Thursday, April 11, 2013

HILI NENO, "MWANAUME NI KICHWA CHA NYUMBA," HUWAPA KIBRI SANA HAWA VIUMBE




Kuna jambo moja ambalo hufundishwa na viongozi wa dini mbalimbali, ambalo pia waumini hulihubiri vizuri kila mahali wapatapo nafasi ya kufanya hivyo. Nalo si jingine ni lile la ‘mwanaume ni kichwa cha nyumba,’ ikiwa na maana kuwa mwanaume ndiye mkuu wa nyumba au familia. Suala hili linazungumzwa kama kwamba, mwanaume kuwa mkuu wa familia ni jambo la kimaumbile, lakini pia huzungumzwa kama vile, ukuu huo ni tiketi ya mwanaume kuikandamiza familia au mke. 

Nijuavyo mimi, wanaume wengi kuwa wakuu wa nyumba au familia ni suala la mazoea zaidi kuliko maumbile. Kwa miaka milioni kadhaa, mwanaume amejikuta akiwa ndiye mkuu wa familia. Kutokana na mazoea haya, jambo hili limekuwa kama vile ni la kimaumbile, yaani haliwezi kubadilika au kubadilishwa.

Lakini mbona kuna wanawake ambao ndiyo wakuu wa familia na familia hizo zinakwenda vizuri tu. Lakini vilevile kuna wanawake ambao hawana waume na wanaongoza vyema familia zao. Kwa bahati mbaya kwenye jambo hili, ni kwamba, kumekuwa na msisitizo kuwataka wanawake wawaheshimu waume na siyo wanandoa kuheshimiana. ‘mwanaume ni kichwa cha nyumba, ndiye msemaji wa mwisho. Inabidi aheshimiwe.’ Kuna watu ambao bila aibu huzungumza lugha hii.

Ni kweli wanaume wanahitaji au wanapaswa kuheshimiwa. Lakini siyo wanaume peke yao, bali binadamu wote wanapaswa kuheshimiwa bila kujali wanafanya nini au wakoje. Kwa hiyo siyo kwa sababu ni wasemaji wa mwisho, basi wao ndiyo wanaopaswa kuheshimiwa. Kwa kuamini hivyo wanaume wengi wamekuwa wakitumia nafasi hiyo kuwakandamiza wake zao na hata watoto. ‘Mimi ndiyo msemaji humu ndani, nimesema sitaki, basi.’ Mara nyingi matumizi ya mabavu kwa namna hiyo hutumika.

Kuna haja kwa wanaume kujua kwamba, kuwa kwao viongozi wa familia hakuwapi ubora wa ziada. Wanawake nao wanapaswa kujua kwamba, kutokuwa kwao wasemaji wa mwisho wa familia, hakupunguzi hata chembe ya thamani ya ubinadamu wao, kwani binadamu na wanandoa wanapaswa kuheshimiana. 

9 comments:

Mzee wa Changamoto said...

"...Pamoja na yote naamini pia italeta changamoto na migongano ya mawazo, ndio maana nikasema VUKANI."

VUKANIkeni jamani

Yasinta Ngonyani said...

Kwanza napenda kusema ni furaha ilioje kupna haya maabdishi. Maaba hii ni dalili ya kwamba umerudi na utakuwa nasi. Koero siku nyingine uage. Nimekumiss mno mdogo wangu.
Kuhusu wanaume kuwa wakuu wa nyumba hii ni jinsi tu ya malezi yetu na hasa tamaduni zetu. Ila mimi ningependa kusema si kweli kabisa ni maelewano tu katika kila ndoa......nimejawa na furaha mno kwa Ujio wako mpaka nashindwa Kuwazana

Koero Mkundi said...

Kaka Mzee wa Changamoto na Dada Yasinta ahsanteni sana kwa kupitia kibaraza hiki.

Kwa kweli sasa nina furaha sana kurejea kibarazani kwangu baada ya kuadimika sana.

naomba sasa mkae mkao wa kula maana Koero nimerudi

Mija Shija Sayi said...

Da'Mija huwa napotea lakini Da'Koero ulitia fora...yaani zaidi ya mwaka!!!

Karibu sana mdogo wetu, vipi duniani kunasemaje?

Asante kwa mada hii, cha msingi we need self awareness, tukilipata hili kisawasawa hakutakuwa na matatizo kwenye familia zetu.

Rachel Siwa said...

Kwanza tunashukuru kwa kuwa nasi tena..pia umerudi kwa kasi nzuri..hii kitu mada..imenikuna vilivyo!!!

da'Mija........

sam mbogo said...

Hakika nikweli wasemavyo,mzee wa changamoto,da Yasinta,da mija,pamoja na bisikuti yangu(Rachel).karibu sana bi koero. mimi na unga mkono hoja ya kuwa mwanaume nikichwa cha familia/kiongozi wa familia.kaka s

Vimax Pills said...

I like it this really good information.

Vimax Asli Canada said...

I like it this really good information

jaya sehat said...

I visited several web pages however the audio quality
for audio songs existing at this website is truly fabulous