Nimejichimbia huku
Ni jambo la kusikitisha kuwa linatokea adimiko katika kipindi kibaya. Kipindi ambacho jamii inahitaji sana kuelimishwa hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
Nimesema ni kipindi kibaya kwa sababu kwa kutumia maandishi yetu katika blog zetu hizi zisizoisha visa na mikasa tumekuwa tukiibua mijadala mbali mbali yenye kuelimisha kufundisha na kuchangamsha na kwa kupitia chagamoto hizo, wengi wamejifunza mambo mbalimbali yahusuyo jamii yetu hii, katika Nyanja ya kisiasa na kijamii kwa ujumla.
Adimiko langu halikuwa rasmi, lakini niliwahi kupita humu na kukiri huo udhaifu wa kuadimika pasipo taarifa. Lakini katika hali ya kushangaza nimeshangazwa na adimiko la baadhi ya wadau wenzangu katika vibaraza vyao kimya kimya na tusijue walipoelekea.
Hongera kwako kaka yangu Mubelwa Bandio kw akuliweka Adimiko lako hadharani na hivyo kuwatoa jakamoyo wadau waliozoea changamoto zako hapo kibarazani kwao.
Pia ningependa kuwapa pongezi wale wadau wanaoendelea kutupasha kwa habari motomoto za hapa na pale na kuifanya tasnia hii ya Blog kutodorora.
Ingawa Mwananchi mimi kaamua kutupa yanayojiri kule Afrika ya Kusini kunakochezwa Kombe la Dunia, na ninadhani alisoma alama za nyakati akajua kuwa, kama ataweka longolongo za Politics hatapata msomaji kwa sababu macho na akili za watu wote karibu dunia nzima yako huko Bondeni kwa Mzee Madiba Mandela wakifuatilia kinyang’anyiro hicho.
Mzee wa Mataranyirato yeye akamua kumuandikia mkewe barua ya wazi huku Kamala akijiuliza huyu Mungu ni nani jamani. Mzee wa Nyasa, inasemekana kajitwisha mshipi na sasa anavua dagaa huko ziwa Nyasa, lakini si haba anatupasha mawili matatu.
Kaka yangu Matondo naye nasikia yupo nchini na kajichimbia huko Arusha, nasikitika kwamba niko huku Milima ya upareni kumuona bibi yangu mwenye jina lake Koero na hivyo kukosa nafasi hii adimu ya kukutana naye na kupata Kahawa pale chini ya mti maeneo ya Sanawari kwenye Hoteli ya Naura.
Dada yangu Subi naye yupo analiendeleza libeneke lake pale Wavuti na kama kawaida yake hakosi kutupasha habari motomoto bila kukosa za kisiasa. Bila kumsahau dada yangu kwa mama mwingine Yasinta Ngonyani, naona na yeye kaanza mwendo wa kunyatanyata katika kublog. Sio kawaida kijiwe chake kudororra, lakini safari hii, mweh! amelala doro.....sijui ndio majukumu au ni kupisha kombe la Dunia!
Kaka yangu Bwaya, nakumiss sana, hivi ziko wapi zile fikra zako pevu zenye kutekenya ubongo? Kwa nini lakini uadimike kiasi hiki jamani? Please, Please I beg you, come back Bro! We miss you so much……………..
Ningependa kuchukua nafasi hii kuwaomba wadau wenzangu kuwa, chonde chonde tusipotee mtandaoni kwani tunahitajika sana na jamii kwa ajili ya kutoa elimu ya uchaguzi. Sisi pia ni sehemu muhimu katika kuleta mabadiliko ya uongozi hapa nchini.

6 comments:
Picha nzuri sana.
Karibu japo ado ado, ni vyema kuona kuwa unatukumbuka wanakijiji wenzio. Utuletee dhawadi nyiiiingi thana vavae.
Mh!
Koero ni kweli nimeadimika kidogo hii yote ni kutokana na majukumu mengi pia kwa sasa hapa shule zimefungwa kwa hiyoo muda mwingi nipo na familia si unajua familia kwanza burudani baadaye. Lakini wala usikonde/msikondo MAISHA NA MAFANIKIO IPO.Ila nawe binafsi nina kumiss kwelikweli.
Mama Mchungaji ahsante sana kwa kutukumbuka.
Hakika umeelewa kwa nini nimeieweka kando siasa. Unajua nini? Hata wabunge wamesema televisheni ya taifa (TBC) isirushe vipindi vya bunge bali irushe kombe la dunia.
Kwa hiyo watu sasa hawajali mambo mengine. Macho na akili zao hukoooo bondeni. Nikaona mimi niende mwendo wao....
Watu si umeona hata bajeti hawajataka kuipa nafasi kwenye majadiliano. Suala la mgombea binafsi watu wameona si ishu. Bungeni nako unaambiwa nusu ya wabunge hawahudhurii, kisa, kombe la dunia.
Mama Mchungaji usihofu..linaisha siku si nyingi, tutarudi kukimbiza spidi kali ili kufidia hizi siku.
Ngoja nikunong'oneze....uthithahau kunletea dhawadi.
Jumapili njema.
Hata mie nimem-miss sana kaka BWAYA....hivi yuko wapi huyu?
Sikujua mwalimu matondo alikuwa arusha. Mi pia nipo likizo na nilikuwa arusha mpaka jana.
Post a Comment