mahusiano kati ya jinsia hizi mbili yaani ya kike na kiume kwa sie wanaadamu utakutana na simulizi nyingi za kushangaza kuanzia kimataifa, kijamii kimakabila na hata kiukoo...
niliwahi kusoma habari za Wajapani Kidogo.....

Mummyhery atanikosoa kwa hili..
Kiukweli kulingana na tafiti zao wenyewe Wajapan, walikiri kuwa nao mfumo dume haukuwaacha, umewatafuna na unaendelea kuwatafuta kwelikweli.....

mfano mmojawapo alioutoa mmoja wa watafiti hao ni kuhusiana na salaam.

Ilikuwa hivi: walikuwa kwenye kongamano huko katika nchi za ughaibuni, kongamano hili lilikutanisha wadau mbalimbali kutoka mataifa tofauti tofauti wakijadili masuala ya mazingira...
wakati wa Tea Break, mwanamume mmoja wa kijapan akawa anamsalimia mama mmoja wa kijapan pia kwa lugha ya kwao ya kijapan....(huyo mama alikuwa ni Profesa aliyesomea huko huko ughauibuni na kulowea huko) yule mama aliitikia salaam ile kwa kiingereza...

kazi ikabaki kwa mtafiti yule ya kutaka kudadisi na kudadavua ili kujua kisa cha mama yule kujibu salaam ya mwenzie kwa kiingereza ilhali kasabahiwa kwa Kijapan, je dharau kwa kuwa yeye ni msomi?

Unajua yule mama Msomi wa kijapan alijibu nini?

Alimwambia yule mtafiti, nitamnukuu hapa: "kama nikimjibu salamu yake kwa Kijapan, itanilazimu niinamishe kichwa chini kama Heshima kwake kitu ambacho nisingependa kukifanya"

mama amesoma na sasa mepambazukiwa kuwa halazimiki kuwanyenyekea wanaume eti kwa sababu tu mila zinasema hivyo.....

Si mnaona jinsi mila na tamaduni nyingi zinavyomdhalilisha mwanamke?

haya...... na hayo ya kubeba hilo jidude na kulisujudia si ni hayo hayo?

Nitarejea kwani ninayo mengi ya kuzungumza hapa....

mumyhery said...

Hii mila ya kuinamisha kichwa nia kawaida tu si kwa mwanamke au kwa manaume wote ni namna moja ukisalima inabidi unaimishe kichwa ukiwa mwaname au mwanaume lazima uinamishe kichwa, hata ukiwa unatoa shukrani inabidi uinamishe kichwa hata mkiwa mnaagana wote inabidi muinamishe kichwa, kuinamisha kichwa ni kitu cha kawaida kama kule kwetu kupiga magoti, na jinsi unavyo zidi kuinama inaonyesha jinsi gani unavyo heshimu

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

Koero Mkundi said...

Mummyhery wakati naendelea kuperuzi hili kabrasha ili nije na ushahidi mwingine, naomba nitofautiane na wewe kwa hili la kupiga magoti.

Ki ukweli swala la kupiga magoti nimelishuhudia kwa wenyeji wa kanda ya ziwa tu, kaka Matondo aka Profesa na Profesa Mbele watakuwa ni mashahidi wangu wazuri kwa hili.

huko nitokako mie, hatuha huo utaratibu kabisaaaa, kwa hiyo kujumuisha kuwa huku nyumbani tunapiga magoti si kweli....

Mila zinatofautiana dada... nipe muda bado naperuzi hili kabrasha linalozungumzia mambo ya Gender Equality ili nije na ushahidi mwingine.....nipe muda......

Yasinta Ngonyani said...

hapa kazi kwelikweli....Mie nataka kuungana na dada Mummyhery kuhusu kupiga magoti kwani hata nitokako mie kupiga magoti ni kawaida kabisa hakuna mtu anayeshangaa ni mila yetu. Unapiga magoti unapomsalimia mtu na unapiga magoti unapoaga....hapa kuna mengi ya kujifunza...