Jamani hii sio falsafa ya kaka yangu Simon Mkodo wa Kitururu, kwa hiyo naomba msistushwe na kichwa cha habari hapo juu. Jana nikiwa nimejipumzisha nyumbani baada ya kutoka kanisani, niliamua kufungulia redio ili kusikiliza habari mbali mbali.
Nilipofunga redio nilikutana na kipindi cha watoto kilichokuwa kikirushwa hewani na Redio One, wakati huo ilikuwa ni wakati wa vitendawili, nilijikuta nikivutiwa na kile kipindi kwani kilinikumbusha enzi zile nikiwa mwanafunzi, nilitulia kwenye kiti na kusikiliza kipindi kile.
Mara mwanafunzi mmoja aliyetakiwa kutoa kitendawili chake akasema ‘Kitendawili’
Wenzake wakajibu ‘tega’, na ndipo akasema ‘Vua nguo nikupe utamu’
Yule mwendesha kipindi ambaye alikuwa ni miongoni mwa wale wanafunzi alimkata yule mwanafunzi kalma, na kumuonya yule mwanafunzi, kwa maneno yake mwenyewe alisema, ‘Jamani hivyo vitendawili haviruhusiwi, kwa nini huwaulizi wenzio, muwe mnawaelimisha wenzenu’
Akamchagua mwanfunzi mwingine na kipindi kikawa kinaendelea. Hata hivyo mimi bado nilibaki na swali, Je yule mwanafunzi alimaanisha nini katika kitendawili chake?
Kwa nini hakupewa nafasi ya japo kutoa jibu akiwa Off Air na kisha muongoza kipindi akatoa ufafanuzi? Je watoto walioko majumbani ambao walikuwa wakisikiliza kile kipindi watakuwa na picha gani juu ya kile kitendawili?
Unajua siku hizi kiswahili kimegeuzwa sana kiasi kwamba kila neno siku hizi limegeuka kuwa matusi.
Kwa kawaida watoto ni wadadisi sana na hicho kitendawili huenda watoto wengine waliokuwa kwenye kipindi na wale waliokuwa wakisikiliza majumbani mwao wamewauliza wazazi wao, na kwa bahati mbaya sana mwenye jibu la kitendawili kile alinyimwa haki ya kutoa jibu, Je wazazi watajibu nini?
Mpaka leo bado natafuta jibu la kitendawili kile, mwenye nalo anisaidie……
CCM HATUHITAJI AHADI, TUNAHITAJI MTU MWENYE KUPAMBANIA WANANCHI WAKE - NDG.
ISSA GAVU
-
> CCM Yakemea viongozi wenye kujihusisha na vitendo vya rushwa pamoja na
kukandamiza watu.
" Kwa mujibu wa ibara ya 16 inamtaja nani kiongozi, maana yake...
10 hours ago
18 comments:
Koero nawe, Ok ila kweli kuuliza si ujinga. Nami pia nasubiri jibu ili niweze kuwaambia wanangu....Lol
Mmmmmh!
kwani wewe unafikiri kuna utam gani unaolazimisha kuvua nguo?
Dada yangu Koero, itabidi nikubatize jina la KAPULYA MDADISI.
hata mimi nimefanya udadisi na kuambiwa na wajivi wa vitendawili kuwa jibu lake ni NDIZI....
Na wewe Kamala kama huna jibu utuliage.......
Ramson mie nina swali:- Je ni ndizi ya aina gani?
Ama kweli NAMNA UONAVYO TATIZO NDILO TATIZO. Kwani kulikuwa na tatizo gani kuuliza alivyouliza kama alikuwa na jibu? Na kama ulivyosema Da Koero, wangemuuliza kwanza wakiwa off-air kisha wakatuelimisha kuhusu vitendawili hivi. Kama luha inakua, basi na vitendawili na misemo hukua. Tusitegemee kila siku kuuliza misemo na vitendawili vilevile.
Na kama alivyosema Ramson kuwa kadadisi na kugundua kuwa jibu lake ni NDIZI, basi nani atakayebisha kuwa ukitaka kula na kuujua utamu wa ndizi mpaka uve nguo (maganda)yake? Kuna tatizo la kuelekeza fikra potofu kwenye karibu kila kisemwacho. Kati ya nyimbo nizipendazo ni ile ya Aungurumapo Simba RMX ambayo banza aliweka uhalisia wa maisha yetu japo wapo waliotafsiri kama matusi. Alisema "RAHA YA CHUNGWA, UMENYEWE, KISHA UKATIWE". Mimi ni kati ya walaji wazuri wa chungwa, lakini kila ninapofikiria kulimenya na kubaki na harifu ya maganda baada ya kula najiuliza mara mbili kama "kweli nahitaji kula chngwa wakati huo ama la?'" Na nikimpata wa kulimenya na kukata, NAWEZA KULILA WAKATI WOWOTE. Katika wimbo huo huo, Banza akasema "RAHA YA DAFU, UKISHAKUNYWA YALE MAJI, SHARTI DAU LICHOKOLEWE". Sijui atakayepinga kuwa hu ni ULAJI wa asili wa dafu ni nani? Kama huna kichokoleo kizuri basi ndio ungehitaji "njia m'badala" kama kulivunja kisha ukatumia kichokoleo chako hafifu kulila. Na sehemu nyingine akasema "RAHA YA NANGA BAHARINI, MTONI ITASHIKWA NA TOPE." Kwa sisi tuliokulia kwenye misafara ya majini wajua nanga. Na kwa wavuvi wanajua karaha ya nanga yenye matope. Haimaanishi kuwahuwezi kushusha nanga mtoni (maana waliozoea kuvua mtoni wanafanya hivyo) ila SI KWA RAHA KAMA BAHARINI. Na huo ni ukweli ulio wazi. Sasa kutafsiri vingine na wanavyouliza watu nadhani si tatizo la muulizaji, bali la mtafsiri.
