Saturday, May 2, 2009

SHIRANGA LA UGONJWA WA MALARIA: BORA TUFE KULIKO KUATHIRI MAZINGIRA!

Hawa ndio waathirika
Nimerejea jijini Dar Es Salaam jana, nikitokea Arusha, nilikokwenda kufanya shughuli maalum ya kifamilia.

Kilichonipeleka sikuweza hata kukifanya kwani tangu nilipofika Arusha nilipatwa na Malaria kali iliyopelekea hadi kulazwa hospitalini na kutundikiwa drip kadhaa za kwinini.

Namshuru Mungu nilipata nafuu na hatimaye kupona kabisa. Nadhani kuugua kwangu kulikuwa na kusudi maalum, kwani niliugua katika wiki ambayo kulikuwa na maadhimisho ya siku ya ugonjwa wa malaria na kama kawaida wanasiasa na wataalamu wetu walitoa matamko mbali mbali ili kuonesha kuwa ni kwa kiasi gani serikali yetu inachukua hatua madhubuti katika kupunguza vifo vinavyotokana na ugonjwa huu ambao unapoteza maisha ya watu wengi hapa nchini kuliko hata huu ugonjwa wa ukimwi unaopigiwa mbiu kila siku.

Ukweli ni kwamba nina mashaka sana na juhudi za serikali katika kutokomeza ugonjwa huu wa malaria kufanikiwa.

Kwa nini nasema nina mashaka na juhudi za serikali?

Ni kwa sababu tangu kuzaliwa kwangu mpaka leo hii nimeshuhudia mabadiliko kadhaa ya dawa za kutibu maleria zikiidhinishwa lakini hazikufanikiwa katika kutibu ugonjwa huo zaidi ya kuwasababishia watumiaji madhara na hata vifo.
Pamoja na juhudi hizo zinazochukuliwani na serikali nadhani sasa ni wakati muafaka wa serikali yetu kuangalia upya uwezekano wa kurudisha matumizi ya dawa ya kuulia wadudu ya
Dichloro-Diphenyl-Trichloroethane maarufu kama DDT, ili isaidie kuuwa mazalia ya mbu na kuwatokomeza kabisa kwani tutakuwa tunahangaika kutibu malaria na kila dawa huku mbu wakiendelea kuzaliana bila kuthibitiwa.

Naona huu ni wakati muafaka wa serikali yetu kuachana na kelele za hawa watu wanaojiita wana mazingira wanaotegemea misaada ya kifedha kutoka kwa wafadhili ambao wanafanya hivyo makusudi ili kuvilinda viwanda vyao vya madawa na ajira kwa wanachi wao.

Siku moja nilikuwa nikiangalia Luninga, mara nikamsikia mtaalamu mmoja wa mazingira, akizungumzia madhara ya DDT kwenye mazingira yetu kwamba kuna baadhi ya wadudu na mimea itatoweka, ujinga gani huu!
Yaani ni bora tufe kuliko mazingira na viumbe fulani kutoweka hapa duniani?

Kingine wanachodai wataalamu wetu hao, eti dawa hiyo ya DDT inasababisha Kansa na kuzaliwa watoto wenye mtindio wa ubongo.
Hivi watoto wote wanaozaliwa wakiwa na mtindio wa ubongo na wale wagonjwa wote wanaolazwa pale taasisi ya ugonjwa wa Kansa pale Ocean Road ni kutokana na DDT?

Mbona hawazungumzii huo mlundikano wa madawa feki hapa nchini ambayo huenda ndio yana madhara kuliko hata hiyo DDT.
Juzi hapa mama Margareth Ndomondo Singoda Mkurugenzi wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) ametutangazia kupiga marufuku dawa za malaria aina ya Metakelfine, eti ni feki!
Miaka yote hiyo watu wamekuwa akitumia dawa hii katika kujitibu malaria sasa leo ghafla zinatangazwa kuwa ni feki.
Je ni watu wangapi watakuwa wameathirika na dawa hiyo?

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na waziri wa Afya Profesa David Mwakyusa ambazo hata hivyo zinatofautiana na takwimu zilizotolewa na na Daktari bingwa wa Malaria Muhimbili Profesa Zul Premji, katika mchakato wa kuelekea katika maadhimisho hayo ya siku ya malaria, alibanisha kuwa, takwimu rasmi kutoka katika vituo vya afya idadi ya watu wapatao 20,000 hupoteza maisha kila mwaka hapa nchini kutokana na ugojwa huu wa malaria, na wengi wao wakiwa ni watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na mama wajawazito.
Hata hivyo alikiri kuwa asilimia 60 ya vifo vinavyotokea majumbani kabla ya wagonjwa kufikishwa katika vituo vya afya ni kutokana na ugonjwa huo wa malaria.
Kwa muktadha huo basi, idadi halisi ya wagonjwa wanaofariki kutokana na ugonjwa wa malaria hapa nchini ni zaidi ya watu 80,000 kila mwaka.

