Wednesday, November 11, 2009

SIKU YA KUFA KWANGU!


Wengu tunaogopa kifo!

WAKATI NASOMA HIKI KISA KWA MARA YA KWANZA NILIOGOPA SANA, LAKINI KUNA KITU NILIJIFUNZA, HATA WEWE UNAWEZA KUJIFUNZA PIA.



Naomba wakati unasoma hii habari uwe peke yako na uwe umetulia, bila kubughudhiwa.
Hakikisha hakuna unaloliwaza wakati unapoanza kusoma kwani hiyo itakusaidia kung’amua kile ninachomaanisha katika habari hii.


Naomba usiwe mwoga, kwani ni habari ambayo itakufunza jambo fulani katika maisha.
Haya ungana nami katika kusoma habari hii.


Katika akili yako hebu hisi kama vile unajiona, yaani tengeneza taswira kama vile unajiona ukiwa unaenda kuhudhuria mazishi ya mtu umpendae na unayemfahamu. Jione ukiwa unaendesha gari kuelekea kanisani ambapo ndipo mahali watu wanapokusanyika kuuaga mwili wa marehemu kabla ya mazishi.


Unapofika pale unapaki gari lako na kutoka kuelekea ndani ya kanisa, unapoingia ndani ya kanisa unaona kumepambwa na maua mazuri yenye kunukia na huku ukisikia ala za muziki mororo. Wakati ukielekea kwenye eneo ulilopangiwa kukaa unawapita ndugu, jamaa na marafiki wakiwa na nyuso zenye huzuni na majonzi yenye kuashiria kusikitishwa na kuondokewa na mtu waliyempenda sana.


Unapokaribia kufika kwenye nafasi uliyopangiwa kukaa, unapita karibu kabisa na sanduku lenye mwili wa marehemu na unapotazama mwili ulioko ndani ya sanduku hilo unastuka kuona mwili ulioko ndani ya sanduku hilo ni wa kwako!
Mara kuna sauti inakwambia "haya ni mazishi yako yatakavyokuwa miaka mitatu ijayo kuanzia sasa"


Watu wote walioko pale wamekuja kuonyesha mapenzi yao kwako na kukupa heshima kwa kuuaga mwili wako ili ukapumzike kwa amani.


Duh! Unashusha pumzi na kuketi, ili kusubiri ibada ianze. Unapoangalia ratiba ambayo ulipewa wakati unaingia pale kanisani unakuta wamepangwa wazungumzaji wanne, wazungumzaji wa kwanza wanatoka katika familia yako, mmoja wa watoto wako, mmoja wa kaka zako, dada zako, binamu, shangazi, mjomba, baba mdogo, mama mdogo, bibi, babu na ndugu wengine wa karibu ambao walisafiri maili nyingi ili kuja kushiriki mazishi yako.


Mzungumzaji wa pili ni mmoja wa marafiki zako ambaye mlishibana sana, mzungumzaji wa tatu ni kutoka katika mahali pako pa kazi na mzungumzaji wa nne ni kutoka katika kanisa unalo Sali au kutoka katika taasisi ya kijamii ambayo ulikuwa ukishiriki katika kuihudumia jamii baada ya muda wako wa kazi.


Sasa hebu fikiria kwa makini sana. Ungependa wazungumzaji hawa wazungumze nini juu ya maisha yako hapa duniani? Wewe ni mume, mke, baba au mama wa aina gani? Wewe ni mvulana, msichana, binamu, wa aina gani? Ni rafiki wa aina gani? Ushirikiano wako na wafanyakazi wenzako ulikuwaje?


Ungependa wakuzungumzieje? Ulikuwa ni mtu mwenye tabia gani kwa ujumla? Uliisaidiaje jamii, ulifanikiwa katika lipi? Ungependa wakukumbuke kwa lipi? Hebu waangalie kwa makini watu waliokuzunguka. Kama ungepewa nafasi, ungeyabadili vipi maisha yao?
Kama umesoma kwa makini habari hii naamini kuna jambo utakuwa umejifunza.
Nimegundua kuwa ili ujue kuwa wewe ni mtu wa namna gani ni vyema ukahudhuria mazishi yako mwenyewe………………


Tafakari…………….


Habari hii nimeitoa katika kitabu cha The 7 habits of highly effective people cha Stephen R Covey.

4 comments:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hili ni bonge la meditation kwani meditation ni sawa na kufa kidogo wakati mwingine!!!!!!!!!!!!!

watu wengine watasema nini mimi hainihusu na kinachonihusu ni mimi ambaye sipo.

Yasinta Ngonyani said...
This comment has been removed by the author.
Mzee wa Changamoto said...

Mmmmmhhhhhhhh!!!

MARKUS MPANGALA said...

Ni kama ile ya MALAIKA WA SHETANI simulizi ya kitabu cha BEN MTOBWA. Sasa umekufa siyo, watu wanakuongelea huku ukiskia au? Ndiyo lakini sina hakika kma kuongelewa mabaya kuna taswira mbaya miongoni mwetu maana mabaya hayo yapo kati yetu na tunachagua sisi wanadamu. Ama tuchukie mabaya/makosa na kuwapenda watenda makosa? Maana mabaya yanataengenezwa hayajitengenezi waungwana.

Na pengine inafaa wanadamu tukajifunza kuchukia kwani tunaweza kufundishwa upendo, kwahiyo usimchukie mtu bali chukia makosa yake ya kuchukia.... hakika utamfunisha upendo.

Usiogope kwani kila lililopo duniani ni mali yetu, lakini tujiulize tukishazungumziwa vema/vizuri kwamba tumkuwa waungwana... je inabadilisha nini katika nafsi zetu?

Au labda tunakamatana na uungwana huo? lakini ungwana na binadamu haviambatani bali sisi tunadhani tunaambatana na uungwana.

mmmmmmhhhhh weeeeee mzee wa Lundunyasa kalale hukooooo lione.