Thursday, February 5, 2009

PAPA HUYU ALIKUWA NI KIBOKO!

Hawa hawakushuhudia vibweka vya Papa Leo wa tano

Papa Leo wa tano. Umeshawahi kumsikia huyu? Basi,alikuwa ni Papa wa aina yake, ambaye alifikia wakati fulani alisema kuwa hakuna Mungu. Alikuwa anapenda anasa usisikie. Kila siku alikuwa akialika marafiki zake kwa ajili ya kula, kunywa na kucheza. Alikuwa akifanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kufanya anasa, kama vile hakuwa na akili nzuri. Alikuwa akiuza vyeti maalumu ambavyo ati vilikuwa vinamfutia mnunuzi dhambi zake na ambavyo vingemwingiza Peponi. Hiyo yote ikiwa ni kumpatia fedha za kuponda mali. Ndugu yetu, jiulize kuhusu hizo sadaka zako unazotoa, ni mungu au ibilisi? Kwenye hizi imani ni lazima mtu awe makini, kwani dini maana yake sio mtu kuwa kipofu. Kama unataka kujua zaidi kuhusu papa huyu, soma kitabu kiitwacho, “The book of Heroic Failures”.

No comments: