Wakati mwingine ukikuta kuna makosa ya herufi kwenye Blog hii, naomba uyavumilie, kwani hilo ni kosa la kiuchapaji tu. (Typing error)
Kama hutaki kukubali kama
Mwaka 1985 ,
Hebu niambie, noti ina maandishi gani mengi hadi ikosewe tarehe? Lakini hebu niambie inabidi watu wangapi waipitie noti hiyo kabla haijaidhinishwa kuchapwa?
Naamini ni watu wengi tu waliipitia lakini bado ilikosewa!
Naomba mnivumilie kwa mcharazo….
4 comments:
Duh!! Ni kweli twahitaji kuvumiliana. Lakini sasa mtu akigundua akwambie ama kukuvumilia kunamaanisha "kumezea?"
Usijali, charaza tu mama
Kaka Mubelwa, kukosolewa ni muhimu, bali nimeomba kuvumiliwa tu,
Nikikosolea naamini ndio njia sahihi ya kujifunza zaidi na zaidi na hivyo kuwa bora katika eneo hili la kublog. Au sikueleweka?
Kukosea ni moja ya maisha, usipokosea basi huwezi kujifunza kitu!
tusipokosea maanayake hatutendi lolote i.e wasiokosea ni wale wasio tenda tu!
lakini kuna makosa mengine duu
kuna bintimmoja maarufu kama Irene malonga, alisoma taarifa ya habari pale itv, badala kusema watu kumi, pale kwenye herufi 'i' ya kumi akaweka herufu 'a' na hivyo kusomeka ile kitu nisiyoweza kutaja ili nisilazimike kuomba radhi. basi taarifa ya habari ilikaa kimya dakika kadhaa na hadi sasa sikuwahi kumuona tena eti kisa? katamka a' badala ya i'
tamu hiyo
Post a Comment