Blog hii itakuwa ikiibua mijadala mbalimbali yenye kufurahisha, kuhuzunisha, kuelimisha na ujinga kidogo. Pamoja na yote naamini pia italeta changamoto na migongano ya mawazo, ndio maana nikasema VUKANI.
Wednesday, February 11, 2009
NDOA NYINGI NA TALAKA NYINGI!
Siku hizi hazidumu!
Hivi karibuni nilibahatika kusoma mahojiano ya Mwanamuziki wa kundi la zamani la muziki, maarufu kama Spice Girls la nchini Uingereza Geri Halliwell. Nilisoma mahojiano yake mtandaoni aliyoyafanya na Gazeti la Woman’s Day la nchini humo. Labda niwakumbushe wale wasiolifahamu kundi hili la Spice Girls.Kundi Hili liliwahi kuvuma sana miaka ya 90 nchini uingereza likijumuisha wanamuziki wanne, Victoria, aliyeolewa na Mchezaji maarufu wa soka nchini Uingereza David Beckgham, Emma, Melanie na Geri Halliwell.
Katika Mahojiano hayo, mojawapo ya maswali aliyoulizwa na mwandishi, ni hili la yeye kutoolewa pamoja na kwamba ana mtoto. Majibu yake kwa swali hilo ndio yaliyonisukuma nikae kitako kwenye Kompyuta yangu na kuandika makala hii. Akijibu swali hilo, Geri alisema kwamba hana imani kabisa na maisha ya ndoa, na ndoa kwake sio mojawapo ya agenda zake katika maisha.
Alisema katika kizazi hiki familia nyingi zimeshuhudia kuvunjika kwingi kwa ndoa kama ilivyotokea kwa wazazi wake. “Katika makuzi yangu nimeshuhudia ndoa nyingi zikivunjika mpaka nimefikia kuona kwamba ndoa hazina maana kabisa” alisema Geri. Aliendelea kusema kwamba haoni ndoa hata moja ya mfano ambayo anaweza kuitumia kama Dira yake inayoweza kumshawishi kuolewa, ingawa anapenda sana kuwa na watoto wengi.
Siku hizi hapa nchini vijana wengi wamekuwa wakifunga ndoa kila uchao, lakini hata hivyo Talaka nazo zimekuwa zikiongzeka vile vile. Ndoa zimekuwa nyingi sana kwa sababu watu huoana kiholela. Kuoana kumekuwa rahisi na kusiko kujiuliza mara mbili, ukilinganisha na zamani. Kwa sababu hiyo ndoa zinavunjika sana. Kwa kuangalia ukweli huo utagundua kwamba talaka siyo nyingi sana bali ndoa za hovyo ndiyo nyingi, kwani huanza ndoa na talaka hufuata.
Wanaume na wanawake na hata wavulana na wasichana huoana bila ya kujua sababu ya kuoana kwao. huona kwa sababu wameambiwa kuna kuoana, huoana kwa sababu umri unaenda au kwa sababu watu wameona watu fulani wakiwa na furaha wakidhani ni kwa sababu ya ndoa.
Wazazi nao wanawalazimisha au kuwashinikiza vijana wao kuoa au kuolewa wanataka kuona tu kwamba nao wana wajukuu, wanataka kujua vijana wao wakiwa na wenzi wao ili wajisikie vizuri. Wanaogopa kuambiwa, ‘binti wa fulani hajaolewa mpaka sasa hivi’ au ‘vijana wa fulani wahuni tu hawataki kuoa’. Wazazi nao hawana sababu ya kwa nini vijana wao waoe au kuolewa.
Kuna haja ya wazazi kuwafanya au kuwasaidia vijana wao kujijua vizuri wenyewe, kabla hawajaingia kwenye uhusiano wa dhati wa kindoa. Inabidi kijana ajiuluze kama yu tayari kwa ndoa na je hana jambo ambalo litamzuia au kumfanya ashindwe kutimiza wajibu wake wa ndoa, kwa mfano masomo, kazi na mengine? Je kijana anaamini nini kuhusu ndoa yaani ndoa kwake ni nini? Kama kwake ndoa ni kupata furaha, kukimbia matatizo ya nyumbani, kuzaa, kuwa huru kuamua mambo yake na sababu nyingine kama hizo inabidi ajiulize tena na tena kama sababu hizo ni sababu za msingi.
