Wednesday, June 1, 2011

AKANIAMBIA NIKIZEEKA NA KUWA BIBI KIZEE NISIJE NIKAMUOMBA UGORO!

Ni jana majira ya jioni nikikatiza mitaa ya Msasani, nikakutana na mateja wako wachafu wamekaa kijiweni wakipiga soga. Mara akaijitokeza teja mmoja na kuanza kuniita kwa sauti ya mlegezo (sauti ya mlegezo ni voice tone inayotumiwa na mateja), “Oyaa sister eee..hebu nisubiri basi nikuulize” mie sikumjibu wala kugeuka, niliendelea kuchapa mwendo.Oyaa sister unajifanya uso wa mbuzi sio (hata sikumwelewa ana maana gani), niliendelea kuchapa mwendo bila kugeuka, na mapigo ya moyo yalianza kwenda mbio kwa woga maana niliona dhahiri anaweza kunikaba, kwani nilipita vichochoroni.


Baada ya kuona simjibu wala kugeuka, akaanza kumwaga maneno ya kifedhuli…….


Unajifanya mzuuuri kumbe huna lolote, uzuri wenyewe uko wapi? Sana sana unatumia mgorogo tu, we nini bwana ….. unadhani tuna shobokea mademu sisi,…… shika time yako, huna lolote mshamba tu wewe……


Tena sikiliza…. Ukizeeka na kuwa bibi kizee usije ukaniomba ugoro, maana hamkawii nyie, ukizeeka na kimkongojo chako……(akainama kuonesha mfano wa bibi kizee na mkongojo) lazima utakuja tu …. Kisha akaanza kuigiza sauti ya bibi kizee na kusema, “Mzee naomba kaugoro hapo nitulize kiu yangu”


Sitakupa ng’oooo…….. Ishia huko………


Mie na watu waliokuwa karibu tulivunjika mbavu kwa kicheko, maana ilikuwa kama mchezo wa kuigiza vile.
8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kwanza nilianza kusema na wewe Koero vichochoroni huko unatafuata nini?..baada ya juendelea kusoma nasoma huko nacheka na mpaka mchozi umenitoka...Ila umekatisha bwana...kaaazi kwelikweli

Goodman Manyanya Phiri said...

Wavulana wengine wanayo imani potofu kwamba mdada kutongozwa ni haki yake, hata akitongozwa kinamna gani ni sawa tu!

Mcharia said...

Sipati picha jinsi hata ulivyotaka kutimua mbio, laiti kama angeendelea kukufuata.

Pole kwa mapigo ya moyo kuanza kwenda kasi.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

Duh! siku nyingine ukitaka kupta vichochoroni unambie nikupe skoti bana teh teh teh teh!

Vimax Canada said...

I like it this really good information.

Vimax Asli Canada said...

I like it this blog information, thanks for sharing

Obat Kuat Asli said...

I like it this blog information, thanks for sharing

poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605