Takwimu hizo zinatofautiana kwa kiasi kikubwa na takwimu zilizotolewa na Profesa premji aliyedai kuwa zaidi ya watu milioni moja hufa kila mwaka hapa nchini kutokana na ugonjwa huu wa malaria.
Hata hivyo kwangu mimi tofauti ya kitakwimu sio mada, bali ninalotaka kulizungumzia hapa ni juu ya serikali kurejesha matumizi ya DDT, hili naomba liwe ni mjadala wa kitaifa ili kunusuru roho za watu, jamani watu wanakufa sio mchezo!

Mbona Zanzibar wanatumia? Wao wamewezaje, na kwa nini isiwe huku kwetu Bara?
Hapa tunahitaji ufafanuzi kutoka serikalini, watueleze sababu ya kusita kuidhinisha matumizi ya DDT.

Historia inaonesha kwamba DDT iligunduliwa na mkemia mmoja wa Ki-Swiss aitwae Paul Muller hapo mnamo mwaka 1934, ambapo ilitumika kwa mara ya kwanza nchini humo mwaka 1939 kuuwa vijidudu vilivyokuwa vikishambulia viazi mbatata na kupata mafanikio makubwa.

Mnamo mwaka 1943 dawa hii ya DDT iliingia sokoni rasmi ikianzia katika nchi za Ulaya, ikitumiaka katika kuuwa wadudu watambaao na warukao wanaosababisha maradhi mbali mbali na kupata mafanikio makubwa.

Dawa hii ilitumika pia wakati wa vita vya pili vya dunia katika maeneo ya tropiki yaliyoathirika na maradhi mbali mbali yaletwayo na mbu na wadudu wengine ambayo yaliwasumbua na kuwatia hofu askari walikuwa vitani zaidi ya makombora na risasi.

DDT ilionekana kama muarobani wakati huo na iliheshimika sana kiasi cha kupelekea mgunduzi wake kutunukiwa nishani ya Nobel hapo mnamo mwaka 1948 kutokana na ugunduzi wake huo.

Zipo nchi ambazo zilizofanikiwa sana katika kupambana na ugonjwa huu wa malaria wakati huo miongoni mwa nchi iliyopigiwa mfano ni nchi ya Sri Lanka.
Mwanzoni mwa miaka ya 1950, zaidi ya watu milioni 2 walikuwa wakiripotiwa kuugua ugonjwa huo wa malaria kila mwaka nchini humo. Baada ya nchi hiyo kutumia dawa ya DDT kuteketeza mazalia ya mbu na wadudu wengine hapo mnamo mwaka 1954, idadi ya wagonjwa walioripotiwa katika vituo vituo vya afya ilipungua na hatimaye kwisha kabisa

Hata hivyo inaonekana mafanikio hayo hayakuwafurahisha matajiri na wamiliki wa viwanda vya madawa na kwa hila huku wakitumia fedha nyingi waliwashawishi wanamazingira ili kuipiga vita dawa hii ya DDT, wakilenga zaidi nchi za dunia ya tatu ambazo hazijajitambua na zinazotegemea misaada kutoka nchi wahisani.

Hawa watu ni wajanja sana, hawa ndio walioanzisha shirika la afya duniani WHO, shirika ambalo wanalifadhili kwa mapesa yao wanayochuma kwa kuuza madawa yao, kwa kuwa shirika hilo linatekeleza maelekezo kutoka kwa mabwana hao wakubwa wakatangaza kuwa ni marufuku dawa hiyo kutumika.
Ikumbukwe kwamba hawa wenzetu walifanikiwa kuwatokomeza mbu katika nchi zao kwanza na ndipo matumizi ya DDT yakaharamishwa.

Huku wakitumia njia ya kutoa misaada ya madawa na vyandaru, kwa staili ya kupiga kofi shavu la kulia na kisha busu shavu la kushoto.
Wanajua misaada yao haitawafikia waathirika wote na kwa upande mwingine wataendelea kuuza madawa yao kwa wingi na kujiingizia fedha lukuki, wajinga ndio waliwao!

