Friday, March 9, 2012

MIKOBA YA MANUNUZI INAPOKUWA NA VIJIDUDU GEMS





Utafiti uliofanywa na profesa Charles Gerba wa chuo kikuu cha Arizona nchini Marekani umebaini kwamba wengi wetu hususan sie kina mama hatusafishi mikoba yetu tunayotumia kufanyia manunuzi sokoni. Kuna hii mifuko maarufu kwa jina la mifuko ya Rambo au wakati mwingine tunayo mikoba maalum ya Canvas ambayo tunaitumia kufanyia manunuzi. Mikoba hii huwa tunaitumia na kisha kuihifadhi kwa matumizi wakati mwingine.


Je huwa tunaisafisha mikoba hiyo au tunaitumia mara kwa mara bila kuifanyia usafi kwa usalama wetu?


Profesa Gerba ambaye ni mtaalamu wa masuala ya udongo, maji na mazingira, alichunguza na kupima zaidi ya mikoba 100 kwenye miji ya California na Arizona, na katika utafiti huo aligundua kwamba ni asilimia 3 tu ndio wanaosafisha mikoba yao. Katika utafiti huo aligundua mikoba mingi ikiwa na vijidudu hatari vya Coliform asilimia 50 na E. Coli asilimia 8

“Inashangaza kidogo kuona mtu anatumia mikoba hiyo kubebea nyama, mayai, mboga mboga ambazo hata hazijaoshwa vyema na makorokoro mengine ambapo yamesheheni vijidudu vya maradhi lakini haifanyii usafi mikoba hiyo, bali huiweka kwa matumizi wakati mwingine.” Alisema Mtaalamu huyo wa masuala ya udongo, maji na mazingira,

Profesa Gerba alishauri watu wawe wanaosha mifuko yao kwa sabuni na maji ya moto baada ya matumizi.



6 comments:

emuthree said...

Kuna usemi usemao usafi ni tabia,...utakuta mtu anafagia barazani tu, hebu nenda chumbani kwake mvunguni....

Goodman Manyanya Phiri said...

Sawa kabisa!!!! Na kama ukitaka kupata uchafu zaidi, tumia simu ya hadharani (public phone) au azima simu ya mkononi kwa mtu mwingine. Hata kin***si utakula hapo baadaye kama wewe si mzowefu wa kusafisha mikono yako kwa maji na sabuni baada ya kushikashika vitu huko nje duniani!

Anonymous said...

Ni kweli usafi ni tabia. Kuna watu wamezoea uchafu na hata hawaoni tabu, utakuta mtu nyumba yake safi sebuleni na kwa nje barazani sasa ingia jikoni na chooni mh! kama ilikuwa ushirki chakula anachopika mbona unaanza kujisikia umeshiba ghafla shauri ya huo uchafu wa jikoni kinapoandaliwa chakula, na ukiingia chooni mh mbona unatoka bila kukitumia kama umebanwa haja ndogo mbona inahsa yenyewe ukilinganisha na uchafu uliopo kwa kutoka haraka sana. Jamani mie naona usafi kila sehemu ni muhimu sana hasa kwa wakina mama na kina baba pia.

Vimax Asli Canada said...

I visited several web pages however the audio quality
for audio songs existing at this website is truly fabulous

jaya sehat said...

nice blog and article, thanks for sharing

poker said...

PROMO DELIMA
poker online | Agen Domino | Agen Poker|Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | bandar qiu | Judi online terpercaya

Bonus yang kami sediakan :
* TO (Turn over) sebesar 0.3% yang akan di kami bagikan setiap hari senin
* Bonus referal sebesar 10%

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat.
Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: Facebook
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___http://www.delimapoker.com/?ref=19860605