Wednesday, November 30, 2011

WANAPOJIREMBA KUPITA KIASI INA MAANA GANI
Siku hizi, kuna ugumu wakati mwingine, kujua kama mtu ni mwanamke au ni mwanaume. Vijana na hata watu wazima wengi wanaume hujipamba sana kwa kutumia vipodozi, ambavyo kwa kawaida, vimekuwa vikitumiwa na wanawake. Kuna wanaume wanaopaka nyuso zao dawa za kung’arisha na kupambana kabisa na ndevu.


Hawa ukiwatazama nyuso zao ni kama za wanawake, kwani mwanaume mwenye uso mororo sana huonekana kama mwanamke kwa kiasi cha kutosha. Kuna wanaume wanaovaa hereni, bila hata kujua wazivae kwa namna gani. Uvaaji wa hereni kwa wanaume, ambapo inasemekana ulianzia kule Marekani, ulikuwa ukifanywa kwa sababu maalum na kwa namna maalum.


Kwa mfano kuna waliokuwa, au wanaovaa ili kuonesha upendeleo wao kimapenzi (kwa mfano ushoga) na wengine kwa sababu mbalimbali.Kwa kawaida mwanaume anapotoga sikio moja tu, hasa la upande wa kulia na kulivisha hereni, inamaanisha kwamba, mwanaume huyo ni shoga! Kwabahati mbaya hapa kwetu kuna vijana ambao hutoga sikio moja la kulia na bado wanaamini kwamba, wako salama. Ukweli ni kwamba siku akikutana na raia wa Marekani wanaotafuta mashoga, hawatasita kumwita na kumtongoza.


Ndio maana yake, kwani nyie mlidhani vipi?Kwa kawaida wanaume wamekuwa wakikataa kuvaa mapambo na kujipodoa kama wanawake katika kuonesha kwamba, mwili wao hauhitaji vitu hivyo kwani ni mwili wa kazi hususan za nguvu na hivyo mapambo hayawezi kuwa na maana kwao. Ndio maana najiuliza kujipodoa na kujipamba huku kwa wanaume na kuvaa hereni na makorokoro mengine yanaashiria jambo gani?
9 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kusema kweli mimi siwaelewi kabisa maana nikiwa kama mwanamke tu huwa sijipambi hivyo sasa wao je wanataka kusema Mungu alikosea kuwaumba wawe wanaume? Lakini hata wajitahidi vipi mbona wanaonekana ni wanaume angalia walivyokomaa...Jamani Mungu hana makosa tujikubali kama tulivyo...Oh na Koero karibu tena nilikumiss mdogo wangu...

Goodman Manyanya Phiri said...

Waambie Dada Koero kwani wengine wanaiga tu vya Wazungu bila kuelewa undani wake!

Albert Kissima said...

Makorokoro mengine ndio kama hivyo pichani, wanaume hao wamevaa nguo za kike. Wanaume hawa ni dhahiri kuwa ni mashoga!

Sura ya mwanaume kuwa nyororo hainishawishi kusema kuwa mwanaume fulani anatamani kuwa mwanamke maana hata lishe bora tu hufanya ngozi ikawa na afya na ikawa nyororo. Lakini inapofikia mahali mwanaume (mbali na kuvaa vitu kama hereni, bangili za wanawake n.k) akaanza kuvaa nguo za wanawake na kuongea sauti za kike, kupaka wanja na mambo kama hayo, basi ni wazi kuwa mwanaume huyu anaukana uanaume wake. Hapa, mwanaume wa aina hii ana kila sababu ya kuitwa shoga.
Wapo wanaume ambao kwa bahati mbaya, wamezaliwa wakiwa na upungufu wa homoni za kiume na hivyo kukosa "male Secondary sexual characteristics". Watu wa aina hii kama hawatakuwa ktk uangalizi mzuri basi wanaweza kujipodoa barabara na kujisiriba na makorokoro mengine mengine mengi na kuangukia kwenye ushoga. Lakini wapo wanaume wanaojiingiza ktk ushoga kwa kupenda, kupitia msongo rika, tangazo linakuambia ufanye jambo fulani katika mazingira haya, mtu anajiuliza kwani nikifanya nini kitatokea, mwisho wa siku anajenga tabia na inakuwa mazoea.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mimi huwa sina shida ya kuwatambua hata wakijiremba na kujipamba namna gani? Hata wafanye operesheni za kubadili jinsia...wanajulikana tu!

Kwema da Koero? Za miaka?
===================>

Nilikuwa napita hapa kusema kwamba sasa nimerudi tena rasmi. Tupo pamoja !!!

http://matondo.blogspot.com/2011/12/wanablogu-wenzangu-na-wapenzi-wote-wa.html

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

Obat Vimax said...

I like it this really good information.
I visited several web pages however the audio quality
for audio songs existing at this website is truly fabulous.

Vimax Asli Canada said...

nice blog and article, thanks for sharing

jaya sehat said...

nice blog and article, thanks for sharing

poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605