Monday, January 4, 2010

HAIKUWA BAHATI, BALI MKOSI-SEHEMU YA MWISHO


ILIPOISHIA........

Kwa kifupi nilianza uhusiano na yule mzee na alinishauri niache kazi kisha akanitafutia nyumba kubwa nzuri maeneo ta Mikocheni.

ENDELEA KUSOMA HAPA..........

Nililazimika kuacha kazi baada mpenzi wangu kunifungulia miradi ya Duka la nguo (Boutique) maeneno ya Msasani na Salon ya kike kubwa na Mini Super market, na miradi yote hiyo ilikuwa maeneo ya Kinondoni.

Kwa mida mfupi maisha yangu yalibadilika na kuwa ya juu, nilikuwa namiliki magari matatu ya kifahari na na nilinunua Kiwanja maeneo ya Mbezi beach na kuanza ujenzi bila kumshirikisha yule mzee, ambaye ndiye mfadhili wangu.

Siku moja jioni nakumbuka ilikuwa ni Jumapili wakati nikiwa nimejipumzisha nyumbani, nilisikia mlango ukibishwa hodi, nilimtuma mfanyakazi wangu wa pale nyumbani akafungue mlango. Mara aliingia mama mmoja wa makamo hivi.

Alikuwa ni mama wa heshima, nilikmaribisha sebuleni na kumuuliza kama angependa kinyaji gani, alikataa kupewa kinyawaji chochote, lakini alionekana kuzungusha macho huku na huko kama vile alikuw aanakagua kitu, nilimuacha amalize hamu yake kwani nilidhani alivutiwa na mapambo ya pale sebuleni.

Baadae alisema, “Nadhani wewe ndiye Gifti kama sjakosea” nilimjibu kwa utulivu kuwa ndiye mimi….alishusha pumzi na kusema, “Je unamfahamu Mzee Alex?” Nilishtushwa na swali lile na nilijihisi mapigo ya moyo wangu yakienda mbio, lilikuwa ni swali la Kushtukiza sana. Nilijikakamua na kumjibu kuwa simfahamu mtu huyo.

“Sikiliza mwanangu, wewe ni sawa na binti yangu, na sijui wa ngapi, maana unaonekana kuwa bado u binti mdogo sana, kwa umri ulio nao haistahili kutembea na wanaume za watu tena baba zako ambao wanaweza hata kukuzaa, mbona vijana wenzio wako wengi tu, kwa nini usiwatafute hao, mpaka utembee na mume wangu? Nimeishi naye miaka zaidi ya 40, leo hii binti mdogo wa kukuzaa unataka kunivunjia ndoa yangu?” Aliniambia kwa upole kama vile mama aongeae na bintiye

Ukweli ni kwamba maneno yale yalinishtua sana, nilijikuta nikiwa nimemkodolea macho. Nakumbuka niliwahi kumuuliza mzee Alex kuwa familia yake iko wapi na alinijibu kuwa inaishi nchini Malawi na watoto wake wanasoma nchini Uingereza.

Nilikuwa najivinjari na huyu mzee kwa uhuru hasa na sikuwa na wasiwasi kuwa kuna siku nitakuja kukutana na mtu ambaye angekuja kunikabili na kuniambia kuwa natembea na mumewe.

“Mama samahani naona umepotea nyumba huyu mzee simjui na wala sijui unamzungumzia nani hapa,……tena nakuomba uondoke maana mume wangu atarudi hivi punde asije akakufanyia jambo ambalo utalijutia maishani mwako” Nilijikakamua na kumjibu yule mama kwa upole.

"Binti sikiliza, sipendi niingie kwenye kubishana na wewe, wakati ninao ushahidi wa kutosha kuwa unatembea na mume wangu, lakini……..sikutaka kulisema hili, ila kwa kuwa unaonekana mkaidi, nitakueleza,............ mume wangu si salama, ni muathirika, naomba ukapime afya yako, ili uanze kuishi kwa matumaini” alimaliza kusema na kunyanyuka ili aondoke.

Moyo ulinilipuka na nilijikuta nikiropoka, “He, Mzee Alex ni muathirika?” nilijikuta nikiongea kwa sauti.
"Huna haja ya kukata tamaa, bado unayo nafasi ya kuishi, nenda kapime, mimi nilijigundua miaka kumi iliyopita na mpaka sasa ninaishi kwa matumaini, hata wewe unayo nafasi hiyo” Yule mama alinijibu kwa upole na kisha aliondoka zake na kuniacha nikiwa nimeduwaa, nisijue la kufanya, nilikurupuka na kwenda chumbani, nilimeza vidonge vya usingizi na kujitupa kitandani.

