Blog hii itakuwa ikiibua mijadala mbalimbali yenye kufurahisha, kuhuzunisha, kuelimisha na ujinga kidogo. Pamoja na yote naamini pia italeta changamoto na migongano ya mawazo, ndio maana nikasema VUKANI.
Monday, February 9, 2009
KUSENGENYA: TABIA ISIYO NA MWISHO MZURI
Mwisho wake ni maumivu
Hebu chukulia umechelewa kufika kazini , unapofika ofisini unasikia sauti za wafanyakazi wenzako wakizungumza kwa ndani, unapofungua mlango na kuingia, ghafla wananyamaza na kukuangalia kwa mshangao! Jiulize walikuwa wanazungumzia nini?
Kwa kuangalia mfano huo kwa haraka utagundua kwamba walikuwa wanazungumzia jambo linalokuhusu au walikuwa wanakusengenya. Kwa mujibu wa watafiti mbalimbali, imethibitishwa kuwa wanawake na wanaume wote wanasengenya, labda kinachowatofautisha ni uwiano kwamba wanawake ndio wasengenyaji wazuri zaidi ya wanaume.
Hebu jaribu kutembelea kwenye saluni za kike, utakuta hakuna kinachozungumzwa huko zaidi ya kusengenya, tena kibaya zaidi ni usengenyaji wa kubomoa na kuharibu umaarufu wa watu wengine. Kama wamemtembelea mwenzao au kuhudhuria mazishi ya msiba unaomhusu mwenzao, shuhudia mazungumzo yatakayotawala wakati wanarudi.
Njia nzima mjadala utakuwa unahusu maisha ya mwenzao, kwamba hana hiki , hana kile, au mazishi hayakuwa mazuri kama ya fulani, pia hata kulinganisha thamani ya jeneza la maiti na umaarufu wa mhusika. Utawasikia wakisema “kuringa kote kule kumbe si lolote wala si chochote, ndani kwake kubaya, hana hata kitu cha thamani ukilinganisha na mavazi yake na umaarufu wake”.
Litazungumzwa hili na lile ilimradi tu kumbomoa mhusika. Hivi karibuni niliamua kufanya kautafiti kadogo pale ilipo biashara yangu kwa kuwauliza baadhi ya wateja wangu na wapita njia wengine. Nilizungumza na baadhi ya wanawake pamoja na wanaume kadhaa kuhusu hili suala la kusengenya. Dada mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sharifa, alithibitisha kuwa ni kweli sisi wanawake tunaongoza kwa kusengenya, lakini alitetea kuwa kuna tofauti ya kusengenya na kumzungumzia mtu au watu kwa mazuri na mafanikio yao.
Sharifa alibainisha kuwa sio vibaya kumzungumzia mtu kutokana na mafanikio yake, kwani hiyo kuwapa fursa ya kujifunza kulingana na mafanikio ya mwenzao, pia hata wanapozungumzia mapungufu ya mtu, hiyo ni kwa ajili ya kujifunza kutokana na mapungufu ya mwenzao. Dada mwingine aitwae Bupe, alisema kuwa hata wanaume nao husengenya, yeye alishawahi kumfuma mvulana ambaye punde tu alitoka kufanya naye mapenzi akiwasimulia wenzake jinsi yeye (Bupe) alivyo awapo kitandani, kuanzia mwili wake hadi namna anavyofanya mapenzi.
Ukweli ni kwamba hakuamini tukio lile kwa sababu mvulana aliyemwamwini na kuamini kumkubali kuwa mpenzi wake baada ya kumtongoza kwa muda mrefu, angeweza kusimulia yale yote aliyoyasikia. Kibaya zaidi hata wale waliokuwa wakisikiliza ule utumbo walionekana kwa nje, kuwa ni watu wenye busara. “Usiwaone wamekaa kwenye makundi wakizungumza ni wasengenyaji wazuri sana, tena usidhani wanajadili jambo la maana, sanasana wanazungumzia wanawake wale waliotembea nao alisisitiza Bupe”.
