Friday, January 15, 2010

NAJIVUNIA KUMFAHAMU

Alikuwa ndiye mtu wa kwanza kuniandikia email binafsi akinikaribisha katika ulimwengu huu wa blog, hiyo ni baada ya kusoma ujio wa blog yangu na kutoa maoni yake akinitia moyo.
Kama haitoshi kaka yangu huyu alidiriki kuitangaza blog hii ya Vukani kupitia blog yake ili kuiweka katika ramani ya ulimwengu wa wanablog,
Alizaliwa Aug 10, miaka thelathini iliyopita katika hospitali ya Brackenridge iliyopo AUSTIN, TEXAS. U.S.A
Brackenridge Hospital. Austin, TX (kama ilivyoonekana Aug 1980)
Ni mtoto wa tatu kati ya watano katika Familia ya Mzee Simon na Mama Paulina. Ametanguliwa kuzaliwa na Dada wakubwa wawili na kufuatiwa na kaka zake wadogo wawili (mapacha)

Familia nzima atokayo kijana huyu.
Alianza shule ya awali maarufu kama "vidudu" Lutheran Junior Seminary mpaka alipojiunga darasa la kwanza Shule ya Mazoezi Kigurunyembe. Baadae alihama na wazazi wake kwenda Nachingwea Lindi na kujiunga na Shule ya Mazoezi Nambambo, shule ambayo ndipo alipomaliza elimu ya msingi.
Elimu yake ya Sekondari aliipata katika shule za Ndanda Masasi Mtwara na Ihungo na Iluhya zilizopo Bukoba Kagera. Kisha akaenda Dodoma kwa mafunzo ya ufundi katika fani ya ufundi mitambo, utengenezaji vipuri na ukerezaji (Fitter Mechanics) ambayo aliisomea kwa miaka minne na kupata Grade One. Pia akiwa hapo chuoni alijifunza Ufundi Magari (Motor Vehicle Mechanics)
Alirejea Dar na kuendelea na pilika nyingine na mwaka 2001 alipata kazi katika kituo cha redio maarufu cha 100.5 Times Fm ambapo alikaa mpaka mwaka 2003.

Kaka yangu huyu hakuridhika na maaarifa aliyokuwa nayo hivyo aliondoka nchini na kuelekea nchini Marekani, nchi ambayo ndipo alipozaliwa ili kutafuta maarifa zaidi.
Kwa sasa yuko shule nchini humo akichukua masomo ya awali ya fani ya UHANDISI, huku pia akifanya kazi ambayo haiko mbali na fani hiyo. Ni mtengeneza vipuri katika kiwanda kinachojishughulisha na vipuri vya ndege cha Eaton Aerospace kilichopo Beltsville Maryland.
Nilipofanya mahojiano naye alikiri kuipenda zaidi fani ya uandishi wa HABARI na UHANDISI na anajitahidi kuchukua masomo ya wali yatakayomuwezesha kuunga fani zote.
Kwa upande wa starehe alisema kuwa yeye sio aina ya vijana wanaopenda kujirusha au kuendekeza starehe, bali ni kijana mwenye kipaji halisi cha uandishi wa habari za kijamii, uchambuzi katika medani ya kisiasa na kiuchumi pamoja na habari za kisaikolojia kupitia ukurasa wake binafsi maarufu kama Blog na kama akikereka, kufurahi, kusikitika au akiwa katika mood yoyote ile anapenda zaidi kusikiliza muziki wa kihisia, maarufu kama Reggae.
Anasema muziki huu HUFUNZA, HUBURUDISHA NA KUIKOMBOA JAMII TOKA UTUMWA WA KIAKILI.
Pia alikiri kuwa kwa sasa anayo familia, akiwa na mpenzi wake wa tangu mwaka 2001 aitwae Esther na hivi karibuni wamepata baraka ya mtoto mmoja aitwae Paulina Arianna.
Katika maisha tunayoishi yapo matukio ambayo hututokea, yapo ya kufurahisha na ya kukera au ya kuhusunisha. Mengine unaweza kuyasahau na mengine ni vigumu kuyasahau. Tukio ambalo kaka yangu huyu itakuwa ni vigumu kulisahau ni lile la ajali aliyoipata Disemba 22, 1999 nchini Kenya katika eneo la Nakuru kilomita chache kutoka jijini Nairobi, wakati alipokuwa akisafiri kuelekea Bukoba kula sikukuu na wazazi wake.
Ajali hiyo ambayo ilihusisha basi la Tawfiq na lori ambalo lilipaki njiani ilisabababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na kuacha majeruhi kadhaa akiwepo yeye ambapo amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya mgongo hadi leo, unaweza kuBOFYA HAPA ili kujua yaliyomkuta kaka yangu huyu.
Ni jambo la kujivunia kwamba pamoja na ajali hiyo ameweza kusimama na kuendelea na shughuli zake huko ughaibuni huku akiendelea kubukua kwa ajili ya kujikusanyia taaluma ili aweze kuisaidia jamii hii ya Kitanzania na dunia kwa ujumla.
Najivunia sana kumfahamu na najivunia kupendwa na yeye kwani kwangu mimi huyu ni zaidi ya kaka na nimenufaika sana na mchango wake, kwani ametumia muda wake mwingi kunikuza katika tasnia hii ya blog.
Napenda kumuombea maisha marefu yenye baraka na fanaka ili atakaporejea nchini tupate kufurahi kwa pamoja na kumshukuru mungu, maana neema zake ni za milele.
Ahsante sana kaka Mubelwa Bandio nashukuru kukufahamu

