Monday, September 20, 2010

WAKATI IDADI YA WASALANDIAJI NA WAMEZEA MATE TONGE IKIONGEZEKA, MASHARTI NAYO YAONGAZEKA PIA.

Kazi ipo.....


Ni jambo ambalo sikulitarajia kuwa kumbe pamoja na kunangwa kuwa sioleki na sitakuwa na ndoa imara lakini soko langu liko juu kiasi hiki!

Kusema kweli nimekuwa na wakati mgumu hasa maana kuna wengine ambao wao wamepitia mlango wa nyuma na kuleta CV zao ili kutaka bahati iwadondokee, lakini hata hivyo hilo sio tatizo, bali wasiwasi wangu ni kuwa mzee Mkundi kaongeza masharti kadhaa ambayo nahisi kuna ambao watadondokea pua.

Masharti yenyewe ni haya yafuatayo:

*Mtarajiwa hatakiwi kuwa na umri wa ubarubaru yaani umri wake uwe umefikia kati ya miaka 40 hadi 45, kwani vijana wa umri wa ubarubaru wanakuwa wasumbufu kwa sababu bado ujana unawazuzua.
*Mtarajiwa anatakiwa awe ni mkristo wa dhehebu la sabato (Hili sharti nadhani litakuwa gumu maana mweh! kwa nyakati hizi dini zina vijimambo vyake)
*Mtarajiwa hatakiwi awe mlevi wa kilevi chochote na asiwe anavuta sigara.
*Mtarajiwa anatakiw awe ni mtu wa nguvu kazi asiwe anachagua kazi.
*mtarajiwa anatakiwa awe mtanashati, mpole kiasi, awe na tabia njema na mwenye upendo wa dhati .

Sifa nyingine za ziada zitapewa kipaumbele…..LOL

Haya mwenye sifa hizo aweke CV zake hadharani, hata wale wenye kupitia nyuma ya pazia karibuni kwenye kinyang’anyiro.

13 comments:

Markus Mpangala said...

UBAGUZIIIII mweeeeeeeeeeeeeeee!!!
HARTI HILI........ naenda kwa WACHINA KUONGEZA MIAKA.....

*Mtarajiwa hatakiwi kuwa na umri wa ubarubaru yaani umri wake uwe umefikia kati ya miaka 40 hadi 45, kwani vijana wa umri wa ubarubaru wanakuwa wasumbufu kwa sababu bado ujana unawazuzua.

Markus Mpangala said...

ha ha ha ha ha ha NIMGUTUKA mweeeeeeeeeeeeeeeeee hoooooooooooooooooooooooooooooooiiiiiiiiiiiiiiiiiii haaaaaaaaaaaaaaaa huyooooooooooooooooooooo nimeshtuka.

samahani kwa mcharuko.
Koero UNATAKA KULIZIBA JUA KWA KUTUMIA BAKULI?

ongeza hata sharti jingine la kuikamata mbingu, maana watu tulishakwepa manyunyu .....
Mzee mkundi nakuomba jaribu kutengeneza picha hii hivi UNAWEZA KUPIGA MLUZI HUKU UNATAFUNA KARANGA????/
Mie ni zaidi ya hizo sifa, nafaa kwa shida na raha, iwe leo au kesho, juzi au jana,...... namsubiri mtani wangu shemeji

Fadhy Mtanga said...

ahsanteeeeeeeeeee.....!!!

ahsante sanaaaaaa.....!!!

kuna kila dalili mzee Mkundi alishaona mie ndo nakufaa ndo maana akaona aweke vigezo ambavyo ana hakika ni mimi peke yangu ninayeweza kukidhi.

Markus imekula kwakooooooo shemeji aka mtani aka mkilogram.

hadi hapo shindano lifungwe rasmi kwani si Markus wala Ramson wanaoweza kunipa hofu tena. nakidhi mimi peke yangu.

koero ushakuwa wangu...

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ipange harusi wakati wa likizo (May - Agosti). Nitapenda kuhudhuria!!!

Ramson said...

Wote mmekosa, na bahati hii imeniangukia mie mwana wa Mzee Kayanda.
Kwanza mwezi wa kumi natimiza miaka 40.
Pili mie ni Msabato kwa baba na mama.
tatu mie sinywi pombe wala sivuti misigara wala bhangi.