Lakini ili ujue kuwa shirika hilo lina ubaguzi, ili kuzilinda baadhi ya nchi zao, wakaweka kipengele kuwa itatoa kibali kwa nchi ambayo itakuwa imeathiriwa sana na ugonjwa wa malaria na maradhi mengine yatokanayo na vijidudu viambukizi kutumia DDT, na itakuwa ni kwa muda maalum. Ebo ina maana mpaka watu wafe kwa wingi na ndipo idhini ya kutumika kwa dawa hiyo itolewe?
Huu ni uwenda wazimu, huyu WHO ni nani hasa? Kwani ndio wizara ya afya ya dunia?

Ukisoma takwimu zao, utashangaa, eti wanadai kwa mwaka watu wapatao 20,000 hupoteza maisha kwa maradhi ambayo yana viashiria vya madawa ya kunyunyizia wadudu. Kwangu mimi hiki ni kichekesho, Afrika peke yake inapoteza watu milioni 5 kwa mwaka kutokana na ugonjwa wa malaria, watu 20,000, ni kitu gani.
Tena kwa mujibu wa takwimu zao wamesema maradhi yenye viashiria, sio yaliyotokana na madawa ya kunyunyizioa wadudu, huu ni upuuzi mtupu.

Serikali ya Sri Lanka ni miongoni mwa nchi zilizotekeleza amri hiyo, lakini mara baada ya matumizi ya DDT kusitishwa nchini humo, Malaria ilirudi kwa kasi na kwa muda wa miaka mitatu ya mwanzo zaidi ya wagonjwa milioni moja waliripotiwa kwa mwaka.

Hata hivyo Serikali ya Nchi hiyo ikaamua kurejesha matumizi ya dawa hiyo ya DDT mnamo mwaka 1968 na kupuuza kelele za hawa wanafiki wanaojiita wanamazingira.

Nchi hiyo imekiri kuwa kwa kiasi kikubwa imepunguza maradhi kama malaria, homa ya malale, kichocho, upofu, matende, taifodi maradhi mengine yatokanayo na bakeria.

Sri Lanka imeangalia madhara yatokanayo na mbu na wadudu wengine, na huo uharibifu wa mazingira na athari nyingine za kiafya zinazotajwa kusababishwa na DDT, wakaona, hata hayo madhara ya kiafya yanayosemwa sio makubwa kwa kiwango kinachosemwa bali kimekuzwa tu na wataalamu hao, kwao muhimu ni maisha ya watu.

Mtaalmu mmoja wa Afya nchini humo aliwahi kuuliza ‘Iwapo mtu unakabiliwa na uchaguzi wa kukubali kuwa kipofu kabla ya kutimiza umri wa miaka 30 kutokana na vijidudu waambukizao maradhi hayo ya upofu au uwezekano mdogo sana wa kupata Maradhi ya Kansa kutokana na matumizi ya DDT kama utafanikiwa kuishi zaidi ya miaka 50 au 60, utachagua kipi?’

Haihitaji mtu kutumia akili ya wataalamu wa kutengeneza Roketi kupata jibu.

9 comments:

Subi said...

Koero, pole sana kwa kuugua Malaria. Ninafahamu machungu ya ugonjwa huo hasa baada ya mimi kutundikwa kwinini mwaka 2002.
Kuhusu kipengele cha matumiz ya DDT, naomba nibandike hapa, majibu yangu niliyoandika kwenye kundi pepe la muXalumni ambalo mimi ni mwanachama wake, nitaiweka kama nilivyoiandika kule na nilishawahi kuitetea DDT mwaka jana:

---------- Forwarded message ----------
From: Subi>
Date: Sun, Apr 19, 2009 at 12:00 PM
Subject: Re: [MUCHS Alumni] ITN
To: "Dr.George M"
Cc: MUCHS Alumni muxalumni@googlegroups.com

Thanks for sharing the study and findings.
I think we still have a war to fight in this. At the moment Malaria seem to be in the winning side. A multi approach is required in eradicating this disease. I wonder why there is no much talk about DDT anymore. Please do not bombard me with it's ill health effects - what's more ill than a death of a child due to Malaria every 1 minute that passes us by? and oh, about the environment concerns - please, give me a break, how much have the third world cared for the environment? and what does the Global Warming report project towards Sub Saharan Countries? - Expect the worst. What good does the environment do if all it does is propagate the breed of more mosquito and other disease vectors? I already know about that, am not ready for a lecture now.

