Inaelezwa kwamba Maziko Wamakonde huwa na maombi tofauti na yale yanayofuatwa na madhehebu
mengine. Badala ya Sheikh au Kasisi kusoma dua, Wamakonde wana desturi ya
kuieleza maiti maombi na maonyo ili marehemu huyo asije patwa na madhara wala
asiandamwe na mikasa katika safari yake huko aendako, na pia ndugu wanaobaki
nyuma wasikabiliwe na mabalaa na mikosi ya aina yoyote. Wenyewe wanaamini
kwamba mabalaa huongozana, yaani likitokea moja hufuata la pili, la tatu na
kadhalika. Kwa mujibu wa simulizi zao, kuna madai kwamba pale mambo hayo ya
mila yanapopuuzwa vifo mfululizo hutokea katika familia husika.
Mkuu
wa mazishi Huieleza maiti wakati wa maziko:
“Ndugu umeacha jembe, mshale, shoka, nyumba
na kazi kwa hiyari yako mwenyewe, hakuna aliyekulazimisha kufunga safari hii,
ile wewe mwenyewe umeazimia. Umetuacha sisi huku nyuma kwa hiyari yako
mwenyewe, Hivi, ufikapo kwenye ukomo wa safari yako, ukaeleze yanayokuhusu wewe
binafsi. Wakikuuliza ‘Wako wanadamu wengine waliobaki?’
ukawajibu, ‘hapana.’ Ujitahidi
kuwathibitishia kwamba ni wewe tu peke yako, hakuna mtu mwingine aliyebaki.”
Kwa
maneno hayo, inadhihirisha wazi kabisa kwamba waliobai nyuma wanaogopa kufa.
Ingawa wanajua kuwa kufa kupo, ila kama kunaweza kukwepeka basi ombi lao
lisikilizwe!
Hata
hivyo inadaiwa kwamba mila hii bado inafuatwa na Wamakonde wa Msumbiji, tofauti
na Wamakonde wa Tanzania ambao mila kwa kiasi kikubwa zimeathiriwa muingiliano wa makabila na dini hizi za
mapokeo