Wanaoingia kwenye ndoa siku hizi wengi hawajiulizi kama wako tayari kupata watoto. Unakuta mwanamke akizaa wanaanza kuhisi kwamba walikosea kuoana na hapo kutoka nje huanza na hata kutekelezana wakati mwingine. Hata kama wanataka watoto huwa hawajapanga namna ambvyo watawalea na kama wangependa kuwa na watoto wangapi na maswali mengine kama hayo.
Lakini, kunakushindwa kwingi katika kujiuliza ni kwa kiasi gani mtu anawaza kuwakubali wengine na kuyachukua matatizo yao. Ni vema kijana akajiuliza kama anaweza kuvumilia kasoro au udhaifu wa wenzake kama anaweza kukabili mabadiliko ambayo yanaweza kutokea kwenye uhusiano.
Siyo mtu kujijua peke yake lakini hata kumjua mwingine ni tatizo pia. Mtu anaingia kwenye uhusiano wakati hamjui vema anayeoana naye. Anamjua kwa sura na mwili ndiyo lakini zaidi ya hapo hajui kingine chochote kuhusu huyo mwingine, hajui kwamba ni Malaya, hajui kuwa ni mchoyo, hajui ni mkata tamaa, hajui kama ni “mtoto wa mama” hajui chochote kumhusu.
Unakuta watu wamekubaliana kufunga ndoa, lakini mmoja au wote hawajuani mwingine anatokea wapi hasa. Anasena tu “wazazi wake sijui ni wenyeji wa wapi, sijui Tanga vile, sijui Iringa!”
Ukweli ni kwamba bila kumjua mtu vizuri ni hatari kuoana naye. Wakati mwingine wenzetu ni watu wanaozalisha nguvu hasi nyingi duniani, wakorofi wenye kijicho, walipa visasi, wenye zarau, wapenda shari na mengine. Lakini kwa sababu wanatutendea vema katika wakati fulani tunaamini hawana tatizo.
Wasichana wengi wanakubali kuoana na wanaume ati kwa sababu siku hizi hakuna wanaume. Ni nani amesema hakuna wanaume? Msichana ameona kabisa kijana ni mgonvi na pengine ameshawahi hata kumpiga lakini anajiambia “nikimkosa huyu ndiyo basi sitoolewa tena” kisha anaolewa na wanaishi kwa mwaka mmoja tu.
Wanalazimika kuingia kwenye uhusiano ambao wanaona kabisa hautadumu. Hufanya hivyo kwa hofu ya kuwa wapweke. Wanaogopa sana kubaki bila kuolewa kwa sababu eti wamesikia mtaani kwamba wanaume hawapatikani kirahisi. Aibu tupu! Mara nyingi vijana wanaongozwa na kuhemkwa badala ya tafakari katika kuingia kwenye ndoa. Wanapokuwa kwenye uhusiano kuhemkwa kunaisha na wanarudi kwenye hali halisi ambayo wanashindwa kuibeba.
Kuhemkwa huku ndiko wenyewe wanakokuita kupenda. Wanasema kabisa “nimependa sana siwezi kumwacha pamoja na kunipiga na umalaya wake” Ebo! Mtu ni Malaya na kama hiyo haitoshi bado huwa anakupiga halafu unasema huwezi kumwacha? Kama huo si uwendawazimu ni nini?
Mara nyingi nyingi kuhemkwa kunaisha wakiwa tayari na watoto wawili na maisha wakati huo yanakuwa yameharibika. Wengine kuhemkwa kunaishi wakiwa tayari na ukimwi, wengine wakiwa na chongo, na wengine wakiwa na BP na kisukari juu, kwa sababu ya maumivu makubwa ya kihisia.
Kuna watu wazima ninaowajua ambao nao wameshabadili wake na wanaume mara kadhaa. Kila ndoa wanayoingia inabomoka. Kisa ni kufuata mihemko badala ya kufuata hekima. Hawajifunzi ndoa ya kwanza wala ya pili, wanatembea na kosa lilelile, yote hiyo ni kuhemkwa badala ya kujua na kupenda.