I still defend and advocate for the wise use of DDT in eradicating Malaria. We have used it before at our home in Moshi and for the first 22yrs of my life I never suffered any illness due to Malaria until one stupid day after just a 1 month's field work in Mlali, Morogoro. My kidneys are just perfect, my relatives as well and none had ever been diagnosed with Cancer due to the DDT we carefully used to kill mosquitos. Why did we stop using it? Well, where can we buy it? It's no more in the shops and "Duka la Ushirika" is no more. Politics! Politics! Politics! Too much politics will keep on dividing and killing us even on things that we needed no any tiny bit of it in. Why aren't Italians suffering from the ill effects of DDT? This notion of just agreeing and accepting everything sometimes tickles me off badly big time. Why would they say, "no don't use DDT, it's bad"....after they themselves used it? Puhleez! Alright, say they are right, okay, what difference does it make except changing the mode of death? It's still a death anyway, isn't it?

While others are pushing and making Nuclear Bombs, we on the other end are can not agree to make DDT for safe local use, and we proudly boast that we have distinguished scientists? Yeah, distinguished scientists my foot! Yaani we are debating about making and using DDT carefully as if we are careless? Boy, does anybody need proof what we are. Basically by agreeing with them to not use DDT, we have accepted that we can't be careful. Please give a me a good reason to dispute the benefits of using DDT (and please do not repeat what I said I already know - there is no point of doing that).
What a pity!
I think I am talking to myself too much here.
Have a good week!
.end.
Subi

Mzee wa Changamoto said...
This comment has been removed by the author.
Mzee wa Changamoto said...

Nianze kwa kusema POLE SANA DADANGU. Mimi nilipoona kimya nikajua uko VACATION Arusha kumbe ulikuwa umekwenda "kufunuliwa" mengine mengi kuhusu hili. Asante! Sasa unaona faida ya kuangalia mambo katika mtazamo chanya? Hujarejea hapa na kuanza kulilia pole za kuugua, wala kueleza ulivyotapika ama kujisikia vibaya, bali umeangalia tatizo kwa mtazamo chanya zaidi na kuangalia namna ya kuzuia kutokea tena.
Kuhusu mada hii naamini umeongea na kuweka bayana takwimu na mtazamo wako. Pia Da Subi ameeleza kiutaalamu na kuweka bayana mtazamo wake. Wangu unafanana na wenu. Da Subi amesema "Politics! Politics! Politics! Too much politics will keep on dividing and killing us even on things that we needed no any tiny bit of it in." Ninaamini / na wala sitashangazwa kuona kuwa hata waliosaini mikataba ya kusitisha madawa hayo hawajui kwanini wamefanya hivyo. Si ndio kawaida yao kusaini tu kufuata upepo? YAANI KUNA WACHACHE WASIOFUNGAMANA NA UPANDE WOWOTE TANZANIA YA SASA. Hizi takwimu wanazotoa za watu 20,000 kufa kwa Malaria kwa mwaka sijui ni za mkoa mmoja kama wa Kagera ama la? Sitaki kuamini hata kwa sekunde moja kuwa Tanzania inapoteza watu 20,000 tu kwa mwaka kutokana na Malaria. Hii idadi ni ndogo kuliko hata ya watoto wanaokufa na ugonjwa huu nchini kwa mwaka. Takwimu zaonesha kuwa karibu asilimia 2 ya vifo vya watoto nchini vyatokana na Malaria, sasa serikali ikisema watoto wanaopoteza maisha yao kwa mwaka nchini Tanzania ni wangapi, kisha tukajumuisha na watu wazima tunaweza kuona namba itakavyokuwa kubwa. Lakini nina hakika TAKWIMU ZA SERIKALI SI SAHIHI NA ZIMEJAZWA "MAFANIKIO YA KISISASA" ili kuonesha mafanikio ya vita dhidi ya Malaria. Na hili nina hakika nalo na hata wakisema kuweka REHANI maisha najua nitashinda tuu maana nina hakika takwimu zao ni ndogo mnooo. Lakini narejea tena kuwa kama alivyosema Da Subi (na mimi narekebisha kidogo kuleta maana zaidi) kuwa POLI-TRIX, POLI-TRIX, POLITRIX. Kinachoangalia hapa ni nini wataweza kusema mwakani (wakati wa kampeni) kuonesha takwimu za mafanikio yao. Na kibaya zaidi, HAKUNA ANAYEHOJI USAHIHI WA TAKWIMU HIZO kwa sababu wanaoitwa waandishi wa habari nyumbani na ambao ndio wanaokwenda "kupokea" takwimu hizi ni "ma-ripota" tuuuu. Hawaulizi maswali kupata ufafanuzi zaidi na hawaleti wachambuzi kuangalia uwezekano wa usahihi wa taarifa za wanasiasa wetu. Wao kila wakati ni "akiongea na waandishi wa habari..." "katika taarifa kwa vyombo vya habari.....", "akizungumza na kituo hiki ofisini kwake.....", na kadhalika. Hakuna awezaye kuhoji ni vipi wameweza kupata takwimu ikiwa hata takwimu za wagonjwa wa siku tatu zilizopita unaweza kuzikosa kwenye baadhi ya vituo vya afya nchini Tanzania. Niliwahi kuhoji uwezo na nia ya waandishi wetu hapa (http://changamotoyetu.blogspot.com/2009/02/dah-waandishi-wetu-jamani.html) na bado naamini WAANDISHI WENGI HAWATEKELEZI MAJUKUMU YAO bali nao ni kama WANASIASA WEENGI ambao wanasaini mikataba kuwafurahisha ma-GLOBAL SHERRIF wanaowaeleza kitu cha kufanya hata kama hakina manufaa kwa wananchi waliowachagua.
Kama alivyosema Dada Subi, SIASA ( namaanisha utashi wa kisiasa)HAINA NAFASI KWENYE UNDANI WA UTEKELEZAJI WA MAISHA YA WATU KATIKA MAMBO KAMA VITA DHIDI YA MALARIA. Lakini bahati mbaya sasa nchini kwetu kila mtu anaangalia kitakachomrejesha kwenye "mlo" katika uchaguzi wa mwakani. Hii ni pamoja na kuwadanganya wananchi na kuwaamulia yasiyo na tija kwao.
Naacha. Tukutane "Next Ijayo"

