Wednesday, March 25, 2009

WENZETU WAMEWASHITUKIA SISI TUNAWAKARIBISHA

Wawekezaji wanaouza midoli
Soko la wahamiaji haramu wa kichina wanaoingia nchini Marekani linawaingizia mawakala wa biashara hii kiasi cha dola za Kimaekani bilioni 35 kwa mwaka.

Kwa mujibu wa chapisho la Crime and illegal immigration lililotolewa hivi karibuni nchini Marekani imebainika kwamba mawakala hawa wa Kichina huingiza wahamiaji haramu wa Kichina kati ya 20,000 hadi 100,000 kwa mwaka, na kila mhamiaji anawajibika kuwalipa mawakala hawa haramu kati ya dola za Kimarekani 15,000 hadi 50,000 kama gharama ya kusafirishwa na kuingizwa nchini Marekani!

Wahamiaji hawa haramu hutakiwa kulipa malipo ya awali ambayo huweza kuwa robo au nusu ya malipo yote na kiasi kingine humaliziwa baada ya kufanikiwa kuingia nchini humo.
Chapisho hilo limelitaja jimbo la California kwamba ndilo lenye wahamiaji haramu wengi ukilinganisha na majimbo mengine.

Majimbo yanayofuatia ni Texas, New York, Florida na Illinois, Takwimu za hivi karbuni zinaonesha kwamba zaidi ya robo ya wahamiaji haramu wanaoishi nchini Marekani ni Wachina, ambapo inasemekana kuna wahamiaji haramu wapatao 1,321,000 wanaoishi nchini humo.

Jimbo la California lilitumia kiasi cha dola milioni 521 mwaka 1995 kuwaweka wahamiaji haramu gerezani, ambapo kiasi hicho kingeweza kujenga gereza lenye uwezo wa kuhifadhi wafungwa 2,300, kulipia gharama za askari wa doria wapatao 2,600, ambao wangeweza kufanya doria katika viunga vya California.

Baadhi ya wahamiaji haramu hujihusisha na vitendo vya uvunjaji wa sheria na hawa ndio wanaoigharimu serikali ya marekani. Ukweli ni kwamba waajiri wengi nchini Marekani wamenufaika sana na wahamiaji hawa haramu kwani huwafanyisha kazi kama vibarua kwa ujira mdogo sana ukilinganisha na ujira ambao wangemlipa raia wa Marekani.

Hivi sasa mawakala hawa wamegeukia nchi za Kiafrika ambazo zimefungua milango kwa wawekezaji, Tanzania ikiwamo. Mbinu wanazotumia ni kuwaleta kupitia makampuni ya ujenzi na wawekezaji wadogo wadogo, Yaani hata muuza duka pale Karakoo ni Mchina.

Siku hizi Wachina hawa wanamiliki biashara ndogo ndogo na magereji ya mitaani ambayo yamesambaa hadi mikoani. Wachina hawa wamepanga hadi uswahilini na tunaombana nao chumvi kila siku, na wote hawa hawakutumia njia sahihi kuingia hapa nchini, bidhaa zao ni feki na hata uwepo wao hapa nchini ni feki pia.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nakubaliana nawe, Kwani nilipokuwa songea karibu kila duku lilikuwa si la mtanzania ni kweli tumeingiliwa. inabidi sasa tufanye kitu ni haraka.

Mzee wa Changamoto said...

Ntarejea kwa hili. Asante kwa makala na takwimu mwanana.

Digna said...

Habari za hapa.

Nimepita hapa kibarazani kwako kujitambulisha kuwa nimefungua kijibaraza changu kitakachokuwa kikijihusisha zaidi na masuala ya vijana.
Nimekuwa nimsomaji wa blog yako kwa muda mrefu, na sasa nimeamua na mimi nijitose uwanjani ili kuongeza mchango katika kuielimisha jamii.
Niko ntayari kuelimishwa na kukosolewa pale nitakapoonekana natoka nje ya mstari.
Natarajia ushirikiano wako.

Digna

Mzee wa Changamoto said...

Hii ndio nchi yetu PENDWA. Nchi ambayo hakuna anayeona anawajibika kuwajibu wananchi maswali. Nchi ambayo serikali kuwa kichwa cha mtu ni jambo la kawaida na maamuzi kutofikia utekelezaji ni utekelezaji pia. Kuona bila kusema hasa siku zisizo na chaguzi ni sehemu ya siasa zetu na kumjali mwananchi ni kama mwiko kwetu.
Hakuna wa kujali taratibu za kumlinda mwananchi anayesota. Hawa wanakuja (na bado waje) lakini waje kwa taratibu na wasije kuharibu maisha ya wananchi wetu maana twajua hata huko kwao wamekimbia hali ngumu. Sasa sisi kuwapokea ni jambo la muhimu lakini kama tu wamekuja kufanya tusichoweza ama kuanzisha tuwezacho lakini kwa ubora zaidi. Ila sasa hawa ni kama wamekuja kuua soko la kina mama nanihii pale nanihii.
Inauma na kukera saaana
Lazima mtu aamke na kusema jambo ili "walevi wa sifa" kule bungeni walivalie njuga.
Blessings

Ramadhani Msangi said...

Wachina mnawalaumu bure tu. Tanzania ingewekeza kwenye azimio la arusha kikamilifu hata yenyewe hivi sasa ingekuwa na bidhaa nyingi na watu wengi pia kiasi kwamba ingekuwa inalazimika kujisambaza duniani kama wanavyofanya wachina.

Hivi ni nani alishawahi kujiuliza kuwa sababu ya hawa jamaa kufanya hivi hasa ni nini? au tunalaumu tu matendo yao bila kujua the reason behind? labda tuanzie hapo

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___