Friday, October 22, 2010

KAKA MATONDO, USIONE KIMYA NIKO HUKU!

Jana nimekumbuka sana kublog, ni takribani mwezi na siku kadhaa sijaonekana humu, na hiyo ni kutoakana na kuwa bize katika kuzifukuzia ngawira.

Leo nimekutana na makala ya kaka yangu Matondo akinitafuta nikaoni si vyema nikikaa kimya, unaweza kumsoma kaka Matondo akimlilia dada dada yake Koero kwa kubofya hapa

Nimekuwa bize mno mwayego, na kama mjuavyo kuwa maisha ya siku hizi kila mtu anajichomea kamuhogo kake na familia yake. Kwa hiyo na mie bado niko huku Arusha najichomea kamuhogo kangu.

Nawasalimu wote na nawatakia siku njema.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Alahaula! Ni furaha ilioje kujua kuwa u mzima wa afya yaani we hujui tu ni kiasi gani unapendwa na ulikuwa/una-missiwa. Mwenyezi Mungu na awe nawe kwa kila utendalo huko Arusha. MMh! sasa roho zitatulia PAMOJA DAIMA. NA TUKUMBE SISI SOTE NI NDUGU NA WATPOTO WA BABA MMOJA MMOJA AKIPOTEA KWA MUDA BASI WENGINE HATUNA RAHA KABISA. aHSANTE KWA KUJIBU HARAKA SANA. SIKU NJEMA NAWE.

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Afadhali umesikika na tumefurahi kusikia kwamba hujambo wewe pamoja na familia yako. Jichomeeni kamuhogo kenu salama lakini mkumbuke kwamba wachomaji wachache lakini walaji wengi.

Utarudi lini mtandaoni kwako na kuendelea kublogu kama zamani? Blessings!!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

duh! nyoka katoka pangoni hatimaye....lol!

MARKUS MPANGALA said...

waama, afadhali umekuja.
Si Uliniambiaaaa,
kwamba wajaaaa
Markus nakuongojaaaa,
siku,miezi inapitaaa,
sijakuona mchungaji mamaaa,
Mi napata mashakaa,
usinisahau kabisaaaaaa

PASSION4FASHION.TZ said...

Haleluya! amepatikana akiwa hai kwenye kampeni za kukimbilia mjengoni Dodoma.......lol Koero huagi?mpaka kaka akaamua kutoa tangazo?
Haya tumeshukuru u mzima wa afya tele endelea kuchoma hako kamuhogo walaji tuko wengi hahahaaa!ubarikiwe sana.

Godwin Habib Meghji said...

INAWEZEKANA NI UBUSY KATIKA UCHAKACHUAJI WA KURA, UBUSY UTAPUNGUA BAADA YA OCT 31.

Simon Kitururu said...

Mtoto unakifua kizuri wee!:-(