Na naamini VITENDAWILI na MISEMO inaweza kuwa na utata kama zilivyo kauli nyingine nyingi, lakini la muhimu ni kujua kinaulizwa nini na jibu ni lipi.
Kwa jibu la RAMSON naamini walistahili kumuomba msamaha mtoto kwani alijitahidi kuleta kitu chenye utata na ufikirivu wa hali ya juu na angeachwa kujibu, kila mtu angeona ukweli kuwa UTAMU WA NDIZI UKO NDANI YA "NGUO" ZAKE. Na kama wewe wautaka, basi vua uupate. Yaani ukishanunua ile ndizi, shurti uimenye kabla hujaanza kuifaidi uhondo wake.
Naacha
Tuonane NEXT IJAYO
basi nipeni mji na mimi nasema jibu lake ni muwa!!!hahahahaa!
Aaaaaaaaaaaaaaaa. Tena muwa unaweza kuwa na swali la ziada. Kuwa VUA NIKUPE VITAMU KAMA UTAWEZA KUVUMILIA VIGUMU PIA. Si unajua muwa hauliki bila kuvuka kifundo?
Hahahahaaaaaaaaaaaa. Da Scola umemaliza hapa
Da Yasinta nawe kwa vijiswali vya uchokozi....Mhhh!!!! sasa unataka nikujibu nini, maana na wewe hishi kuwa na visa...
Ahsante kaka Mubwelwa mzee wa Changamoto kwa ufafanuzi mziri, naamini mpaka hapo dada yangu Yasinta atakuwa ameelewa sasa....Ila ya dada yangu Schola Mbipa...kaaaaaazi kweli kweli maana kama huko kuvua nguo ili upate vitamu itakuwa ni muwa basi kazi ipo.....
Ila leo kuna jamaa yangu kaja na mpy baada ya kumpa hicho kitendawili ili kupima IQ yake eti kasema kuwa jibu lake ni PARACHICHI.......LOL
Mie bado najifunza tu hapa...Ila dada zangu Yasinta na Schola.....kazi ipo....LOL
Hapa aiwezekani kuwe na jibu moja!
Kwa kuwa kuna vitu kibao ukitaka kuvifaidi inabidi uvivue nguo !
Ingawa vingine ingawa hunoga ukivivua lakini waweza pia kuvifunua tu halafu kwa mrija ufyonze juisi ya ndani ya embe iliyobinywabinywa embe sindano.
Cha kusikitisha ni kwamba tunda ulijualo kwa utamu si lazima ni kweli liwe tamu ukilivua nguo nakulionja! Ndio maana hata kama ni ndizi au muwa; SI kila ndizi na Muwa ni tamu!:-(
Na ukiwa Morogoro msimu wa machungwa ntakushauri utafute ya tokayo kijiji cha Matombo kwa kuwa yanasifa ya utamu kuliko yoyote mengine yatokayo Morogoro.
Halafu inakatisha sana tamaa kama kwa nje ni bomba la mvuto lakini ukionja wastukia uhafifu katika kunoga UTAMU.:-(
KULA NANASI KUNAHITAJI NAFASI.......
Nimekuelewa Ramson lakini bado sijapata jibu kamili ni ndizi aina ganai kwani kuna ndizi za aina nyingi mzuzu, mbanga, kisukari, katuri, kaporota n.k:-)
umenikumbusha wakati nipo shule kule dodoma, jioni mwalimu alizoea kusema wavulana juu wasichana chini akiimanisha hosteli za wasichana zilizokuwa sehemu yenye mwinuko na sisi tulikuwa pande nyingine.ni kiswahili tu na mambo yake ni utata tu. baaada ya kauli hiyo ilikuwa nivicheko tu
Dada Yasinta, nadhani hiyo ndizi itakuwa ni MZUZU.......AU?
Duh!
Naomba nichukue nafasi hii kuwashukuru wasomaji na wanblog wenzangu mliotoa maoni yenu kuhusiana na mada hii....ukweli ni kwamba kama alivyosema kaka Mubelwa mzee wa Changamoto kuwa kiswahili kinapotoshwa kwa sababu ya watu kutaka kuweka maan zao wanzotaka ilhali sio madhumuni ya muhusika.
KUna haja ya kurejea katika kiswahili fasaha bila kupotosha maan halisi iliyokusudiwa.....BLESSING ALL...
Asante
Post a Comment