Kijana mmoja aitwae Dikupila ambaye anamiliki saluni ya kunyoa nywele jirani na ofisi yangu, kwa upande wake aliyewatetea wanaume kuwa siyo wasengenyaji, kwani hayo ni mambo ya wanawake. “Sisi wanaume kusengenya! Haiwezekani, hayo ni mambo ya wanawake, sana sana ukikuta mwanaume anajadili udhaifu wa mpenzi wake hadharani basi ujue huyo jamaa anamatatizo makubwa ya kiakili” alisema Dikupila.
Watu wengi wa jinsia tofauti niliobahatika kuzungumza nao walikuwa wanakiri kusengenya lakini walikuwa wanajaribu kutengeneza fasili ya neno kusengenya kwa namna ya kukidhi haja zao. Kwao kusengenya walisema ni mtu kutafuta namna ya kujifunza kuwa bora kupitia makosa ya wengine. Je tabia hii inaweza kuachwa? Wengi walikiri kwamba siyo rahisi tabia hiyo kuachwa kwani imekuwa ndiyo sehemu ya maisha, kwamba haiwezekani watu kukaa pamoja na kuacha kuzungumza matukio na yanapozungumzwa matukio, ni lazima yatawahusu watu hivyo kujikuta watu wanasengenya.
Na tabia hii imejikita kila mahali kuanzia nyumbani, mitaani, hadi maofisini, mashuleni na vyuoni. Binafsi naamini kwamba tabia inaweza kuachwa kwa watu wakijikita zaidi katika kufanya kazi na kuwa wabunifu, hasa maofisini. Kama ni suala la mazungumzo iwe ni ya kuleta ufanisi na tija katika kazi kwani waajiri hulipa mishahara kutokana na ufanyaji wetu wa kazi na uzalishaji.
Utakuta mtu anafika kazini amechelewa na akifika anaanza kusengenya, atazungumzia hili na lile wakati muda unaenda na muda wa kazi ukiisha anafunga kazi na kuondoka. Ukichunguza utakuta tangu asubuhi hakuna chochote alichofanya zaidi ya umbea. Watu wa aina hii wanakuwa wa kwanza kulalamika mishahara ikichelewa. Yapasa watu kubadilika na kutia shime katika ubunifu.
Majumbani na mitaani vilevile nako hapafai. Kwa mfano utakuta mtu ana saluni yake na ana wateja wengi wanasubiri kuhudumiwa lakini wahusika utawakuta wanatumia muda mwingi kusengenya na hivyo kupoteza muda bure. Wale wateja wenye haraka kwa kawaida huwa wanaondoka na kutafuta mahali pengine. Hivyo ikiwa watu watajirekebisha kwa kufanya kazi kwa bidii na kuacha tabia ya kusengenya naamini nchi hii uchumi wake utakua kwa kiwango kizuri na kila mtu atafaidi matunda ya jasho lake.
Ni vema kama mtu hawezi kusema jambo lolote zuri kuhusu mwenzake akakaa kimya, kwani ni njia bora ya kusitiri heshima yake.
Nasio aliwahi kuimba kwenye wimbo wake wa Dangerous akasema "don't worry about the pretty things you hear them (they) say, don't trust no enemy can trust no friend". Japo lugha zaidi ni patois ambayo grammar yake (kama ipo) ni tofauti na kiingereza, lakini analosema ni kuwa kusimuamini mtu kwa kila anachosema machoni mwako. Ndilo lililomkuta Dada Bupe. Well, kusengenywa hakufai kwa namna yoyote ile, japo wapo wasikiao masengenyo wakabadilika kutokana na kuogopa kuwa wahanga wa yaliyowakuta wenzao. Ndio yale ya ukiona mwenzio ananyolewa. Sasa wanaposengenya mtu mwenye kazi nzuri na pesa nyingi wakati maisha ya watoto wake ni duni kwa kuwa tu anaendekeza ulevi, kama kuna aliyepo pemeni na akasikia hayo na yeye ni kama asengenywaye ujue inaweza kuwa "turning point". Lakini Da Koero, mara zote athari za usengenyaji hutokana na hatua azichukuazo msengenywaji. Akiamua kuendeleza ubishani na magomvi nao anawapa la kusema, akiamua kujifunza kitu na kujijenga kutokana na mapungufu atakayojifunza atakuwa amenufaika. Lakini sasa, ni mpaka ajue anachosengenyewa na nia hasa ya kusengenya ni kumsema mtu na asijue kuwa anasemwa. Kwa hiyo usengenyaji si mzuri kama ulivyosema na unapaswa kuachwa, na badala yake watu wawe na ujasiri wa kuhoji na kueleza hisia zao kwa "wapendwa" wao uso kwa uso maana hilo litaonesha wajali na litajenga zaidi. Amani kwako na kwenu pia
Tatizo ni jinsi jamii iuchukuliavyo usengenyaji mpaka tuna magazeti kibao ambayo kinamna ni ya kisengenyaji na ndiyo yanunuliwayo kwa wingi kwa sababu jamii inahamu yakujua yasiyo ya maana MPAKA kama ni kweli mheshimiwa ni kweli ana chupi moja au LA.:-(
Nachojaribu kusema ni ; katika usengenyaji mengi ni uongo na yasiyo na manufaa.