Sasa Jee ni nani amekusudiwa kudondokewa na hiyo bahati?
naomba mjaze wenyewe maana Mtanga na Markus na hao wengine walioko nyuma ya pazia wameangukia pua...LOL

Haya Koero naomba utoe maelekezo ya namna ya kufikisha posa maana hapa nilipo ni mbali sana lakini hata kwa email naamini itafika kama sio leo basi kesho

Mlisema hampati mbona kampata, mlisema hampati mbona kampata,
Wahafidhina wameangikia pua haooo....LOL

Markus Mpangala said...

Nini pombe mzee Mkundi bin Japhet na wale binamu zako wa Mamba miamba?

MARKUS ni huyu HAPA
Hanywi pombe wala kuonja tangu azaliwe
Hali nyama
Hali maharage
Hanywi soda,
Hanywi juisi ya kiwandani
Hali mayai,

UNATAKA NINI mzee Mkundi na bintiyo...

MARKUS huyu hapa,
ni bingwa wa kilimo,mahindi,viazi na .......
Ramson naomba uwe na nasubira watafute wazee wenzio wakupe viuno vyao vya kizeeee Lol

Anonymous said...

Mimi nahisi aliyesema atakayemuoa Koero, atapata shida ..
Sasa huyo mzee anapotoa masharti kwa binti yake, anajuaje kama binti anakubaliana na vigezo hivyo?
Hapo ni kuingilia uhuru wa Koero kuamua maisha yake, na kufanya uchaguzi. Hawa wazee wa kizamani...
Ebu angalia, eti sharti kwamba asichague kazi, ina Mzee Mkundi akiamua wiki yote hiyo ni kuzibua choo chake, nyingine kulisha ng'ombe, basi kidume anakuwa jinga tu kukubali, pthuuu nimetema mate.
Hapo mwanaume atakuwa ameolewa na Mzee Mkundi.
Koero, zingatia matakwa yako, mumeo utaishi naye wewe na kwenye nyumba yenu, na sio kwa masharti ya Baba, nina imani una akili ya kujua yupi ni mwema na yupi ni kiraka tu. Misimamo yako imeanza kuyeyuka nini, hasa kwenye masuala ya uvunguni...
Wanawake wamepewa uwezo zaidi, achana na mfumo usioeleweka

Koero Mkundi said...

ha ha ha haaaaaaa!!!
Annony kaniacha hoi kweli.....
Ni kweli ni mawazo ya kizamani mtu kuchaguliwa mume au mke lakini labda nilichosahau kusema tangu mwanzo ni kwamba hayo ni mapendekezo tu..... kila mzazi anayo matarajio yake linapokuja suala la kuolewa au kuchagua mchumba... sio lazima maoni ya wazazi yafuatwe ingawa yanaweza kutumika kama guide line kwa mtoto ili asije akauvaa mkenge (wanaume wa siku hizi ni ma-pretender kweli!!)
Kwa hiyo mie ninavyo vigezo vyangu ambavyo ni vya chumbani....LOL

Ni hayo tu mwayego....

Markus Mpangala said...

NAKUNUKUU KOERO 'Kwa hiyo mie ninavyo vigezo vyangu ambavyo ni vya chumbani'.

NUKUU YA PILI

'wanaume wa siku hizi ni ma-pretender kweli!!)'.

Koero umepotea wapi......????? hapa ndipo lilipolala tatizo la kwanza la wanawake, kwamba wanaume ni wadanganyifu..... walianzaje?? ni kwanini? kwa wanawake je???

SIJALI
Markus mie,
nipe miye,
nimekuja miye
penzi nipatiye,
nifute aibuye,
wanaume wasipitiye,
nipe sininyime,

NIPE SIRI YA CHUMBANI,
nami niwe ndani,
meza kuu ya ubani,
walau nijue haniiii,
nikubusu, mamiiii
nipate amani,
moyo naweka rehani,
mwili wako jamani,
nimeze ewe haniii
nipe miye maanani
nimegee jamanii,
liwe langu penzi,
lidumu nilienzi,

SIMON KITURURU said...

Mmmmmh!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mchagua jembe........

inabidi aje yeyote anayejua kutongoza tu na kufanya kagera style

Msangi said...

Huyu ndio dada yangu bwana...heheheeeee, naogopa kusema kitu mie hapa

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___