Friday, October 2, 2009

JE VITABU HIVI VINAPATIKANA WAPI?

Wasomaji wapendwa na wanablog wenzangu, baba yangu Mzee Mkundi anaomba msaada wa kutaka kujua vinapopatikana vitabu vya DARUBINI, yaani vile vitabu vilivyokuwa vimeandikwa UJINGA WA MUAFRIKA, anakumbuka baadhi ya hadithi zinazopatikana humo kama vile:

KAUTIPE NA UTUMBO WA KUKU

UREMBO WA NDONYA

KAWAMBWA NA KAPU LA KARANGA

CHAI YA DC

Pia anatafuta vitabu vya KISWAHILI vya darasa la nne, la tano na la sita, vya miaka ya 1980 anakumbuka hadithi zinazopatikana humo kama vile:

BROWN ASHIKA TAMA,

KAPULYA MDADISI

KIBANGA AMPIGA MKOLONI

MWEKA NADHIRI NA SHETANI

NUNDA MLA WATU

CHILUNDA APAMBANA NA CHUI

Mwenya kujua vinapopatikana vitabu hivi anijuze, baba anataka kuweka maktaba yake vizuri kwa ajili ya wajukuu zake………

13 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hivyo vya miaka ya 1980 ni ngumu kuvupata niliulizia book shop Peramiho nsikupata ila kwa bahati nzuru miaka ile ya -90 tulinunua kwa hiyo hapa kwetu tuna maktaba ndogo ya watoto wetu pia wajukuu:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hivi ni sawa na kuutafuta mzizi wa jiwe. hata mimi nikivipata nitamtukuza Mungu

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Naamini ukienda pale Maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam ile sehemu ya East Africana (kama haijabadilishwa jina - na utahitaji rukhsa maalum kuingia huko) utaweza kuvipata. Mara ya mwisho nilipokwenda pale nilikiona kitabu cha darasa la pili/tatu? cha zamani kilichokuwa na hadithi zinazozungumzia "Manenge tumbo niache Nimwachie Mandawa".

Nitaangalia pia katika maktaba yetu hapa Chuo Kikuu cha Florida na si ajabu nikavipata baadhi yake. Nikipata kimojawapo basi nitascan au kurudufisha na kumtumia Mzee Mkundi. Nimekumbuka mbali!

John Mwaipopo said...

You made my day! Mzee Mkundi lazima atakuwa anakumbuka mbali.

dk Nzunzulima East Africana haijabarizwa jina lingine isipokuwa imebatizwa upumbavu. hivyo vitabu viko sehemu ya pamhlets lakini ukienda sehemu hiyo utakayoyaona usimsimulie mtu. ni kama dampo vile. vitabu havijapangwa kwa namaba kama inavyoonyesha kwenye class mark. hata ukiomba masaada mfanyakazi wa maktaba anakuonyesha kwa mbali ' nenda katafute paleeee'. nao hawawezi tena. tofauti na sehemu zingine mfanyakazi anakupeleka mpaka kwenye shelve na anakuchomolea kitabu husika.

Koero hebu jaribu taasisi ya elimu kule mwenge. wanaweza kuwa navyo ama kukueleza wapi pa kuvipata, pengine hata publishers, pengine hata watunzi. si haba watunzi/waandishi wa vitabu hivyo wanaweza kuwa na nakala.

Kingine jajifunz hapa ni ari ya kununua na kutunza vitabu katika maktaba za nyumbani (tuzianzishe). ukiwa na kauwezo kidogo nunua kitabu hata kama hukisomi, chaweza pata msomaji hapo baadaye.

Albert Kissima said...

Mzee Mkundi ni mfano mzuri wa kuigwa,binafsi ananihamasisha katika usomaji wa vitabu na kuiboresha home Library kwa kadiri iwezekanavyo.

Shukrani pia kwako dada Koero.