Udhaifu wa kuvumilia uongo uliopo mpaka UKWELI ujitokeze ndio usababishao tutapetape kujitetea au hata kugombana ili kutaka kuharakishia umati ujue usengenywayo ni ya uongo.
Naamini kama ni mvumilivu na usengenywayo ni ya uongo, toa muda tu UKWELI utajulikana na asengenyaye atajulikana mpaka ni kwanini anataka kudadisi na kuongelea yasiyomuhusu.
Mimi nimezaliwa na mama na baba, na wote ni watanzania. wazazi wangu ni wakulima na ni wafanyakazi waliojiajiri, ninao wadogo zangu, dada zangu na kaka zangu kadhaa. wote tunapendana.
Mnaweza kuwasiliana na mimi kwa kupitia Barua Pepe, anuani yangu ni hii: koeromkundi@gmail.com au koeromkundi@ymail.com
UCHAGUZI 2025: BALOZI NCHIMBI ATOA WITO
-
*Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John
Nchimbi amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya
wat...
UCHAGUZI 2025: BALOZI NCHIMBI ATOA WITO
-
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu
pamoja na...
UCHAGUZI 2025: BALOZI NCHIMBI ATOA WITO
-
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
amesema kuwa msingi wa sera za CCM utabakia kuwa ni maendeleo ya watu
pamoja na...
Wamefyatuka wanafyatuana mbele ya mafyatu!
-
Juzi tilishangaa sana. Mwe! Nani angeamini kuwa mafyatu wanene na wanono
wangefyatukiana na kufyatuana hadharani? Unene kweli taabu japo una raha ya
kul...
A Gift From Fair Trade Books, Red Wing, Minnesota
-
On February 15, 2025, I went to Red Wing, Minnesota, to give a talk at the
Red Wing Public Library. My Talk was on African storytelling. After my
talk, a...
NAPENDA KUWATAKIENI KHERI SANA YA MWAKA MPYA 2024
-
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda sisi wote kwa
kuona Mwaka 2024. Wengi walitamani kuona lakini haikuwa bahati kwao.Binafsi
mim...
-
[image: Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio]
Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio
alt=”” class=”w...
-
[image: Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio]
Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio
alt=”” class=”w...
Darasa 45: Maisha yetu kama zoezi la matofali
-
Darasa linakukumbusha kuwa...… Watu watatu ni mimi na wewe. Watu kumi ni
mimi na wewekwa sababu kuna watu tumesimama nyuma yao. Lakini pia, ni watu
wetu ...
Mwaka mpya na vitu vizuri..
-
via
above 2 imgs via
via
via
via
Heri ya mwaka mpya 2019 wapenzi wa HHmag. Uwe mwaka wa afya ,baraka na
vitu vizuri. Karibuni.
MY FIRST VLOG!!!
-
kUNA BAADHI YA WATU BADO WANASUBIRI NIRUDI HUMU ILA HAMJAMELEWA KUWA
NIMEHAMA NA NIMEFUNGUA A WEBSITE NA KUBLOG HUKO NA NAPATIKANA AT
WWW.NURUTHELITE.COM,K...
Facts The Economist Got Them Wrong on Magufuli
-
*By Dr. Herman Louise Verhofstadt*
* “A BIT like President Donald Trump, Tanzania’s president, John Magufuli,
likes to fire employees on television. In No...