Nakubaliana na Geri Halliwell kwamba, kuna talaka nyingi. Lakini kama nilivyosema, nadhani kuna ndoa za kuhemkwa nyingi, na ndizo zenye kusababisha talaka nyingi.
Kwanini watu wanaoa au kuolewa, kwanini wanaoana? Kwanini watu wanatoka nje, kwanini wanatoa talaka, kwanini wanakubali kuoana? Kwanini kuoana? kwanini iwe lazima kuoana? kwanini iwe kama ilivyo? Sijui lakini nasema hivi, kama ndoa ni halali ya mwanadamu basi kuachana ni halali ya mwanadamu LAKINI tukumbuke hata mpanzi alipopanda mbegu zingine zilipandwa mibani na zingine mwambani, lakini zile za kwenye ardhi nzuri zilizaa udongo mzuri. Jendoa zetu zinaongozwa kwa falsafa gani? Mapenzi yetu yanakwenda kwa itikadi gani? Au tunaiga mambo ya kununu maua,zawadi,mabusu hadharani,kukumbatiana hadharani,kuongozana kama kumbikumbi nk.? Kwanini mtu anakuwa malaya? au kwanini anatoka nje? SWALI: nini kinachosababisha kuwa malaya? kinachotumika kwa umalaya ni nini? Na kwanini umalaya au kutoka nje ni tabia za wanandoa? kwanini ndoa hazidumu hata tukupigana makofi ya mawili kwa tofauti ambayo tumekosa falsafa na itikadi. KUMBE tunaiga kila kitu toka ughaibuniDUH! majuzi kuna ndoa ilifungwa na sherehe ikafanywa pale jirani Movenpick nyooooooo! eti bi harusi baada ya fungate kabanduliwa na X wake!!!! ha ha ha ha ha ha niliangua kicheko..... lakini jamaa kasema hakuna noma. SWALI kwanini wanadamu wanafunga ndoa? Muungano wa watu wawili, nini kinachowaunganisha? NAWAZAAAAAAA lakini jibu sipati Basi ngojeni Lucky Dube awakumbushe simulizi zake katika IT IS NOT EASY..... halafu anasema 'the choice that i made, didnt workout!
Mimi nimezaliwa na mama na baba, na wote ni watanzania. wazazi wangu ni wakulima na ni wafanyakazi waliojiajiri, ninao wadogo zangu, dada zangu na kaka zangu kadhaa. wote tunapendana.
Mnaweza kuwasiliana na mimi kwa kupitia Barua Pepe, anuani yangu ni hii: koeromkundi@gmail.com au koeromkundi@ymail.com
DKT TULIA AFUNGUA MKUTANO MKUU WA IPU
-
*Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa
Mabunge Duniani (IPU), Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 6 Aprili, 2025
amefun...
Chukua Mkwanja Wako Mapema Leo
-
HATIMAYE baada ya jana kushuhudia mechi kibao zikipigwa na matokeo mengine
yakiwa yakustaajibisha, leo hii ni zamu tena ya wababe wengine kibao
uwanja...
Wamefyatuka wanafyatuana mbele ya mafyatu!
-
Juzi tilishangaa sana. Mwe! Nani angeamini kuwa mafyatu wanene na wanono
wangefyatukiana na kufyatuana hadharani? Unene kweli taabu japo una raha ya
kul...
A Gift From Fair Trade Books, Red Wing, Minnesota
-
On February 15, 2025, I went to Red Wing, Minnesota, to give a talk at the
Red Wing Public Library. My Talk was on African storytelling. After my
talk, a...
NAPENDA KUWATAKIENI KHERI SANA YA MWAKA MPYA 2024
-
Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutulinda sisi wote kwa
kuona Mwaka 2024. Wengi walitamani kuona lakini haikuwa bahati kwao.Binafsi
mim...
-
[image: Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio]
Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio
alt=”” class=”w...
-
[image: Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio]
Tumore prostatico: la prognosi in base a stadio, grado e rischio
alt=”” class=”w...
Darasa 45: Maisha yetu kama zoezi la matofali
-
Darasa linakukumbusha kuwa...… Watu watatu ni mimi na wewe. Watu kumi ni
mimi na wewekwa sababu kuna watu tumesimama nyuma yao. Lakini pia, ni watu
wetu ...
Mwaka mpya na vitu vizuri..
