Wednesday, November 18, 2009

NIKAPIGIWA “EMCHEKU”

Usiku ndio muda muafaka

Ni usiku wa saa tatu hivi, niko kijijini kwa bibi Koero, na tuko jikoni tunaota moto, huku akinisimulia simulizi mbalimbali juu ya maisha. Bibi Koero ni hodari wa kutoa simulizi zenye kufundisha na za kusisimua.

Tukiwa katikati ya mzungumzo, mara tukasikia michakato ya miguu huko nje kuashiria kuwa kuna mtu huko, “Emcheku aha” ilikuwa ni sauti ya kiume kutoka nje, bibi aliniambia nitoke ili kuangalia kuwa ni nani.

Nilipotoka, kwa kuwa kulikuwa na giza, niliona kivuli cha mtu, lakini alikuwa na kurunzi yenye mwanga hafifu, na alikuwa akiiwasha na kuizima, nilirudi ndani kwa hofu na kumweleza bibi Koero mauzauza niliyokutana nayo huko nje.

Bibi Koero alicheka sana, na kuniambia kuwa, huyo ni mgeni wangu, kaja pale kuposa, na mlengwa ni mimi kwa kuwa hakuna binti mwingine pale nyumbani bali ni mimi.
Nililishangazwa na aina ule ya posa, kwangu mimi ile ilikuwa ni habari, na ili kujua mengi zaidi, nilimdadisi bibi Koero ili anisimulie juu ya utaratibu huo.

Bibi Koero anasimulia kuwa enzi zao, binti akivunja ungo, vijana huanza kufika pale mida ya usiku kupiga hiyo “Emcheku” inawezekana wakafika zaidi ya wavulana kumi kwa usiku mmoja kulingana na uzuri na tabia ya binti huyo.
Emcheku ni salaam ya heshima anayotoa mvulana anapokwenda kuchumbia.

Kwa kawaida wavulana hao wakifika kila mmoja kwa muda wake na kupiga hiyo Emcheku, Binti husika huambiawa atoke nje kuonana na mvulana huyo na kama hajampenda basi humweleza na huyo kijana huondoka zake, na akitokea mvulana anayempenda, basi hupewa ruhusa na binti huyo ili alete Posa na hapo ndio milango hufunguliwa kwa mvulana huyo kumtembela mchumba wake.

Mara nyingi matembezi hayo hufanywa usiku na mvulana akifika binti huruhusiwa na wazazi kutoka nje ili kuzungumza na mchumba wake, lakini walikuwa hawaruhusiwi kukutana kimwili au kuonjana mpaka utakapofika muda muafaka watakapofunga ndoa takatifu.

Tofauti na zamani, bibi Koero, anasimulia kuwa, siku hizi vijana wamebadilika sana na wengi wameuharibu utaratibu huo na kuugeuza kuwa kichaka cha kufanyia ngono. Wavulana siku hizi kama anamtaka binti, hupiga hiyo Emcheku na binti akiridhia, humhadaa, mpaka amuonje na akifanikiwa kuingia mitini na posa inaota mbawa.

Unaweza kukuta mvulana anawahadaa wasichana zaidi ya kumi lakini aisoe hata mmoja baada ya kuwaonja.

Wasichan nao wamekosa subira, kila wakisikia hiyo emcheku, wanajua kuwa ni bahati imewajia, kumbe hakuna lolote ni wavulana mafisadi tu wenye uchu wanataka kuwaonja na kisha kutoweka.

Sasa sijui na mimi nilipigiwa hiyo emcheku ili kuonjwa……LOL

9 comments:

Ramson said...

Sasa Koero, kumbe na mimi nikija kwa mzee Mkundi na kupiga hiyo mcheku, bahati yaseza kunidondokea eh!!

Mcheku...teh teh teh.....
Kaazi kweli kweli binti

Yasinta Ngonyani said...

Mmmmmh! Zamani ilikuwa safi sana kwa kweli. Maana siku hizi kazi kwelikweli wanaume bila kuonja haiwezekani. Ninashangaa sana siku hizi vijana wanachumbia na halafu anamchukua binti na kuishi naye na baadaye anampa mimba na kuzaa mtoto kabla ya ndoa. Wakati zamani ilikuwa kinyume kabisa yaani mpaka siku ile ya ndoa hapa ndo mtaanza kuonjana. ngoja niache niwape na wengine nafasi.

MARKUS MPANGALA said...

SIJUI

PASSION4FASHION.TZ said...

Hahahahaa,Koero na vijihadithi vya bibi Koero,safi sana nimecheka ila ni nzuri sana,kwetu ni "Chagolaga"huko hakuna Emcheku ni ngoma na ngoma huanza mchana na kumalizika jioni giza linapoingia,sasa baada ya hapo ndio chagolaga inaanza kama huwezi kukimbia kazi kwako.

Faith S Hilary said...

looooooooooool!!! mbavu sina baada ya hiyo sentensi yako ya mwisho hehehehehhee..ila hii iko very interesting...

Mzee wa Changamoto said...

Sasa unatoka bila tochi unaenda kuongea na huyo "emcheku"zi bila kumuona?
Dah!!!
Ama kweli kuishi kwingi ni kuona, kusikia, kutunza kumbukumbu na kusimulia mengi
Hahahahaaaaaaaaaaaa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Kuna chagulaga, niangusage, sasa emcheku.kuna kushobela kule kwetu na kusherera. Yasinta nakoero mnaonekana kuchukia kuonjesha, kwani hamjawahi onjwa nyie?

aliwahi kuuliza swali ndg mwaipopo kuwa ukinunua gari kabla ya kukubali huruhusiwi kuendesha angalau km5 tu hivi?

ni mwanamke gani anayekubali kuolewa bila kujua ukubwa/uzuri/urefu/udogo na hata suru ya kifaa cha kum-emchekusa?

Mzee wa Changamoto said...

Simo

Simon Kitururu said...

eemcheku wee!:-(