Ndugu wasomaji wa kibaraza hiki, leo nataka tujifunze namna ya kuomba maji kupitia lugha za makabila tofauti tofauti.
Hivi karibuni nilikwenda Wilayani Babati, kule nikakutana na watu wa kabila moja liitwalo Wasandawi, nilikuwa na kiu, lakini nilipata tabu sana kuomba maji maana lugha pekee ambayo nilitakiwa kuwasiliana nao ilikuwa ni Kisandawi, basi ilikuwa kaazi kweli kweli.
Kipare:
Nighenja mazi ya kunwa=Nisaidie maji ya kunywa
Kinyawezi:
Nalilomba minze kakunwa=Naomba maji ya kunywa
Kichaga:
Ngikundi Mringa= Naomba maji ya kunywa
Kingoni:
Nitangatilai manji mlongo wangu=Naomba maji ya kunywa ndugu yangu
Kimasai:
Njaaghe Ngare= Naomba maji ya kunywa
Kihehe:
Ndisuka Ululenga= Naomba maji ya kunywa
Kimeru:
Ngitelewa Mringa= Naomba maji ya kunywa
Kijaluo:
Miaa pi= Naomba maji ya kunywa
NIMEPATA MSAADA KWA MJUVI WA LUGHA YA KIJAPANI
Kijapani:
Kwanza inabidi useme:- 1. kao nodo itai - nina kiu
2. mizu nomu itai - nina hamu ya kunwya maji
Ukisha sema moja kati ya hayo hapo juu ndio unaunganisha na lingine kati ya haya hapa:-
1. omizu kudasai
2. omizu chodai
3. omizu onegai shmasu
Kihaya:
Ninshaba amaizi= Naomba maji ya kunywa
Haya wengine mtajazia hapo.
17 comments:
Heee! wa msikana veve unileki hoi! Nimenukuu "Kingoni:
Nitangatilai manji mlongo wangu=Naomba maji ya kunywa ndugu yangu"
Pia unaweza ukasema nimwomba manji gakunywa.= naomba maji ya kunywa
Na halafu Kimanda Nisuka manji gakunywa= Naomba maji ya kunywa
Kisukuma (Kinyantuzu) - Nalilomba minzi agung'wa au nagulombaga minzi agung'wa
Samahani hapo kwenye Kimanda nilikosema unajua kinafanana sana na kingoni Ni hivi Nisuka masi gakunywa. Na pia kwa kiswid ni:- Kani jag be att får ett glas vatten
Kijita atasema mt simon....lol
Kisimbiti: Ndasabha amanshe ghukunywa
Dada Yasinta, hicho Kiswidi, naomba utufundishe namna ya kutamka kwa kiswahili, maana mwenzako huku ulimi umeteguka
Koero, kwa jinsi ulovyo andika kijapani Watashi wa ina maana mimi
omizu maji, kwa jinsi ulivyo andika ina maana MIMI MAJI
@ Mumyhery DUH!
Yaani ndughu dhangu wapare wao hawajui kuomba ila kuthaidiwa thu!
Love this post
Burrrrdaaani na hazina ya lugha zetu!
NIGAILE MACHI YA KUNYUWA - naomba maji ya kunywa. Ifakara hiyo ila sijui ni kimbunga, kindamba au kipogoro na kwa kizulu NG'ICELA AMANZI - naomba maji
Kimatengo: "Naa masi ga kuunywa."
Mie simo
Kidachi, Ik wil water om te drinken, au Kan ik heb water te drinken.
**'Wil' tamka vil, na 'Water' tamka 'Vata'
okey Koerounataka matamshi ya kiswid kwa kama kiswahili yaani kan jag be att får ett glas vatten utatamka hivi:- kani yogu be ati forr eti glasi vatteni.
Kama mwanaisimu, hapa nimefaidika sana!
Dada Yasinta samahani naomba nikukosoe kidogo kwa kuwa wote tunaelimishana.
Hapa unalewa kusema:
Kan jag få ett glas vatten?
Ukitaka kutumia lugha ya upole utasema:
Skulle jag kunna få ett glas vatten?.
Nipo likizoni Dar. Napatikana kwa namba 0716 333270
Skulle jag kunna få = could I have/receive
Dada Yasinta samahani naomba nikukosoe kidogo kwa kuwa wote tunaelimishana.
Hapa unalewa kusema:
Kan jag få ett glas vatten?
Ukitaka kutumia lugha ya upole utasema:
Skulle jag kunna få ett glas vatten?.
Nipo likizoni Dar. Napatikana kwa namba 0716 333270
Skulle jag kunna få = could I have/receive
Tang'a amanche gakunywa (kikurya)
Post a Comment