-
via
above 2 imgs via
via
via
via
Heri ya mwaka mpya 2019 wapenzi wa HHmag. Uwe mwaka wa afya ,baraka na
vitu vizuri. Karibuni.
MY FIRST VLOG!!!
-
kUNA BAADHI YA WATU BADO WANASUBIRI NIRUDI HUMU ILA HAMJAMELEWA KUWA
NIMEHAMA NA NIMEFUNGUA A WEBSITE NA KUBLOG HUKO NA NAPATIKANA AT
WWW.NURUTHELITE.COM,K...
Facts The Economist Got Them Wrong on Magufuli
-
*By Dr. Herman Louise Verhofstadt*
* “A BIT like President Donald Trump, Tanzania’s president, John Magufuli,
likes to fire employees on television. In No...
Kiringo Mikononi Mwa Polisi....
-
*Jeshi la POLISI MKOA WA MJINI MAGHRIB linamshikilia Mtumishi wa bodi ya
mapato Tanzania (TRA) kwa tuhuma za kumlawiti Kijana wa kiume mwenye Umri
wa ...
Nimepata vitabu hapa Iringa
-
JUMAMOSI hii, Iringa ni tulivu sana. Jua likiipunguza baridi ya hapa.
Hali ya hewa ni ya kupendeza sana. Mandhari ya mji huu mkongwe haihitaji
maelez...
I HATE YOU, MOSQUITO
-
[image: Image result for mosquito]
*by eva ndimara *
I don’t like you
I hate you – mosquito!
Year 1990 you killed our grandpa.
You, agent of death...
SHEIN RANGERS YACHAPWA 3 - 1
-
Mchezo wa kirafiki uliochezwa jana dhidi ya SHEIN RANGERS na katabazi fc
uliisha kwa Shein Rangers kupoteza kwa magoli 3-1 kiukweli timu yangu jana
haikuch...
Beautiful things..
-
above 2 imgs via
via
above 2 imgs via
via
That quotation, well said.
Have wonderful day and God bless everything you do. Check out more
decoration ...
Je, Mnajua tofauti ya mapenzi na mahaba?
-
Kwa mujibu wa wajuvi wa lugha, Mapenzi ni hisia za upendo kwa mwenza wako
na mahaba ni vitendo vya kuyathibitisha mapenzi.
Ni kwamba mapenzi yako moyon...
Bado n’nasimama
-
Safari ya maisha… Zawadi ya maisha, In’thamani ambao wengi hawatambui…
Mwelekeo wake wala sijui. Bado n’natembea. Amani duniani hamna… Vita kila
kukicha,...
Kwa heri Asiimwe, Malaika wangu
-
*Ni wakati mgumu sana katika maisha yangu. Si jambo jepesi kufiwa na mtoto.
Nafarijika kwa maneno ya wote walionitumia salaam za rambirambi. Hapa
chini, na...
NI WEWE KAMPENI, MAENEO YA ITUNUNDU PAWAGA JANA
-
Ni Wewe ni kampeni iliyozinduliwa na redio Ebony FM iliyoko Nyanda za juu
kusini, ikiwalenga zaidi wananchi wa vijijini ambao miundo mbinu ya umeme ...
WHATEVER WENT WRONG WITH WINNIE?
-
*He stood by his wife, still captivated, when those around him denounced
her for violence and treachery. Now, even Nelson Mandela himself has come
to see t...
Cheka nuna.
-
Na ukinuna,..
Je moyowo watabasamu?
Na ukicheka,..
Je moyo ununao ni wa kibinadamu?
Cheka nuna na ikibidi lia,...
Na si mwisho wa cheko yalizayo ni utamu?...
TUNAHAMA
-
KULINGANA NA TEKNOLOJIA NA MABADILIKO YA TEKNOHAMA
....lol nimetumia misamiati ee
YES 8020 FASHIONS SASA TUNAHAMA TOKA HAPA NA TUTAKUWA TUNAPATIKANA HUMU
...
bacon topped british turkey
-
*Ingredients*
Ingredients1 x 800g / 1lb 12oz British turkey breast roll joint
4-5 tbsp redcurrant jelly
1 tbsp oil
1 small onion, peel...
Functioning males are highly demanded than ladies
-
In the past and recent present, women were gold in most societies but
nowadays things have changed. Spinsters, single mothers, widow and divorced
women’...
