Wednesday, January 27, 2010

VYOMBO VYETU VYA HABARI NA MAJINA YA VIGOGO NA WATOTO WAO


Hivi karibuni Gazeti la Mwananchi liliandika juu ya habari ya mtoto wa Kigogo mmoja huko Moshi kukamatwa kwa kosa la kulawiti. Mtoto huyo anatuhumiwa kumlawiti mtu mmoja aliyekamatwa ugoni katika Hoteli ya KNCU, akishirikiana na watu wengine.

Katika Gazeti hilo waliwataja watuhumiwa waliofikishwa mahakamani akiwemo mume mshika ugoni na mke wake ambao naamini ni makabwela kwa kosa la kumlawiti mtuhumiwa wa ugoni, lakini jina la mtoto wa kigogo huyo bado lilikuwa halitajwi pamoja na kuwa alifkishwa mahakamani.

Sswali ninalojiuliza ni hili, Je kuna sheria maalum inayowalinda watoto wa vigogo kutajwa katika vyombo vya habari pale wanapotuhumiwa kwa makosa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria?

Mimi naamini sheria hiyo ipo, na inafanya kazi. Kwa nini nisiamini wakati mara nyingi vyombo vya habari vimekuwa vikitumia msamiati wa “Mtoto wa Kigogo fulani” bila kutaja jina huku walioshirikiana naye wakitajwa waziwazi?

Nimekuwa nikishuhudia ubaguzi wa waziwazi katika vyombo vyetu vya habari kwa kuwataja baadhi ya watuhumiwa kwa majina na kuficha majina ya watoto wa hao wanaoitwa vigogo au vigogo wenyewe, hivi kwani Vigogo ni akina nani hasa?
Je wako juu ya sheria? Wanalindwa kwa maslahi ya nani?

Naomba wajuzi wa Sheria watuelimishe juu ya hili.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mimi si mwanasheria na nadhani naruhusiwa kutoa hoja yangu hapa. Ni kwamba hata mimi naomba wanasheria watuelimishe kwani kwa nini wengine watajwe na wengine wafichwe wakati binadamu wote ni sawa.?

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ndio

MARKUS MPANGALA said...

PAINLESS DICTATORSHIP ndiyo hii, kwani hakuna katiba au sheria au sera yoyote inayozuia kutajwa jina la mtoto wa kigogo au kikuni au kifimbo. Vyombo vyetu vya habari ninaendesha mambo kipumbavu.
ana yale magazeti yanayojiita makini wakati mwingine ni UDAKU kama stori hii. sidhani kama kanuni za uandishi wa habari kuna mahali wanazuia kutajwa majina ya watoto wa matapeli hao.

udaku uliowahi kunadikwa kuwa Zitto Kabwe anatembea na barua ya kujiuzulu katika gazeti la Mwananchi mwaka jana na Ramadhan Semtawa ni kukiuka kanuni za faragha kwani ile ilikuwa siyo habari ya kutuandikia ni ujinga mtupu. ile ilikuwa gumzo la marafiki lakini wakaligeuza na kutukengeusha kwamba ni stori.
magazeti makini yanatabia ya kurudia mambo yaleyale kwa mtindo uleule kwahiyo mimi wakati mwingine naona ni UDAKU tena afhali udaku wa magazeti ya udaku.

nakubaliana nawe kuwa tuhoji ni sheria ipi inayowalinda watoto wa vigogo bin vikuni au vifimbo!