Niliamka usiku wa manane kama saa nane za usiku hivi, nilikuwa na njaa, nilikwenda jikoni nikajitengenezea mkate wa nyama na juisi nikala, kisha nikakaa kitandani na kuanza kutafakari maneno ya yule mama. Niliona kama vile ile ilikuwa ni ndoto na huenda ingekwisha muda wowote, lakini hapana haikuwa ni ndoto ulikuwa ni ukweli mtupu.

Siku iliyofuata nilimpigia mzee Alex simu lakini haikupokelewa nilituma ujumbe lakini hakujibu, baadae alinijibu kuwa yuko nchini Uingereza na angerudi baada ya mwezi mmoja, kuanzia siku hiyo namba yake ilikuwa haipatikani na mawasiliano na yeye yakakatika, nikaachiwa segere nilicheze peke yangu.

Namshukuru shangazi yangu aliweza kuniliwaza na kunipeleka kupimwa na kweli niligundulika ni muathirikawa ukimwi, na ninaishi kwa matumaini sasa. Sijaanza kutumia dawa ila najitahidi sana kula vyakula vizuri na kufanya mazoezi.

Kwa kweli nina wakati mgumu sana, kwani kwa jinsi muonekano wangu ulivyo, nasumbuliwa sana na wanaume vijana na wazee, wananitaka kimapenzi na wengine wanataka wanioe, na nikiwaambia kuwa mimi si salama nimeathirika, wanabisha kabisa na wengine wanadiriki kusema hata kama nimuathirika hakuna shida hata akifa powa tu lakini atakuwa amefaidi. Yaani nashindwa kuwaamini wanaume, tena wengine wameoa na wana familia zao, lakini we kutwa kunivizia.

Namshukuru mungu nimemudu kujikubali na kuyakubali matokeo, najua ni lazima nitakufa, siku moja lakini namshukuru mungu kwa kunipa ujasiri huu nilionao mpaka sasa nimemudu kuishi kwa amani na kuepuka vishawishi.

Nawaasa vijana wenzangu hasa mabinti wa shule kuwa sio kila king’aacho ni dhahabu, ukimwi upo na unaua, tujiepushe nao.

***************MWISHO************

7 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Kusoma hapa pia kumenikumbusha mahubiri fulani ya Pastor mmoja (Joel Osteen www.joelosteen.com) ambaye alisimulia kisa cha jamaa mmoja ambaye alinusurika kufa na baada ya hapo Dk akamwambia ana miaka kadhaa ya kuishi. Alichofanya ndugu huyo ni kuhesabu siku zilizopo katika miaka hiyo na kuelekea baharini ambapo aliokota idadi ya vikonokono sawa na siku alizohesabu na kuziweka kwenye bilauri la kioo na kisha kuliweka pembeni na awekapo mswaki. Kila asubuhi akiamka wakati akipiga mswaki huchukua kimoja na kutupa. Pale alijifunza kuthamini kila siku ipitayo kwani kila alipotupa kimoja, alijua namna vinavyopungua.
Na mimi ndivyo nilivyo sasa.
Kila nisomalo hapa NALISOMA KWA UMAKINI ZAIDI BAADA YA KUWEPO UWEZEKANO WA KUKUKOSA NA KUKOSA HABARI / HADITHI ZA KUSISIMUA KAMA HIZI
Hii imefunza mengi kuliko kuburudisha, japo mfumo wako wa kusimulia ndio ufundi mkubwa.
Kuna maswali mengi watu wanaweza kujiuliza kuwa "kweli hakushitukia zawadi zote zile?" lakini unapokuwa katika "tundu bovu" ni ngumu kuona hilo hasa kwa jicho la kibinadamu.
Tunalohitaji ni kuongozwa na ndani mwetu kuliko nje. Kuongozwa na MOYO KULIKO MAHITAJI na hili litasaidia saaana kuepusha mambo kama haya.
Nawaza kama wa kulaumiwa ni mchumba aliyeonesha kumutesa wakati kuna anayeonekana kuwa "pumziko" upande wa pili ama kama kumtesa na kumkimbia ndio salama ya kaka huyo maana kama dada huyu angeendelea na mahusiano na Baba huyo huku akiendelea na mpenzi wake basi sasa hivi waathirika wangekuwa mmoja zaidi ya tufahamuvyo (japo hatujui kama hakuwa ameathirika kabla na kama mpenziwe hajaathirika mpaka sasa)
LAKINI YOTE JUU YA YOTE, ni kuwa Shangazi yetu amekubali hali, analinda wengine na ameamua kuwa mkarimu wa kutosha kutushirikisha habari yake hii yenye mafunzo makuuubwa kwetu
Namshukuru saana Aunt "Gift" na nina hakika kuwa kwa kuwa amekubali hali halisi, basi ataishi kwa matumaini na wengi watajifunza toka kwake.
Kama nilivyosema nilipoandika kuhusu Kaka Kamala, kuna sababu ya kwanini yamemkuta yeye na sio mimi na wewe. Labda mimi ama wewe tungejiua na wengine wasingejifunza toka kwangu ama kwako, lakini ona alivyo jasiri kuikubali hali, kutoambukiza na sasa anaelimisha
MLANGO ALIOFIKIRI ULIFUNGULIWA BAADAE AKADHANI UMEFUNGWA ILA NAONA NDIO UMEFUNGULIWA ILIWENGINE WAJIFUNE
Much Luv Lil Sis
Blessings