Saying goodbye to the AdSense for Feeds blog
-
Thanks to everyone who has been a loyal reader of this blog over the years.
After some consideration, we recognize that we're just not generating
enough co...
Tanzania between Old and New
-
July 10, 2012
by Göran Hydén, NAI Associate and Distinguished Professor of Political
Science, University of Florida, Gainesville.
There has been good news...
JAMANI NIMERUDI TENA NILIKUWA MASOMONI
-
IMERUDI tena kwenye kibaraza chetu, karibuni sana nilikuwa nigeria nasoma
masters ya Journalism Curriculum Development and Designing nimemaliza
nimerudi T...
Car for hire in Dar-es-Salaam
-
You can hire this car in Dar.
The car with a driver will only cost you 100'000TZS (500SEK), +petrol
+300TZS per mile (1,6km),
for one day in the city of ...
Hyr bil i Dar-es-Salaam
-
Hyr bilen!
Du kan nu hyra vår bil för 100'000TZS (500SEK) per dag, + bensin + 300TZS
per mile (1,6km), inklusive chaufför.
Priset gäller i Dar. För längre...
Stranger
-
Ever seen a stranger infront of your house?
Haha! I just saw this guy talking to the phone, really loud and just funny
the fact that he is outside and I ...
ABOUT ME
-
*PERSONAL INFORMATION *
*Name: Malkiory Matiya*
*Date of birth: 1.2.1967*
*Nationality:Tanzanian*
*Religion: Christian *
*Gender: Male*
*Languages: Swah...
UNA WAZO ZURI?WAAMBIE WENZAKO!
-
Kila siku mimi hupenda kupitia tovuti mbalimbali.Huwa napitia takribani
tovuti mia mbili kila siku.Lakini ninavyozipitia mimi ni kwa kutumia huduma
ya blog...
Jinsi ya Kuweka Video Kwenye Blogger/Blogspot
-
Baada ya huduma ya kublogu ya Blogger kununuliwa na Google, nilidhani kuwa
wangeboresha huduma zao haraka. Naona hawana haraka. Bado zana kama
WordPress zi...
2 comments:
Kwanini watu wanaoa au kuolewa, kwanini wanaoana? Kwanini watu wanatoka nje, kwanini wanatoa talaka, kwanini wanakubali kuoana? Kwanini kuoana? kwanini iwe lazima kuoana? kwanini iwe kama ilivyo?
Sijui lakini nasema hivi, kama ndoa ni halali ya mwanadamu basi kuachana ni halali ya mwanadamu LAKINI tukumbuke hata mpanzi alipopanda mbegu zingine zilipandwa mibani na zingine mwambani, lakini zile za kwenye ardhi nzuri zilizaa udongo mzuri.
Jendoa zetu zinaongozwa kwa falsafa gani? Mapenzi yetu yanakwenda kwa itikadi gani? Au tunaiga mambo ya kununu maua,zawadi,mabusu hadharani,kukumbatiana hadharani,kuongozana kama kumbikumbi nk.?
Kwanini mtu anakuwa malaya? au kwanini anatoka nje?
SWALI: nini kinachosababisha kuwa malaya? kinachotumika kwa umalaya ni nini? Na kwanini umalaya au kutoka nje ni tabia za wanandoa? kwanini ndoa hazidumu hata tukupigana makofi ya mawili kwa tofauti ambayo tumekosa falsafa na itikadi. KUMBE tunaiga kila kitu toka ughaibuniDUH! majuzi kuna ndoa ilifungwa na sherehe ikafanywa pale jirani Movenpick nyooooooo! eti bi harusi baada ya fungate kabanduliwa na X wake!!!! ha ha ha ha ha ha niliangua kicheko..... lakini jamaa kasema hakuna noma.
SWALI kwanini wanadamu wanafunga ndoa? Muungano wa watu wawili, nini kinachowaunganisha?
NAWAZAAAAAAA lakini jibu sipati
Basi ngojeni Lucky Dube awakumbushe simulizi zake katika IT IS NOT EASY..... halafu anasema 'the choice that i made, didnt workout!
mpangala umenena hili swala pia nitete ni kwa nini tunaoana hata hatujua na wala hatuko tayari kujua.
Post a Comment