Thursday, April 23, 2009

SHAMBA LA BIBI KOERO


Hili ni shamba la Bibi Koero. Picha hii niliipiga mwaka jana mwanzoni kabla sijaanza kublog, nilipoenda kumtembelea bibi yangu Koero huko Upareni. Nakumbuka nilipofika bibi yangu alifurahi sana, kwani nilikuwa sijaenda kumtembelea kwa takribani miaka mitatu hivi. Kutokana na furaha aliyokuwa nayo, alinichinjia Jogoo mkubwa nikamfaidi peke yangu.
Nimemkumbuka sana bibi yangu, laiti ningekuwa na mabawa ningeruka kama ndege na kwenda kumtembelea bibi yangu Koero.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hongera kwa kuwa na bibi mwema hivyo anayekuchinjia na jogoo mkubwa. Na pia hongera jwa kuwa kurithi jina lake(wajina) Halafu hilo shamba ni nzuri sana maana naona sio mahindi tu hata ndizi zipi au niseme migomba. Ukienda kumsalimia bibi Koero basi mpe zake salamu.

Mzee wa Changamoto said...

Basi wapendwa wasomaji Koero ametoka ghafla nami namalizia stori.
Basi siku ya kwanza ikawa ni stori tuuuu huku namueleza mambo meengi kuhusu teknolojia na mambo ya shule na maisha kwa ujumla. Asubuhi yake ni stori na kula. Yaani kwa bibi ni kula na kunywa tuu. Hataki usemeshwe wala nini. MPAKA RAHA. Nilipokaa kwa muda kiasi na "ugeni" kuanza kutoka nikajiona najichanganya zaidi kwenye shughuli ndogondogo kama kuosha vyombo na nyingine za ndani kisha nikahisi nakaribia kukaribishwa kwenye shamba ambalo nimepiga picha hapo. Basi hapohapo nikakumbuka kuwa nahitajika kurejea Dar.Sikuwa nakimbia kilimo, ila nilikumbuka kuwa nimeshakaa vya kutosha kwa bibi.
Hahahahahahahaahaaaaaaaaaaaaa
Shamba zuri Dada. Napenda saana kilimo japo mimi shambani napeleka jembe na si kamera. Mmhhhhhhh.
Kaa salama, kuwa na wakati mzuri na msalimie BIBI KOERO.

SWALI:Kwa hiyo kule upareni unaitwa Bibi? (kwa kuwa umerithi jina la bibi?)

Mwanasosholojia said...

Dada Koero kumbe umechukua jina la bibi!Hongera sana, nawapenda sana bibi zangu ingawa sasa wameshatangulia mbele ya haki. Nimelipenda kweli shamba la bibi yako, nina swali moja labda unaweza kunisaidia, nayaona mahindi (kama sikosei) hapo pamoja na migomba, kwa pamoja vimestawi kweli! Sasa, ikifika kipindi cha kuvuna huwa bibi anavuna kwa wingi pia, kama taswira ya kustawi inavyoonesha?

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Unajua, kizazi cha mama na mabibi zetu ni kizazi chenye nguvu ajabu na kabisa hakikuathiriwa na haya mambo tuliyoletewa na utandawazi. Unakuta bibi kizee kabisa kabisa lakini bado anayo afya nzuri na nguvu tosha za kwenda kufanya kazi katika shamba lake; na ukimkataza na kumletea haya mambo yetu ya kisasa mtaishia kukosana bure. Inafurahisha kama nini. Kizazi chetu sisi tunaoishi kwa deko na kula hivi vyakula vyetu vilivyohandisiwa kibayolojia sijui kama kweli tutaweza kuwa na uwezo wa kuwa na mashamba tukishafikisha umri kama wa Bibi Koero. Shamba hilo limenikumbusha Usukumani. Safi kabisa!

Koero Mkundi said...

Bibi Koero anatimiza miaka 80 mwaka 2010 kama mungu akipenda afike huko, huyu ni mdogo wake na bibi yangu mzaa mama ambaye ametangulia mbele ya haki, ni bibi pekee aliyebaki kati ya mabibi watatu, natamani niishi miaka mingi kama yeye, ukimuona yuko strong na nyumba yake imezungukwa na shamba analima hapo haponymbani na kufuga kuku, ni bibi ambye hakujaaliwa kupata mtoto lakini kutokana na upendo wake kila mtu
anamuheshimu na kumjali. ukiongea
nae ni mtu anayefikiri kabla hajasema kitu na mwenye upeo ingawa hakusoma, na anapenda sana kutumia neno "Nadhani" kabla hajasema kitu. Mama yangu anadai kuwa nimerithi kila kitu kutoka kwake, ingawa sijui kama ni kweli.
Kati ya wajukuu wooote waliochukuwa
jina lake mimi ndio kipenzi chake, nadhani ni kwa kuwa mimi ndiye mdogo kuliko wote, hao wengine wameolewa na wana familia zao.
Kuna wakati baba alitaka kumchukuwa aje huku mjini atulie ale na kunywa lakini Duh! alikataa kata kata, kwa madai kuwa amezoea mazingira ya pale nyumbani kwake shamba lake na vijishughuli vyake vidogo vidogo pale nyumbani, muda mwingi anautumia pale shambani kwake..
Ukifika nyumbani kwake utakuta vitoto vya pale mtaani viko pale nyumbani vinacheza kwani wanampenda sana....
Nimemkumbuka sana bibi yangu......
Nikipata nauli hakika nitaenda kumtembelea........