Hatukuafuata kanuni
JE HIVI UNAJUA:
Kwamba tofauti kati ya nchi masikini na nchi tajiri haitokani na umri ambao nchi inayo. Na hilo tunaweza kulitambua kwa kuangalia nchi kama India na Misri; ambazo zina zaidi ya miaka 2000 tangu kuwepo kwake hapa duniani lakini bado ni nchi masikini!
Kwa upande mwingine nchi kama Canada, Australia na New Zealand ambazo miaka 150 iliyopita zilikuwa ni nchi masikini na zisizohesabiwa kama nchi zenye uchumi imara, lakini leo hii ni nchi zenye maendeleo makubwa na tajiri sana.
Tofauti ya nchi tajiri na masikini haitokani na nchi kuwa na maliasili na rasilimali za kutosha.
Japan, ni visiwa vidogo ambavyo karibu asilimia 80 vimezungukwa na milima na haina ardhi ya kutosha kwa kilimo na ufugaji, lakini ni nchi yenye uchumi imara sana.
Ni nchi ambayo inaagiza malighafi kutoka nje na kuzalisha bidhaa mbalimbali na kuziuza karibu ulimwenguni kote.
Mfano mwingine ni nchi kama Switzerland ambayo hailimi zao la Cocoa, lakini ni nchi ambayo inazalisha bidhaa ya chocolate yenye ubora hapa duniani. Ni nchi ambayo inalo eneo dogo kufaa kwa ufugaji lakini wameweza kuwa wazalishaji wazuri wa mazao ya mifugo yenye ubora wa hali ya juu kama vile Jibini. Ni nchi ndogo ambayo ina usalama, sheria nzuri na hali njema ya kazi unaoifanya iwe nchi salama zaidi kuliko nyingine duniani.
Wakuu kutoka nchi zilizoendelea wanaowasiliana na wakuu wenzao wa nchi masikini wanaonesha kuwa hakuna tofauti kiakili.
Tukisema Rangi, Kabila au dini kuwa ndio kipimo cha tofauti ya nchi tajiri na msikini ni kujidanganya bure.
Wale wahamiaji kutoka nchi masikini ambao katika nchi zao walikozaliwa walionekana kuwa wavivu kupindukia ndio wazalishaji wakubwa katika nchi hizo tajiri.
Je tofauti yake ni nini hasa?
Tofauti ni mtazamo wa watu katika nchi hizo masikini, ambapo unachagizwa na elimu na utamaduni usio na tija ambao umekuwepo kwa miaka mingi.
Kwa kuangalia tabia na mienendo ya watu wa nchi zenye maendeleo na tajiri utagundua kwamba asilimia kubwa ya watu hao inafuata kanuni zifuatazo katika maisha yao.
Kanuni hizo ni hizi zifuatazo:
· Maadili
· Uadilifu
· Uwajibikaji
· Kuheshimu sheria na taratibu
· Kuheshimiana na hasa kuheshimu uhuru wa mtu mwingine
· Kupenda kazi
· Kujinyima na kuweka akiba na hatimaye kuwekeza katika biashara.
· Kujituma
· Kujali muda
Ni watu wachache sana katika nchi masikini wanaofuata kanuni hizo katika maisha yao ya kila siku.
Sisi sio masikini kwa sababu eti tuna uhaba wa maliasili/rasilimali au mazingira yaliyotuzunguka ni magumu.
Sisi ni masikini kwa sababu tuna tatizo la mtazamo na namna ya kufikiri.
Kama unaitakia mema nchi yako, basi sambaza huu ujumbe kwa watu wengi nchini kwako ili waujue ukweli huu:
Makala hii nimeitafsiri kutoka katika mtandao.
Chanzo hiki hapa: http://www.mikebonnel.com/
Nakiri kuwa tafsiri ni yangu kama kutakuwa na mapungufu naomba mnivumilie.

4 comments:
kujali muda: hili lingebalidi mambo mengi sana kwa watanzania.
Na hii si katika Nchi tu, hata katika familia. Angalia familia nyingi zenye mafanikio, huwa zimetilia mkazo mambo hayo uliyoyataja hapo juu.
Umenena mama mchungaji. Sadaka yangu nakuletea hapo hapo kilimo kwanza :-(
mh ni ya kufikirisha. ila yawezekana wengine hawahitaji utajiri!!
Post a Comment