Friday, July 17, 2009

KOERO SAFARINI DAR!!!!

Wasomaji na wanablog wenzangu, leo saa nne asubuhi hii naondoka hapa Arusha nikielekea Dar Es Salaam, kwa ajili ya kuwaona wazazi wangu na mambo mengine madogo madogo.

Nitakuwepo Dar Es Salaam kwa muda wa siku tano, kwani Jumatano narudi arusha kuendelea na majukumu yangu yaliyonihamishia Arusha.

Kama mnavyojua kuwa safari ni hatua na hivi vyombo tunavyosafiri navyo vinatengenezwa kwa mikono ya wanaadamu, namuomba mungu anifikishe salama.
Naomba mniombee safari njema na nitakapofika nitawajuza kupitia humu katika blog yenu ya VUKANI.
Nawapenda wote……………..

10 comments:

Anonymous said...

Safiri salama!
Wasalimie wazazi utapofika.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hakikisha ukifika umtafute mzee wa lundu nyasa plz, 4 u neva know!

Godwin Habib Meghji said...

Safari njema

mumyhery said...

Safari njema Bwana akutangulie

Fadhy Mtanga said...

Niandikapo maoni hapa naamini kwa uweza wa Mwenyezi Mungu umefika salama. Hivyo pole sana kwa uchovu wa safari. Karibu sana Dar es Salaam.

Koero Mkundi said...

Wasomaji na wanablog wapendwa ninavyoandika hapa ndio nimefika yaani hata sijaongea na mama na baba yangu, hii inaonesga ni kiasi gani ninawapenda.
Muhimu ni kutaka kuwajulisha kuwa kutokana na maombi yenu nimefika salama salimini,

Nawashukuru sana kwa kuniombea safari njema, na sasa ngoja niongee na hawa wazee ili niwajuze yaliyojiri huko njiani na ndipo kesho nitakapowajuza kijimkasa kidogo nilichokumbana nacho njiani........msihofu ni vijimambo tuuuu

PASSION4FASHION.TZ said...

Koero mpenzi nimefurahi kusikia umefika salama kabisa,na bado tutaendelea sara na maombi ili hiyo j'5 pia urudi salama.

Yasinta Ngonyani said...

Koero nami nadhani sijachelewa nafurahi umesafiri salama na upo katika hali nzuri salimia sana baba na mama.

Mzee wa Changamoto said...

Koero.
Ninajaribu kupiga picha ya Baba na Mama walivyofurahi kujiunga nawe. Najua unajua kuwa tunajua kuwa wanakupenda na nina imani kuwa unaamini kuwa twaamini u-dada bora.
Basi tunazidi kukuombea uwe unavyotakiwa kuwa kwani ndio peee na la muhimu tuhitajilo kwa ajili yetu sote.
Salaam kwa Baba, Mama na Ka'Mdogo J na wote hapo nyumbani.
Blessings