11 comments:

Simon Kitururu said...

Mkuu Mubelwa Bandio mawazo yake ni bonge la shule kwangu! Na asante Dada Koero kwa kutugawia dondoo nyingine zijaziazo maridhawa kuhusu huyu Kaka.

Yasinta Ngonyani said...

Koero nafurahi kwa kutuhabarisha habari za mwanakaka huyu ni kweli. Ahsante.Nami nasema najivunia wewe mdogo wangu kwa yote ututendeayo. Ubarikiwe sana.

Mzee wa Changamoto said...

Wow!!
Asante saana Kaka Mkodo. Unajua kuwa umenifunza mengi kwenye blog hasa ujanja wa Video na Sauti. Wapo wasiojua kuwa wakati naanza ku-blog sikujua hata namna ya ku-post picha, muziki na videos na isingekuwa ninyi (wewe, Da Subi, Kaka Jeff Msangi) nisingekuwa naweka niwekavyo pale. Nuff Respect to y'all.
Dada Yasinta umekuwa chachu kwenye habari za maisha. Yaani kuifanya "kila habari ndogo kuwa habari kubwa". Ni kama asemavyo KOJO NNAMDI kuwa "where every local news is international news". Kwako nilijifunza kuthamini habari "ndogo" zinazowahusu "watu wadogo" ambao ndio jamii kubwa na ambayo natoka mimi. Kwa hiyo nilijifunza KUJITHAMINI.
Koeroooo!! Nimeshakwambia "USIJISHUKURU KAMA MWENDAWAZIMU". Wewe hua la kunishukuru wala kujivunia kuhusu mimi. Ni mimi na sisi tunaojivunia zaidi uwepo wako. Nilichofanya ilikuwa ni wajibu wangu na ujue kuwa HATA KAMA NISINGEKUANDIKIA EMAIL AMA KUKUTANGAZA KWENYE KIJIBARAZA CHANGU KISICHO NA WASOMAJI WENGI ZAIDI YENU WANAFAMILIA bado watu wangekujua, wangekusoma na wangekukubali kama ambavyo unakubalika sasa na utaendelea kukubalika.
Nahisi nimekuwa na familia kuuubwa baada ya ku-blogu na nimeerevuka na kupevuka kwa kulazimika kusoma na kuelewa nitakiwacho kusoma kabla sijaweka na kutoa maoni.
Huu ni mchanganyiko wa ufahamu wa hali ya juu ninaoupata toka kwenu wanafamilia.
Nawapenda nyote, nawaheshimu na Asante kwako Da Mdogo Koero kwa kutoa muda kusikiliza ya wengi (nikiwemo mimi)
Nakupenda, Nakuheshimu na Nakuombea kama nifanyavyo kwa wanafamilia (bloggers) wengine
Blessings

Albert Kissima said...