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kama asemavyo kijana wa changamoto, kila post ni muhimu.

dada wa watu alifurahia maisha na akupenda kutawaliwa na masikini maishani mwake ehe!

harafu unasema ni love for!

MARKUS MPANGALA said...

Jamani jamani jamani wapo watu jamani lakini imenigusa Malawi?....ngoja nakunywa maji................, eheee jamani mwingine alipelekwa kusoma London aligharimiwa kila kitu mtoto wa kike yule mwanzo alimnyima mzee wa wayu akimtunzia kidume chake, lahaula yule mzee akawa anamtembelea kule London, na kama ujuavyo eti wanawake wanahuruma sana, duh mtoto wa kike akampatia tunu baada ya kuombwa naye akatafakari kuhusu ukarimu bandia wa mzee yule, jamani mtoto wa kike mwaka wa 3 sasa najiuguza analia pale Samora, hana wa kumlaumu bali mwenyewe.....

lakini tunawezaje kuepuka vishawishi? Tunawezaje kuwaepuka washawishaji? je washawishiwa tunachukua hatua gani? kipi kinaongoza maisha yetu hata kama hatuwezi kuwadhani mabaya watu? ni kwanini mtu uliyetarajia akufute chozi ndiye aliykufanya ukalia, utafanye?

kimsingi ni kuikubali hali haina maana sana kujihukumu hata ukasababisha maumivu ya mwili.

NGOJA NIMUUNGE MKONO KAKA MZEE WACHANGAMOTO...KWAMBA KULIKUWA NA UWEZEKANO WA KUSHTUKIA.....LAKINI KWELI ALIGOMBEA DOLA HUKU AKIJUA MAHABUBA WAKE ANAJUA KUWA ANAJAMBO NALIFICHA.
AAAHH YAMESHATOKEA. MUNGU AMSAMEHE DUH! BONGE KITABU HILI KOERO!

ONYO; BADO NAMTAFUA DADA ASIMWE!!!!!!!

Mija Shija Sayi said...

Shetani ana akili kishenzi, huvizia pale udhaifu wako ulipo ndiyo maana hutoa vishawishi tofauti tofauti kwa watu tofauti, lakini tusisahau kwamba Mungu wetu naye yupo kutulinda na kutuundia ujanja wa kukabiliana na akili za shetani, ndiyo maana anatuambia TUKESHE TUKIOMBA KWA MAANA KWA NGUVU ZETU PEKEE HATUNA UBAVU WA KUMSHINDA SHETANI. Halafu tunaona kama utani vile, ndo kama haya sasa.

Anyway...

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe mija na shoka zako, shetani ni nani na \mungu ni nani pia? ehe mbona unawalaumu wakati hapa kuna mzee Alex, mkewe na kakimada kanakotamani mailioni, unawaita shetani? yaani mtu atoe hela, demu apokee avue nguo nakutandaza miguu wewe useme shetani???

Thidanganyiki mimi ehe

Mija Shija Sayi said...

Shauri yako Kamala..

MARKUS MPANGALA said...

Uapnde wa pili wa maoni yangu, niliwahi kutoa hoja ya HUDUMA. kwamaba wapo watu wanajenga mapenzi kutokana na huduma na kama ilivyo hapa. na wengine wanadhani ni rahisi kujinasua kwa haya kama ilivyotokea. Nina hakika pamoja na kumlaumu mzee Alex, ninaweza kumtazama binti kwa msikitiko na lawama pia.

ukisoa msimamo kama hivi unaweza kujikuta kila jambo linakujia kwasababu tuya heri na baraka. na labda tuaminivyo mungu hasemi nae kwa haraka bali amekupa akili ya kuamua na kutambua