Monday, May 11, 2009

ANA KILA SABABU YA KUJIVUNIA!

Nyumbani alikozaliwa Mama Namsifu Kiangi

Anaitwa Namsifu Kiangi, alizaliwa mwaka 1941 huko katika milima ya upareni, iliyoko wilaya ya Same Mkoani Kilimanyaro. Ni mtoto wa 5 kuzaliwa kati ya watoto 7 wa mzee Kiangi. Alizaliwa katika kijiji ambacho kinapakana na msitu wa Shengena
Huu ni msitu maarufu ambao ulikuwa ukitumiwa na wazee wa kipare enzi hizo katika kufanya matambiko, hiyo ilikuwa ni kabla ya ujio wa hizi dini za Kimagharibi.

Dini ya kwanza kufika katika eneo hilo ilikuwa ni dini ya Kikristo ya dhehebu la Wasabato. Dhehebu hilo ndilo kubwa lenye wafuasi wengi katika eneo hilo la milima ya upareni kuliko dhehebu lolote lile,
Baada ya ujio wa dini hiyo wazee wengi wa kipare waliachana na mila na desturi zao na kuwa waumini wa dini hizi za kimagharaibi hususan Usabato.

Alizaliwa na kukulia katika dini hiyo ya kisabato, na lipofikisha umri wa kwenda shule wazaziwake walimpeleka shule, alifaulu vizuri darasa la nne na kuendelea na masomo katika shule ya Kimisionari ya Parane, ambapo aliendelea na masomo yake mpaka Middle School.

Alipomaliza middle school hapo mnamo mwaka 1964, aliajiriwa serikalini katika mojawapo ya wizara za serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Aliolewa mwaka 1965, na mzee Japhet Kisarika Mkundi ambaye naye alikuwa ni mtumishi katika taasisi za kigeni.
Mtoto wao wa kwanza wa kiume walimpata mwaka 1967, wa pili wa kike alizaliwa 1970, wa tatu wa kiume alizaliwa mwaka 1973 wa nne wa kike alizaliwa mwaka 1975, wa tano wa kike ambaye anaitwa Koero Japhet Mkundi alizaliwa mwaka 1985 na wa mwisho wa kiume anayeitwa Jarome alizaliwa mwaka 1988.

Akiwa ni Msabato mwenye kufuata maadili aliwalea wanae kwa umri na kimo katika maadili ya Kisabato, na kuna wakati alilazimika kuwalea wanae akiwa peke yake kwa muda wa takribani miaka 8 baada ya mumewe kwenda ughaibuni kikazi na masomo.

Kwa kushirikiana na mumewe wameweza kuwasomesha watoto wao wote na sasa wanajitegemea, baadhi wakiwa wameajiriwa na wengine wakiwa wamejiajiri.
Pia wapo ambao tayari wana familia zao na wameweza kuwaletea Mama Mkundi na Baba Mkundi wajukuu kadhaa

Mama huyu anayo kila sababu ya kujivunia, kwani kwa kushirikiana na mumewe wameweza kujenga familia yenye upendo na amani.

Jana Ilikuwa ni siku ya Mama Duniani (Mothers Day) sisi watoto wa mama Namsifu Japhet Mkundi Kiangi, tulimuandalia mama huyu kijisherehe kidogo cha kumpongeza kutokana na malezi yake kwetu. Niliporejeaa kutoka Morogoro majira ya jioni, niliungana na wenzangu katiaka sherehe hiyo fupi ya kumpongza mama yetu.
Sikuwahi kuandika makala hii jana kutokana na muda kuwa mwingi lakini hata hivyo sijachelewa.

Nawatakia Mama Namsifu na Baba Mkundi maisha marefu.
Ningekuwa na utaalamu kama wa Kaka Mubelwa Bandio ningemuwekea ule wimbo wa Tancut Almas ya Iringa usemao Sina cha kukupa mama.
Lakini naamini kaka Mubelwa ataniwekea wimbo huu wiki ijayo katika ile safu yake ya zilipendwa……..

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Koero nakuomba unifikishie salam zangu kwa mama Namsifu.Nami nasema HONGERA AKINA MAMA WOTE DUNIANI

Anonymous said...

that place looks like in my country too.. we have so many banana tree!!! :D

Mzee wa Changamoto said...

Najua kuwa wajua jinsi tunavyojua kuhusu Mama. Nilisema ambayo sikusemewa na sasa wasema kuwa Mama amekuwa Mama wa kinaMama na sote twajivunia.
Sina hakika kama salamu za-expire lakini naomba hizi kwa mama zimfikie. Sio tu twamtakia maisha mema na ya faraja, bali kwa namna alivyowaandaa kina nyie ambao kwa uamuzi wa kishirika mmetusaidia kina sie, basi naomba umshukuru kwa yote.
Ni malezi ya Mama na Baba ambayo twayaona sasa yakitufaa.
HESHIMA NA UPENDO KWAKO MAMA

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___