"kuna nguvu iliyo ndani mwetu isiyo na nguvu inayohitaji nguvu miongoni mwetu" na kuna posti nyingine kama mbili hivi zinazoongelea hii nguvu. Ni kati ya posti nilizozipenda sana pale katika kibaraza cha Mzee wa Changamoto. Ipo pia ile ya kuzitaja blogs mbalimbali,zilitajwa kistaa,kitaalamu na ktk hali eeeh ya kuvutia saaaana.
Kwa kweli namna apangiliavyo blog yake ni "changamoto yetu" sisi sote,angalia tu, WALIWAZA NINI,THEM AND I(Hii sijaiweka vizuri,nakiri, atanisaidia),n.k.


Tuonane NEXT IJAYO.

Godwin Habib Meghji said...

Very interesting, Sikuwahi kufikiri Mzee wa changamoto ni MUANDISI. siku zote nilijua ni MUANDISHI. Hii ni kutokana na uwezo wake mkubwa wa uhandishi na uchambuzi wa habari. HIVI MIMI NDIO NINAVIITA VIPAJI.

Faith S Hilary said...

No words can describe what a wonderful person he is. Ni hayo tu :-)

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mnayoyaona na kuyasoma katika mtandao wa changamoto mbona hayaonyeshi hata 1/6 tu ya ukomavu wa kifikra na kimtazamo wa huyu mchangamotoshaji makini? Nendeni kwenye mitandao ya kimijadala kama Wanabidii.net, Strictly Gospel na kwingineko ndiyo mtafahamu kwa nini huyu kijana anaitwa "Mzee wa Changamoto". Ngoja niishie hapa!

Mzee wa Changamoto said...

Kaka Albert. Haya niandikayo ni maisha nikumbanayo nayo. Kisha twawashirikisha wengine. Lakini maisha haya nayaandika niyaandikavyo baada ya kudodosa dodosa mawili matatu toka kwenu. Kisha najifanya kuja na yangu lakini ukweli ni MUUNGANIKO WA MAANDISHI MENGI NISOMAYO KWENU. (Umenifanya notoboe siri. Lol) Wewe twa-chat almost kila lunch break yangu na najifunza mengi toka kwako. Nuff Respect to ya My brother.

Kaka Godwin. Wala mimi si mhandisi. Ndio "naota" kuwa mmoja wao na ndio naanza masomo ya awali. Ila box la hapa na uhitaji wa kimaisha wanifanya nipunguze kasi. Itanichukua muda kuliko wengine lakini naamini nitafika tuuu. Tunatakiwa kuonana punde kaka. Wewe ni chachu yangu kwenye mambo ya kusaka elimu. Nasubiri siku ya siku. Blessings.

Dada Faith. Aaaaaaawwwwww!! (FB Style)
Kila nikisoma hapo najihisi nshakufa. Si unajua sifa hizi hatujazoea kuwapa walio hai? Lakini umenionesha njia kuwa unaweza kusifia hata kabla msifiwa hajafa. Thanx for daily buzz and chat on FB. Holla to my hero.

Kakangu Mwalimu Matondo. Wewe nimejaribu kukuiga ustadi wako wa kueleza mengi kwa aya chache na fupi sijaweza. Ndio maana story zangu zawa ndefu kiasi cha kuwashinda "skimmers" kuzisoma na matokeo yake nadhani uelimishaji unabaki kwa walioelimika maana wanapenda stori ndefu. Lakini uwepo na ushiriki wako (pamoja na Mwl Mbele) vimeleta changamoto na kuinua morali yetu kujua hata mimi nisiyejua kitu zaidi ya kusoma na kuandika nasomwa na wanaofundisha kufikiria kabla ya kuandika.
Una mchango mkubwa saana kwa haya yatokeao.

Nyote nawarejeshea UPENDO na kila siku NAWAWEKA KWENYE SALA ZANGU. Kwani ni ninyi mnifanyao mimi kuwa mimi.
Nawapenda, Nawaheshimu na nawaombea pia
Blessings

Mija Shija Sayi said...

Binti kipaji hapo nimekukubali. Watanzania tuna kila la kujivunia kwa HAZINA hii(MUBELWA BANDIO). Hebu tujiulizeni hivi ingekuwaje kama Mubebwa asingekuwepo, maneno ya faraja na busara tungeyapata wapi? Sio siri Mzee wa changamoto unaweza kufariji na kumtia mtu nguvu ya kunyanyuka tena hata kama mtu alianguka muanguko wa Ki-haiti.

Ubarikiwe kaka.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

Amen!

Sisulu said...

amen