Kiringo Mikononi Mwa Polisi....
-
*Jeshi la POLISI MKOA WA MJINI MAGHRIB linamshikilia Mtumishi wa bodi ya
mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kumlawiti Kijana wa kiume mwenye Umri
wa ...
Nimepata vitabu hapa Iringa
-
JUMAMOSI hii, Iringa ni tulivu sana. Jua likiipunguza baridi ya hapa.
Hali ya hewa ni ya kupendeza sana. Mandhari ya mji huu mkongwe haihitaji
maelez...
I HATE YOU, MOSQUITO
-
[image: Image result for mosquito]
*by eva ndimara *
I don’t like you
I hate you – mosquito!
Year 1990 you killed our grandpa.
You, agent of death...
SHEIN RANGERS YACHAPWA 3 - 1
-
Mchezo wa kirafiki uliochezwa jana dhidi ya SHEIN RANGERS na katabazi fc
uliisha kwa Shein Rangers kupoteza kwa magoli 3-1 kiukweli timu yangu jana
haikuch...
Beautiful things..
-
above 2 imgs via
via
above 2 imgs via
via
That quotation, well said.
Have wonderful day and God bless everything you do. Check out more
decoration ...
Je, Mnajua tofauti ya mapenzi na mahaba?
-
Kwa mujibu wa wajuvi wa lugha, Mapenzi ni hisia za upendo kwa mwenza wako
na mahaba ni vitendo vya kuyathibitisha mapenzi.
Ni kwamba mapenzi yako moyon...
Bado n’nasimama
-
Safari ya maisha… Zawadi ya maisha, In’thamani ambao wengi hawatambui…
Mwelekeo wake wala sijui. Bado n’natembea. Amani duniani hamna… Vita kila
kukicha,...
Kwa heri Asiimwe, Malaika wangu
-
*Ni wakati mgumu sana katika maisha yangu. Si jambo jepesi kufiwa na mtoto.
Nafarijika kwa maneno ya wote walionitumia salaam za rambirambi. Hapa
chini, na...
NI WEWE KAMPENI, MAENEO YA ITUNUNDU PAWAGA JANA
-
Ni Wewe ni kampeni iliyozinduliwa na redio Ebony FM iliyoko Nyanda za juu
kusini, ikiwalenga zaidi wananchi wa vijijini ambao miundo mbinu ya umeme ...
WHATEVER WENT WRONG WITH WINNIE?
-
*He stood by his wife, still captivated, when those around him denounced
her for violence and treachery. Now, even Nelson Mandela himself has come
to see t...
Cheka nuna.
-
Na ukinuna,..
Je moyowo watabasamu?
Na ukicheka,..
Je moyo ununao ni wa kibinadamu?
Cheka nuna na ikibidi lia,...
Na si mwisho wa cheko yalizayo ni utamu?...
TUNAHAMA
-
KULINGANA NA TEKNOLOJIA NA MABADILIKO YA TEKNOHAMA
....lol nimetumia misamiati ee
YES 8020 FASHIONS SASA TUNAHAMA TOKA HAPA NA TUTAKUWA TUNAPATIKANA HUMU
...
bacon topped british turkey
-
*Ingredients*
Ingredients1 x 800g / 1lb 12oz British turkey breast roll joint
4-5 tbsp redcurrant jelly
1 tbsp oil
1 small onion, peel...
Functioning males are highly demanded than ladies
-
In the past and recent present, women were gold in most societies but
nowadays things have changed. Spinsters, single mothers, widow and divorced
women’...
Saying goodbye to the AdSense for Feeds blog
-
Thanks to everyone who has been a loyal reader of this blog over the years.
After some consideration, we recognize that we're just not generating
enough co...
Tanzania between Old and New
-
July 10, 2012
by Göran Hydén, NAI Associate and Distinguished Professor of Political
Science, University of Florida, Gainesville.
There has been good news...
JAMANI NIMERUDI TENA NILIKUWA MASOMONI
-
IMERUDI tena kwenye kibaraza chetu, karibuni sana nilikuwa nigeria nasoma
masters ya Journalism Curriculum Development and Designing nimemaliza
nimerudi T...
Car for hire in Dar-es-Salaam
-
You can hire this car in Dar.