mumyhery said...

Pole sana mdogo wangu yaani malaria huwa nashindwa hata kupata maneno ya kuelezea jinsi nnavyo iogopa

Bennet said...

Pole sana kwa kuugua malaria na tumshukuru mungu umepona.
Nchi kama Afrika ya Kusini wao wanatumia DDT ila matumizi yao ni tofauti na hayana athari katika mazingira kwa sababu wao wanapiga dawa ndani ya nyumba na hivyo kuzuia mbu kutua kwenye kuta zao.
Kitu kikubwa kwenye mapambano dhidi ya malaria ni kinga kwa maana ya kujikinga kung'atwa na mbu kwa kutumia vyandarua vyenye dawa, kuharibu mazalia ya mbu na wewe mwenyewe kuongeza kinga ya malaria mwilini kwa kutunia dawa za asili kama aloe vera

Yasinta Ngonyani said...

Koero mdogo wangu pole sana kwa kuugua hilo gonjwa ambalo linaua watu wengi. Namshukuru mungu u salama sasa

Hii mada yako inabidi ipelekwe mbele kwani ni kali mno.

Mwanasosholojia said...

Jamani Koero dadangu, pole sana!shukrani kuwa uko fine!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

dawa za maralia na magonjwa mengine ni za kiasili na misosi zaidi.

hapo kali nilikuwa na maralia sugu. sikupona kwa kemikali za wazungu. wakati naishi moshi nilitibiwa na mitishamba ya wamasai. niliporudi bukoba nilitibiwa na enkaka, nyarubale na nyingine. hapa dar kana mama mmoja kijichi anatibu kwa dawa ya kihaya. guarantee ni mwaka mzima regardless unaishi kwenye mbo au la.

vinginevyo tumia aloevera orijino. kunywa na uchungu wake, hamna mchezo. ukila matunda kama tikiti maji, tafuna mbegu zake, nakwambia itaondoka yenyewe na unajenga kinga.

punguzeni vyakula vya kizungu, kula vya kibongo kulinda afya. maralia kwangu sio ishu yaani, hainizuii kuingia kwa ofisi wala kuniiingilia maishani

poker said...

PROMO DELIMA
poker online terpercaya | poker online | Agen Domino | Agen Poker | Kumpulan Poker | bandar poker | Judi Poker | Judi online terpercaya | bandar qiu | situs judi online

Ayo segera daftarkan diri anda dan bergabunglah bersama kami !!
Delimapoker.com Situs Agen Poker Online Terpercaya di Indonesia akan melayani Anda dengan profesional, memproses depo/wd dgn cepat. Come join and be a winer with us !!

Untuk info selanjutnya silakan chat ke :
Livechat_____: delimapoker
BBM__________: 7B960959
Facebook_____: delimapoker
Phone number_: +85595678845
pendaftaran___