Markus Mpangala. said...

nadhani inabidi jitihada zenye manufaa.... naungana kaka Mwaipopo kujaribu hawa wachapishaji. maana mwenyewe nimetafuta kitabu cha WAAFRIKA NDIVYO TULIVYO cha Dk Malima Bundala hadi nimekata tamaaa.

Sophie B. said...

Dada Koero asante kwa swali hili maana litatusaidia wengi, tafadhali ukipata hivi vitabu tunaomba tufahamishe pa kuvitaka maana hata mimi na baadhi ya watu naowafahamu tumevitafuta bila mafanikio.Kazi nzuri!

Bennet said...

Kama nakumbuka vizuri kuna mheshimiwa mmoja aliagiza vitabu vyote vya zamani (shule ya msingi) vichomwe moto baada ya wizara kutoa mtaala mpya

Koero Mkundi said...

Nawashukuru wote kwa kujaribu kunielekeza panapopatikana hivyo vitabu, lakini naomba nikiri kuwa sijafanikiwa kuvipata na bado Mzee Mkundi anaendelea kuvitafuta.
Safari ya kuvitafuta hivyo vitabu tulianzia chuo kikuu kwenye makataba yao lakini hatukufanikiwa, tukajaribu katika maduka kadhaa hapa mjini, pia hatukufanikiwa, na bado hatujakata tamaa, kuna mtu alinishauri kuwa huenda vikapatikana kwenye maktaba ya Hayati baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, lakini sijui ilipo hiyo maktaba yake, kwani inasemekana kuwa alikuwa ni msomaji mzuri wa vitabu na pia mtunzaji mzuri wa kumbukumbu, naambiwa alikuwa na vitabu vingi sana.

Kama ningefanikiwa kuvipata kwenye makataba yake labda ningeweza hata kuvidurusu.
{Photo Copy}
Hata hivyo sujakata tamaa naendela kuvitafuta, na mwenye taarifa mpya basi atuwekee hapa.

Naomba msaada wenu

Gemini Mushi said...

kama vilichomwa kweli ni laana itakyomtafuna kwani vinahitajika kwa rejea. Walimu wetu waliosoma miaka ya 1970 watumie fursa hii kukusanya yaliyokuwemo na kutunga vingine vyenye hadithi, mashairi, masimulizi mbalimbali nk. mf. Mambo yote ya Juma na Rosa, Lusi na Luka, Manenge na mandawa, nyoka na jongoo, babu na Luka, Sadiki na Sikiri, Nondo Mla watu, Sizitaki hizi Mbichi, Kama mnataka Mali mtaipata shambani, nk. Mimi niko tayari Kuungana na watakaoamua kukusanya yaliyokuwemo kuwakumbusha ninayokumbuka.Vitabu hivyo vinatufaa kufufua huu mfumo wetu wa elimu uliochanganyikiwa.

Unknown said...

mmenikumbusha mbali saaana miaka ya 1981-1987 nilipokuwa nasoma shule ya msingi Kishoju kata ya Mubunda Wilaya ya Muleba nilikuwa nimekaririri vichwa vya habari kama BENDERA YA TANU,AHADI ZA MWANA TANU,MAISHA YA NYUMBANI,SADIKI NA SIKIRI,MWENGE,TWENDE TUKAWINDE,ADUI WA AFYA,MATIBABU UCHAGUZI SHULENI,NUNDA MLA WATU,JOGOO ALIYESEMA,SABASABA,MUSA MTOTO SHUJAA,MIIKO YA WATAZANIA,KUJITEGEMEA KIJIJINI,USIKU WA MBALAMWEZI,SISI SOTE NI NDUGU,KIJIJI CHETU,
Nkivuiopata nitamshukuru Mungu sana,wenye navyo tuambiazane 0719527499/0763484571

Anonymous said...

Kulikuwa na kisa cha KIJIBWA CHA MZUNGU ndani ya kitabu cha UJINGA WA MUAFRIKA.kilikuwa kitabu kizuri sana.

Unknown said...

Wapi mnapatikana