The car with a driver will only cost you 100'000TZS (500SEK), +petrol
+300TZS per mile (1,6km),
for one day in the city of ...
Hyr bil i Dar-es-Salaam
-
Hyr bilen!
Du kan nu hyra vår bil för 100'000TZS (500SEK) per dag, + bensin + 300TZS
per mile (1,6km), inklusive chaufför.
Priset gäller i Dar. För längre...
Stranger
-
Ever seen a stranger infront of your house?
Haha! I just saw this guy talking to the phone, really loud and just funny
the fact that he is outside and I ...
ABOUT ME
-
*PERSONAL INFORMATION *
*Name: Malkiory Matiya*
*Date of birth: 1.2.1967*
*Nationality:Tanzanian*
*Religion: Christian *
*Gender: Male*
*Languages: Swah...
UNA WAZO ZURI?WAAMBIE WENZAKO!
-
Kila siku mimi hupenda kupitia tovuti mbalimbali.Huwa napitia takribani
tovuti mia mbili kila siku.Lakini ninavyozipitia mimi ni kwa kutumia huduma
ya blog...
Jinsi ya Kuweka Video Kwenye Blogger/Blogspot
-
Baada ya huduma ya kublogu ya Blogger kununuliwa na Google, nilidhani kuwa
wangeboresha huduma zao haraka. Naona hawana haraka. Bado zana kama
WordPress zi...
3 comments:
Nasio aliwahi kuimba kwenye wimbo wake wa Dangerous akasema "don't worry about the pretty things you hear them (they) say, don't trust no enemy can trust no friend". Japo lugha zaidi ni patois ambayo grammar yake (kama ipo) ni tofauti na kiingereza, lakini analosema ni kuwa kusimuamini mtu kwa kila anachosema machoni mwako. Ndilo lililomkuta Dada Bupe. Well, kusengenywa hakufai kwa namna yoyote ile, japo wapo wasikiao masengenyo wakabadilika kutokana na kuogopa kuwa wahanga wa yaliyowakuta wenzao. Ndio yale ya ukiona mwenzio ananyolewa. Sasa wanaposengenya mtu mwenye kazi nzuri na pesa nyingi wakati maisha ya watoto wake ni duni kwa kuwa tu anaendekeza ulevi, kama kuna aliyepo pemeni na akasikia hayo na yeye ni kama asengenywaye ujue inaweza kuwa "turning point".
Lakini Da Koero, mara zote athari za usengenyaji hutokana na hatua azichukuazo msengenywaji.
Akiamua kuendeleza ubishani na magomvi nao anawapa la kusema, akiamua kujifunza kitu na kujijenga kutokana na mapungufu atakayojifunza atakuwa amenufaika. Lakini sasa, ni mpaka ajue anachosengenyewa na nia hasa ya kusengenya ni kumsema mtu na asijue kuwa anasemwa.
Kwa hiyo usengenyaji si mzuri kama ulivyosema na unapaswa kuachwa, na badala yake watu wawe na ujasiri wa kuhoji na kueleza hisia zao kwa "wapendwa" wao uso kwa uso maana hilo litaonesha wajali na litajenga zaidi.
Amani kwako na kwenu pia
Tatizo ni jinsi jamii iuchukuliavyo usengenyaji mpaka tuna magazeti kibao ambayo kinamna ni ya kisengenyaji na ndiyo yanunuliwayo kwa wingi kwa sababu jamii inahamu yakujua yasiyo ya maana MPAKA kama ni kweli mheshimiwa ni kweli ana chupi moja au LA.:-(
Nachojaribu kusema ni ; katika usengenyaji mengi ni uongo na yasiyo na manufaa.
Udhaifu wa kuvumilia uongo uliopo mpaka UKWELI ujitokeze ndio usababishao tutapetape kujitetea au hata kugombana ili kutaka kuharakishia umati ujue usengenywayo ni ya uongo.
Naamini kama ni mvumilivu na usengenywayo ni ya uongo, toa muda tu UKWELI utajulikana na asengenyaye atajulikana mpaka ni kwanini anataka kudadisi na kuongelea yasiyomuhusu.
nawaza, nawaza. kaka zangu wamemaliza yote ASANTENI
Post a Comment