Monday, March 2, 2009

ALITAKA KUATHIRI SELF-ESTEEM YANGU

Ilibidi nikajichimbie Ngorongoro ili kupumzisha akili

Mtafaruku ulionitokea kwa kutofautiana na mama yangu uliniacha na majeraha mengi kiasi cha kuathiri self-esteem yangu
Kwa mujibu wa tafsiri niliyoipata katika makala ya kaka Bwaya aliyoipa kichwa cha habari kisemacho
Self-Esteem: Ni muhimu kwa mwanao

Bwaya aliliezea neno Self-Esteem kuwa ni ni jumla ya imani ama hisia tunazokuwanazo kuhusu nafsi zetu, ama kule kujielewa kibinafsi. Namna tunavyojielewa, huathiri kwa kiasi kikubwa dhamira ama mitizamo tuliyonayo ama tabia zetu na hivyo huathiri namna tunavyoweza kukabiliana na hisia mbalimbali.Aliendelea kusema Self-Esteem (fikra-chanya) pia huweza kufafanuliwa kama muunganiko wa uwezo binafsi pamoja na zile hisia za kujisikia kupendwa anazokuwa nazo mtu. Kwa hiyo, mtoto anayefurahia mafanikio yake lakini hajisikii kupendwa huweza kuishia kushindwa kujiamini (low self-esteemed). Vivyo hivyo, mtoto anayejisikia kupendwa lakini bado ana mashaka na uwezo wake katika kufanya mambo fulani fulani , naye hali kadhalika huishia kuwa kama yule wa kwanza. Hatojiamini.

Hali hiyo iliyoelezewa na kaka Bwaya ndiyo iliyonikumba baada ya ule mtafaruku, kwani mama alianza kuhoji uwezo wangu wa kuendesha biashara niliyoianzisha na pia alijaribu kunishusha sana kielimu kuwa kama nitaendelea kukataa kuendelea na masomo na kutaka kujikita kwenye biashara basi sitafika mbali nitashindwa vibaya, kwa kuwa nina elimu ndogo.

Nadhani kila mmoja wetu anafahamu kuwa kauli za wazazi zina nguvu sana, kwani tumejengewa kuamini kuwa analolisema mzazi ndilo sahihi hasa kama linahusu mustakabali wetu. Mpaka leo sijui ujasiri wa kupingana na mama niliutoa wapi, maana hata dada zangu walinishangaa sana kubishana na mama kiasi kile. Hata hivyo walimlaumu mama kuwa, eti ni yeye amenidekeza kwa sababu ni mtoto wa mwisho kwa watoto wake wa kike nikiwa nimepishana sana na dada zangu kiumri.

Kitendo cha mama kunikatisha tamaa juu ya biashara zangu kilinifanya nijenge fikra HASI na kuanza kuhisi kuwa labda alikuwa sahihi, kuwa sitaweza kusimama kibiashara kama nilivyokuwa nikiamini, na kuona kuwa sitafanikiwa kufikia malengo yangu.
Nilijikuta nikiwa njia panda, nisijue ni nini cha kufanya. Na ndipo nilipopatwa na msongo wa mawazo.

Iibidi nianze kupata ushauri nasaha ili nirejee katika hali yangu ya kawaida, kwani nilishapoteza mwelekeo na kujikuta nikiwa sijiamini kabisa kiasi cha kutaka kukaa tu bila kufanya chochote, kwamba bora nipoteze vyote yaani biashara na shule.

Baada ya kupata ushauri nasaha na kurudi katika hali yangu ya kawaida ikabidi nisafiri kidogo kwenda Arusha kwa mjomba angu kupumzisha akili na kujitafuta upya.
Nashukuru sasa nimepona na naamini malengo yangu yatatimia baada ya mama kunikubalia niendelee na biashara zangu.

Ukweli ni kwamba matatizo wanayoyapata vijana wengi wa umri wa utineja ni kuwa na kiwango kidogo cha fikra chanya (Low Self esteem) na inachangiwa sana na aina ya malezi tunayoyapata kutoka ama kwa wazazi wetu au walezi, na wakati mwingine hata waalimu.

Kwa kawaida mtu mwenye kiwango kidogo cha fikra chanya anakuwa karibu sana na matatizo ya kisaikolojia, hebu chunguza vijana wanaotumia madawa ya kulevya, pombe kupita kiasi, waliojiingiza kwenye vitendo vya kiuhalifu, umalaya, wanaopata mimba za utotoni na wale wanaoshindwa kuendelea na masomo kwa sababu ya kutokuwa na uwezo darasani, wote hawa kuna uwezekano mkubwa wakawa wanakabiliwa na tatizo la kuwa na fikra hasi zilizopandikizwa na wazazi au watu walioko karibu nao.

Watu wenye fikra Chanya (Self esteem) wanakuwa na mchango mkubwa katika jamii iliyowazunguka, wanakuwa ni watu wanaojiamini na wepesi kuthubutu katika biashara hata kama inahatarisha mitaji yao.

Kwa hiyo kufanikiwa kwetu katika kufikia malengo yetu inategemea zaidi aina ya malezi tunayoyapata kutoka kwa wazazi na walezi wetu.

7 comments:

Jimy said...

Are you serious?? Sikutegemea kama hiyo ishu itafikia kiwango hicho.
Good kwamba mambo shwari sasa!

Yasinta Ngonyani said...

