Sunday, February 28, 2010

CHOZI LA MWANAMKE!

Kuzaa kwa shida

Kulea kwa shida

Kutafuta maji kilomita kadhaa tena ya kisima


Kutafuta kuni kilomita kadhaa

Kupikia familia zao

Kilio cha mwanamke wa Kiafrika ni nani akisikie!?

Ndugu wasomaji leo wakati natokea Karatu kuja Arusha mjini, njiani nilikutana na wanawake wakiwa katika shughuli zao za kila siku katika kuhudumia familia zao, nilikutana na wanawake wakitafuta kuni, wako waliokuwa wakitafuta maji tena umbali mrefu. hiyo ilinikumbusha madhila wayapatayo wanawake wa vijijini ambao wanaishi katika mazingira magumu ajabu, halafu tunaambiwa eti kuna usawa, utoke wapi?


10 comments:

Anonymous said...

Mungu atosha.
Picha nyingi sana za matukio ya wanawake na akina mama huwa zinaniacha na simanzi kubwa sana. Iko picha moja nimeoina kwenye blogu ya Mroki Mroki (Father Kidevu) inamwonesha bibi mmoja mkoani Kilimanjaro akiwa na mkongojo na mkono mwingine shavuni, chozi limenidondoka kwa uchungu usio na sababu, mwishowe husema, Mungu atosha, ninawiwa kusaidia kwa kila namna ninayoweza. Mungu atosha.

Jacob Malihoja said...

Nani kama mama!

Watu wote wanajua hili lakini mfumo dume ndio chanzo cha yote haya!

Ila Koero, usikonde! mimi nasikia kilio cha akina mama! na kwa muda sasa machozi yao nayakinga kwenye bakuli na nitakwenda kuyamwaga pale kwenye viti vyekundu kwenye ule mjengo ili yeyote atakaye endeleza ufisadi ambao ndio chanzo cha machozi ya mama na alaanike! niombee nipate nauli!

Na Tanzania itakuwa mfano! inauma sana!

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli inaumiza sana jinsi wanaweke tunavyoteseka. Sijui hii ni laana. Nashindwa hata la kusema maana ni kweli watu tunalia na tunalia lakini......basi ngoja niache kwani chozi lanidondoka hapa sioni kitu..

Mija Shija Sayi said...

Yasinta si laana wala nini, ni kwa sababu wanawake tumezidi kulialia sana na kupenda upendeleo. Kwa ufupi sisi wenyewe tunayataka, hebu angalia uwezo tulio nao wa kuyakabili maisha, kuanzia zoezi zima la mimba hadi kuzaa, kuitunza familia peke yetu huku waume zetu wakiwa vilabuni, kudunduliza vijihela vidogo tulivyo navyo hadi kusomesha wanetu na mengi mengine.

Kama yote haya tunayaweza tujue hata machozi tunaweza tukajifuta wenyewe tusisubiri kufutwa, ni suala la kuamua na KUJIAMINI tu.

Tusikubali na tusikubali kwa vile:-Nia tunayo na Nguvu tunazo za kuweza kumuangamiza huyu adui UWOGA.

Subirini niingie madarakani.

Albert Kissima said...

Dada Koero, yawezekana kabisa wanawake hao walikuwa wanakabiliana na hali halisi ya mazingira yao,ninamaanisha kwamba hali hiyo wasingeweza kuikwepa kulingana na mazingira yao. Je, unafahamu waume zao walikuwa wapi kwa wakati huo? Yawezekana kabisa kuwa kuna mgawanyo wa majukumu kiasi kwamba waume wao nao walikuwa ktk mazingira fulani wakipigika vilevile na pengine kwa kazi wazifanyazo ungeweza tena kuwahurumia mara mia zaidi. Kwa hiyo kabla ya kusema wanawake hao wananyanyasika ni vema pia tukajua upande mwingine nao unafanya nini na kama hakuna mgawanyo sahihi wa majukumu pia ijulikane.

John Mwaipopo said...

au inawezekana koero uliwaona wanawake wajane tu. huko ulikopita hakukuwa na wanaume? na kama wakikuwako wakikuwa wanacheza karata ama wanakunywa pombe? kama walikuwa wakistarehe, basi tuna haja ya kuwalilia wanawake watesekao. nasema watesekao maana wengine wanatesa kutegemea jamaii na jamii. kule tanga na pemba mwanamke haruhusiwi kufanya kazi ama hata kwenda sokoni kufanya manunuzi. kazi yake ni kupaka hina kila mtindo na kujifukiza udi na kula kungumanga. mchangiaji mmoja ameongelea pengine ni mazingira yao ndio yanawalazimu kufanya hivyo. hebu tujuze waume zao walikuwa wapi na wakifanya nini.

hilo la kubeba mimba na kuzaa tutamuuliza mungu siku ikifika.

Mzee wa Changamoto said...

Ouch!!!!
Heaven Help Us All

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Mnalitazama hili suala kwa mtazamo na mantiki gani? Mmejaribu kuongea na akina mama hawa wakawaambia kwamba wana shida? Kuweni makini na jambo hili ili msije mkaingia katika mkumbo ule ule wa 'wataalamu" wa Anthropolojia na Historia kutoka Ulaya waliofikia majumuisho (generalizations0 ya kushangaza walipotia guu lao Afrika kwa mara ya kwanza!

Nendeni mkaongee na wanawake hawa kwanza. Mtakayojifunza huko yatawashangaza na pengine yatabadili maoni yenu kabisa. Nina mifano mingi ya ninachokisema hapa!

Mija Shija Sayi said...

Hii ndiyo raha ya kublogu jamani, tunajifunza mengi. Mwl Masangu umeongea jambo la msingi sana.

Anonymous said...

You ran away from UDSM claiming that the education there is NO good. It is beginning to show now; and you will live to regret that decision of yours regardless of whether you are rich or not.

Probably people don't understand you because your articles are superficial, emotional and half cooked. If you had stayed at Mlimani ant took classes on Philosophy, Psychology and Fundamental Statistics/Logic, it would have helped you a lot - not to become rich but kupanua akili yako and your thinking capacity.

Punguza kupiga makelele. There is a reason people don't understand you. Your mother was right; and she will always be right. You need to go back to school girl!!!