Sunday, July 12, 2009

WANAWAKE HUPOTEZA MUDA MWINGI SANA KUCHAGUA NGUO YA KUVAA!!!

Hii nimeidesa kutoka katika mtandao wa Jamii Forum, nimeona niwashirikishe wasomaji wa blog hii ya VUKANI na wanablog wenzangu ili kupata ukweli juu ya hili.........

Matokeo ya utafiti uliofanywa nchini Uingereza umeonyesha kuwa wanawake hutumia muda mwingi sana katika maisha yao kuchambua makabati yao kutafuta nguo ipi ya kuvaa wakati wanapotoka majumbani mwao.

Kwa mujibu wa utafiti huo wanawake hutumia muda mwingi sana katika maisha yao wakitafakari nguo ipi ya kuvaa wakati wanapoenda makazini, kwenda 'Out', kwenye vakesheni au shughuli zao za kawaida za kila siku. Utafiti huo uliofanywa na kampuni kubwa ya maduka ya nguo ya Matalan ya nchini Uingereza ulishirikisha wanawake 2,491.

Utafiti huo ulifanywa kwa wanawake wenye umri kati ya miaka 16 na 60 ulionyesha kuwa wanawake hutumia takribani dakika 20 kutoa uamuzi wa nguo ipi wavae kabla ya kutoka kwenda kujirusha mwishoni mwa wiki. Wanawake hutumia dakika 52 kutoa uamuzi wa nguo zipi za kuchukua wakati wanapoenda vakesheni.

Wakati wanapokuwa vakesheni wanawake hutumia dakika 10 wanapoamka asubuhi kuamua nguo ipi ya kushinda nayo mchana na nyakati za usiku hutumia dakika 10 nyingine kuamua kivazi kipi cha usiku cha kuvaa. Utafiti huo ulionyesha pia kuwa wanawake hutumia dakika 36 kuchagua nguo ya kuvaa wakati wa kujiandaa kwenda kwenye sherehe na maharusi. "Kwa wastani wanawake karibia wote hujaribu nguo zaidi ya mbili kila siku asubuhi kabla ya kufikia uamuzi nguo ipi ya kuvaa" ulisema utafiti huo.

Wanawake wanaofanya kazi nao hutumia takribani dakika 15 usiku wa kuamkia siku ya kazi kuchagua nguo ya kuvaa wakati wanapoenda makazini, ulimalizia utafiti huo.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hapa kinachotakiwa kuwa na nguo kidogo au mbili au moja kwa hiyo hhakutakuwa na haja ya kuchagua itakulazimu kuchukua hiyo na kuivaa.

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahahaaaaaa. Asante Da Yasinta. Uchaguzi unatokana na kuwa na nguo nyingi za kuvaa. Kweli kabisa. Lakini haya matatizo ya wanawake yanaanza mbali. Inasemekana (sikumbuki kama ni utafiti ama ni hisia tuuu) kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wa kufanya manunuzi ya gharama za chini japo wanafanya kwa vitu wasivyohitaji. Yaani wana uwezo wa kupata vitu kwa bei poa, ila vitu hivyo vitakwenda kujaza nyumba tuu maana havina umuhimu sana. Sasa kama kati ya hivyo ni nguo, basi hakuna shaka kuwa watasumbuka maana wanakuwa na nyingi kuliko uhitaji. Hivi mwanamke mwenye nguo saba ana shida ya kujua ipi ya kuvaa? Ni kuzipanga za Jumatatu mpaka Jumapili na akiamka ni kuangalia tu kama bado "iko kwenye shepu" ya kuvalika kisha "anajitumbukiza" na kuondoka.
Asante kwa utafiti. Duh!! Nikujuavyo dadangu, naongeza dakika moja na nusu katika kila dakika ya utafiti.
Na hapo hawajaweka dakika za KUJIKWATUA kwa mi-angel face na midubwashika mingine inayowafanya wajibadili na kupoteza utambulisho wao.
Kaaazi kwelikweli

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wanawake kama koero bwana!! duh wanahangaika kurusha tako!!!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

let's pray:

THANK YOU GOD FOR CREATING ME A MAN - amen

Mzee wa Changamoto said...

Hahahahaaaaaaaaaaa. Kamala umenimaliza na sala.
Ameen