Mhh Nashukuru kama umepumzika na hali imekuwa safi. Naona mjomba amekupa matunzo mazuri pia labda ushauri. Ni kweli kila jamii ina malezi yake.

Kissima said...

Koero pole sana kwa hali iliyokukuta.

Kwa upande mwingine,uamuzi wako wa awali wa kuacha chuo na kujikita kwenye biashara ulikuwa ni uamuzi mzito ambao nadhani ulichukua tafakari ndefu.

Kwa maana hiyo pingamizi lolote lile lisingeweza kuathiri maamuzi yako wala kukuathiri kisaikolojia.
Kwa hali iliyokukuta inanipa picha ya kwamba haukuwa na msimamo thabiti kuhusu uamuzi wako wa kuacha chuo na kujikita kwenye biashara,pengine labda mbali na maamuzi yako ulipata ushawishi kutoka ktk chanzo fulani, sijui.

Mawazo ya mtu yameweza kuuathiri uamuzi wako huo, hebu fikiri biashara yako ikijakwenda kombo(kwa mfano) will you be able to accept the situation in an easy way?

Kwa uamuzi wako dada yangu hautakiwi ku regret,kuwa tayari kupokea changamoto mbalimbali lakini usiwe mrahisi wa kubadilisha mawazo na kujuta. Hii itakusaidia sana ktk mafanikio ya mradi wako.Umeshaweka hayo malengo,simama nayo,zingatia mradi wako.Cha msingi sana usirudi nyuma otherwise ukubali kwamba maamuzi yako hayakuwa sahihi. Kila la kheri dada yangu.

SIMON KITURURU said...

Dada Koero, Poa uko bomba sasa.

Dada koero kuanzia Einstein mpaka Bill Gates hawakufikia wasifiwako moja kwa moja.Namaanisha chuo.

Kumbuka ni kwa mapenzi Mama alishauri na Kumbuka ni kwa Mapenzi ya Koero kwa Koero , Koero anafuata moyo wake.

Na uhakika siku yoyote ukitaka kurudi chuo utaweza ya chuo. Na ya chuo Tanzania wanaweza wengi ingawa wakimaliza chuo wanahitaji kuajiriwa ilikuendelea nayasiyo ya chuo.

Katika darasa langu chuo kimoja nilisoma na Wanigeria , Wahindi na Wapakistani pamoja na.....dunia... . ilikuwa Sweden.

Nikagundua mpaka aina ya watu na makabila yao.

Wa IBo kutoka nigeria na wengi wahindi walikuwa wanasoma mpaka PHD ili wajiajiri. Wanigeria kutoka Benin State hasa wanawake ndio ilikuwa wengi wanaweza kuuza mpaka kikojoleo.

MIMI mpare, anyway, mama Mjita kwa hiyo tusijenerelaizi.

NAACHA!


Kabla sijamalizia kuacha,...

...kuna rafiki zangu watatu kutoka Pakistani wameajiriwa na Mhindi waliyekuwa wanamsaidia darasani sasa hivi navyoongea.

Kuna Wa Ibo , mimi nawaita wayahudi wa Afrika, mpaka sasa wafanyacho na elimu, natamani Tanzania tungekuwa tunasoma na kuingia mtaani kufanya matusi kama wafanyavyo.

Wewe ni mfanyaji na sio mpiga taralila na unajua hilo.

FANYA!

Fuata Moyo wako na ni kweli njia yoyote itakuwa na milima na mabonde.

Usiache elimu lakini kwa U jumla mambo yakichanganyia.

Elimu ina jicho lake pia katika kuona NANIHII.

AU?

Koero Mkundi said...

Kaka Simon Mkodo Kitururu,
Ahsante kwa ushauri wako mzuri.
Ukweli ni kwamba sio kwamba nitaacha kupiga kitabu as per say.
No no no no.......
Natarajia nikitulia nitajiunga na masomo ya long distance lerning abroad au nitajiunga na chuo kikuu huria hapa nchini ambapo nitasoma nikiwa relaxed, rather than kurerejea kwenye zile hectic situation za pale mlimani.
bado nipo nipo sana, nitasoma lakini sio ile ya kukamia kwa sana bali as a funny.

Tuko pamoja kaka.

Fred Katawa said...

Koero kwa yaliyokukuta hebu jaribu kujifikirisha nukuu zifuatazo.
"Some people think that a teacher(mzazi)transplants his own thoughts into his pupil's(mtoto) mind.Well,only bad teachers are like that.Good teachers are not gardeners,they are midwives;they don'ttransplant their own thoughts,they help bring to the birth the thoughts their pupils have conceived"By Aristotle.zaidi ya miaka 2400 iliyopita.
"There are two things to aim at in life:first to get what you want,and,after that,to enjoy it.Only the wisest of mankind achieve the second"
"Mtumwa(mtoto)na Bwana(mzazi)wote ni watumwa,kwa kuwa hakuna bwana bila mtumwa na hakuna mtumwa bila bwana.Bwana anakuwa mtumwa kwa kuwa anataka kuuendeleza utumwa,kwa maana hiyo anakuwa mtumwa wa kuuendeleza utumwa kwa sababu tu ya kutaka ubwana.Hawa wote wanahitaji ukombozi kwa kuwa wote ni watumwa"
Mzazi na mtoto hayo ni maneno yangu hayapo kwenye nukuu.

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___